Fisadi.Jones
Senior Member
- Aug 15, 2008
- 110
- 7
Nashukuru kwa mawazo, yawezekana hobbies haziendani. Nasiwezi kujilazimishia kuiga hobbies zake! Na zaidi ya hapo naoana anapenda magenge kama chokoraa. Mtu asiyekuwa na discipline na kuithamini ndoa yake ni kama chokaraa.
Du! Jamani, kabla hujamuoa mtu au hujaolewa na mtu tafadhali jaribu kumjua. Ukishamjua ndio uamue upo tayari ama la. Ukiyajua mapungufu ya mtu kabla ni bora kwa sababu ukiingia ushajipanga kuvumilia.
Kama ni uchokoraa kuna uwezekano huyo jamaa alikuwa nao toka zamani. Pengine sio yeye aliyebadilika ... bali ni wewe ndio umebadilika, macho yakafunguka, na kuanza kutambua uwepo wa uchokoraa wake.
Chonde chonde jamani mjue mwenza wako kabla hujasema "nakubali".
Mshakaji wangu mmoja aliolewa na jamaa hivyo-hivyo, akaja kugundua wakati wapo ndani kwamba jamaa anamatatizo ya kukojoa kitandani. Kazi kwelikweli ...
Kwa wale madume wenzangu tunaojidanganyaga kwamba the past history does not matter ... ushauri wangu ni kwamba chunga sana. Ukawii kuanza kujilaumu
Kama unaweza tumia hata usalama wa taifa kumjua mtu wako. Na wewe jitahidi mwenza wako akujue fika, nje ndani. Maana inawezekana wewe una lalama na hili, kumbe na yeye anayakwake moyoni.
Rule 1: Mjue mwenza wako, ikiwezekana kabla hata hujamchanulia, unless you are not there for the long haul ... in which case u can always quit badala ya kulalama