Uganda yapitisha sheria mpya kukataza wanawake kuvaa nguo fupi

Uganda yapitisha sheria mpya kukataza wanawake kuvaa nguo fupi

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
MAADILI UGANDA:Uvaaji vimini, kubaki nusu uchi sasa ni kuvunja sheria nchini humo, rais Museveni asaini sheria inayobana vitendo vya ngono vinavyoharibu maadili.
140219081848_africa_miniskirt_304x171_bbc_nocredit.jpg


Maandamano ya kkupinga agizo la wanawake kutovalia sketi fupi

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.

Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .

Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha.

Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.

Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.

Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.

Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
source: BBC
 
Taasisi ya Urais Uganda ni Taasisi ya mtu mmoja, ana uhuru wa kuendesha nchi atakavyo, sijashangaa kesho ikipitishwa amri ya kutotabasamu hadharani!
 
MAADILI UGANDA:Uvaaji vimini, kubaki nusu uchi sasa ni kuvunja sheria nchini humo, rais Museveni asaini sheria inayobana vitendo vya ngono vinavyoharibu maadili


mcl

Aje na huku amuambukize presida wetu hiyo sera. Keros sana. Natamani niendelee kuleta watoto KIUME Tuuu.
 
Kweli tuna imani zetu za dini, lakini kama mtu atajiamulia kuvaa kimini, asikutie wasi/shaka afadhali angekuwa anatoka(mmojawapo) katika familia yenu sawa, hapo mnaweza kuingiliana mipaka, lakini sio mtu asiekuhusu
 
Taasisi ya Urais Uganda ni Taasisi ya mtu mmoja, ana uhuru wa kuendesha nchi atakavyo, sijashangaa kesho ikipitishwa amri ya kutotabasamu hadharani!

Labda, lakini hii ni sheria sio amri ya rais, imepitishwa na bunge! Pia walipitisha sheria ya adhabu ya kifo kwa mashoga Museveni akakataa kusaini.
 
kutetea vimin ni kutetea uzinzi na umalaya.unaanika uchi nje nje halafu mnalalamika "ooh wanaume wa kibongo sio waaminifu" ooh wanaume hawaliziki kabisa hata umfanyie kila kitu.

Tuache ubishi kuzaliwa mwanaume ni faida!!
 
Kwani kwetu si ipo? Ukimkonyeza demu bila ridhaa yake unaweza kufungwa miaka 30. Sheria zipo tu ila haziwahusu akina Kapuya. Zikifuatiliwa hata Presidaa anaweza pigwa mvua za kutosha .
 
Kweli tuna imani zetu za dini, lakini kama mtu atajiamulia kuvaa kimini, asikutie wasi/shaka afadhali angekuwa anatoka(mmojawapo) katika familia yenu sawa, hapo mnaweza kuingiliana mipaka, lakini sio mtu asiekuhusu


Acha ujinga wako hapa, jitahidi siku zingine mtu kuuficha ujinga wako usiuweke hadharani, hizo nguo za kulalia watu ndo wamefanya za kutembelea, nguo za CLUB za usiku ndo zimekuwa za kutokea, sema wewe ni limbukeni na haya mambo umeyaanza ukubwani ndio maana unaona raha. sasa nakwambia haya mavazi ni sawa na uchafu yanatia kinyaa kama vile mtu analamba usaha wa kidonda ndugu
 
Back
Top Bottom