Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Huu ugomvi wa Yanga na Kagame ulianza mwaka 2012 Mara baada ya Yanga kwa nguvu kubwa kushinda Kagame Cup ili Yanga ipate nafasi ya kwenda kuonana na Kagame... toka mwaka huo baada ya kutoelewana naye Yanga haijashiriki Kagame Cup kwa visingizio lukuki kila mara linapokuwepo Kombe la Kagame ili kumkomoa kutokana na kilichotokea huko ambacho ni dhahiri hakikuwa na manufaa kwa Yanga au hawakuwa na kukubaliana. na mwaka huu haitashiriki tena ili kumkomoa Kagame na kombe lililopewa jina lake. ni aina fulani tu ya siasa ambayo inarudisha nyuma mpira wetu kwa sababu ambazo ni binafsi za mtu mmoja. ningewashauri yanga washiriki kombe hili ili kujipa mazoezi na kujipima wakijiandaa na mashindano ya kimataifa hapo mbeleni.