Habari wanaJF,
Ni muda nimekuwa kimya humu, lakini kuna jambo muhimu limejitokeza jirani zetu
Uganda ambalo lina
uhusiano wa moja kwa moja na kile tulichokiona Tanzania wakati wa uchaguzi β hasa kwenye masuala ya
intaneti na udhibiti wa mawasiliano.
Uganda imetoa
zuio la uingizaji wa vifaa vya Starlink, likihitaji
kibali cha maandishi kutoka kwa Mkuu wa Majeshi (UPDF) kabla ya vifaa hivyo kuruhusiwa kuingia nchini. Nakala hii hapa:
Haya yametokea
wiki 2 tu kabla ya uchaguzi mkuu.
Hebu tuangalie:
- kilichotokea,
- kwa nini hili ni jambo kubwa,
- na linatuambia nini kuhusu mustakabali wa intaneti Afrika (ikiwemo Tanzania).
Kilichotokea Uganda (Desemba 2025)
- π Mamlaka ya mapato Uganda (URA) ilitoa waraka rasmi kwa maafisa wa forodha.
- π« Waraka huo unazuia uingizaji wa Starlink na vifaa vyake vyote bila kibali cha kijeshi.
- πͺ Kibali kinapaswa kutoka kwa Chief of Defence Forces β UPDF.
- β±οΈ Maelekezo yameanza kutekelezwa mara moja.
- π³οΈ Haya yote yanatokea wiki 2 tu kabla ya uchaguzi mkuu.
Kwa ufupi, Starlink hairuhusiwi kuingia Uganda bila ruhusa ya jeshi.
Starlink Ina Tishio?
Starlink ni intaneti ya
setilaiti. Haitegemei minara ya simu, mkongo wa taifa, au kampuni za simu za ndani.
Inarusha mawimbi moja kwa moja kutoka angani hadi kwa mtumiaji.
Ndiyo maana:
- inafanya kazi hata maeneo ya vijijini,
- ni ngumu kuzimwa kwa njia za kawaida,
- na imekuwa mbadala wakati wa internet shutdowns.
Ndo maana wenzetu waliokuwa nayo (waandishi wa habari kutoka Kenya, Marekani na kwingineko), waliweza kuendelea kupata huduma wakati kwa uchaguzi. Na pia providers wengine kama Konnekt Afrika walikuwa hewani muda huo wote.
Kwa uzoefu wa hivi karibuni,
kuzima intaneti wakati wa uchaguzi si ajali. Zamani tuliona wenzetu wakizimiwa. Tujikumbushe baadhi yya matukio:
- πΊπ¬ Uganda (2016, 2021): intaneti ilizimwa wakati wa uchaguzi (total shutdown).
- π¨π² Cameroon: intaneti ilikatwa kwa miezi kadhaa.
- πΏπ¦ Zimbabwe, πΈπ³ Senegal: throttling wakati wa maandamano.
- πΉπΏ Tanzania (2025, internet ilituacha):
Serikali nyingi huchukua njia mojawapo kati ya hizi:
- β kuzima mtandao (Oktoba 29),
- π kupunguza kasi (throttling - kwa mliokuwa makini internet ilisua sana tarehe 9),
- π« kuzuia apps kama WhatsApp, Facebook, X, YouTube, JamiiForums.
Lakini Starlink, kama mitandao mingine, haitegemei mkongo wa taifa, haidhibitiwi kirahisi na mamlaka za ndani, hivyo inavunja βcontrol pointβ ya serikali.
Athari Kwa Wananchi wa Kawaida
Hili si suala la siasa pekee. Linagusa:
- πΌ Biashara za mtandaoni
- π§βπ» Online workers (kama mimi)
- π« Elimu ya mtandaoni
- ποΈ Upatikanaji wa habari
- π¨βπ©βπ§ Mawasiliano ya kifamilia
Kile kinachoendelea Uganda kinatufundisha jambo moja muhimu:
Vita vya uchaguzi sasa si kura pekee β ni vita vya miundombinu ya intaneti.
Kadri teknolojia mbadala zinavyoibuka ndivyo serikali zinavyobadilisha mbinu, kutoka kuzima mtandao, kwenda kudhibiti nani anaweza kuwa na intaneti huru.
Intaneti leo si anasa. Ni hitaji muhimu kama maji, barabara, au umeme. Na kinachoendelea Uganda (baada ya Tanzania) ni
ishara ya kinachokuja mbele (the new normal).
Umejipangaje kwa hali hii mpya?