Ugenini jitahidi kati ya rafiki zako basi awepo mbea mmoja na mropokaji mmoja watakusaidia kijasusi

Ugenini jitahidi kati ya rafiki zako basi awepo mbea mmoja na mropokaji mmoja watakusaidia kijasusi

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
UGENINI JITAHIDI KATI YA RAFIKI ZAKO BASI AWEPO MBEA MMOJA NA MROPOKAJI MMOJA WATAKUSAIDIA KIJASUSI.

Yawezekana ukaona ni kinyume kwa sababu wengi husema hao marafiki hawafai ila kijasusi wanafaa sana muhimu tu uishi nao kwa akili kubwa sana yaani utumie madhaifu yao kukunufaisha wewe .

Iwe eneo la kazi, mtaani ama kwenye jumuiya yoyote sio mbaya ukiwa na rafiki mmoja Mbea na Mropokaji mmoja ila wasijue kama lengo lako ni kutaka wakunufaishe na wala usiruhusu wajue taarifa zako ambazo zikisambaa zitaleta shida na hapo utakuwa kwenye hatua nzuri ya kunufaika na watu hao .

RAFIKI MBEA

Sifa ya Mbea ni kutafuta habari fiche na kusambaza hivyo basi kwa tabia yake hiyo atakusaidia kujua:
1.Kujua mifumo mbalimbali ya ugenini.
2.Kuwajua watu na siri zao.
3.Kujua njama ovu dhidi yako.
4 .Kujua kipi kiliendelea dhidi yako kipindi haupo.

RAFIKI MROPOKAJI.

Sifa kubwa ya huyu ni kuongea bila kufikiria anaongea wapi na nani , huyu atakusaidia:
1.Kuropoka siri za watu.
2.Kuropoka taarifa ambazo ulifichwa.
3.Kuropoka madhaifu ya wengine hivyo kukusaidia wewe kuwafahamu wenyeji wako vizuri.

TANBIHI: Mbea na Mropokaji ni watu hatari sana kwako pia hivyo nasisitiza ishi nao kwa akili kubwa ili wakunufaishe wewe kijasusi.

#Mwanasayansi Saul kalivubha
Instagram @fikia ndoto zako.
 
Uhakika wana faida kubwa na hasara chache lakini hatari kabisa
 
Maisha ni ubatili hata ujifanye unasiri vip siku ukifaaaa tutasomewa siri zako
 
Haya sasa watu wa Mbeya na viunga vyake tumefikiwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom