Binti Magufuli
JF-Expert Member
- Apr 2, 2011
- 7,479
- 5,157
Nakaaya, ambae ni dada wa Nancy Sumari, amemjibu Mange kuhusiana na uzi aliouweka kwa blog yake kuhusu ndugu hawa kuwa mbuzi na chui. Uzi ule ulionekana kuelemea kwa Nancy Sumari kwani ulionesha wazi wazi kwamba yeye ndio tatizo, kwani aliiba mchumba wa dada yake na pia anamdharau dada yake kwa vile hana utajiri kama ilivyo kwa Nancy. Sasa picha hizi ni majibu ya moja kwa moja toka kwa Nakaaya kwenda kwa muke ya muzungu.
Mnasema ni mambo ya kifamilia ....ni kweli ila Nakaaya na Nancy tambueni nyie ni watu maarufu Tanzania hivyo kuandikwa kwa mema au mabaya ni lazima. Yawe ya kifamilia au kikijiji. Kugombana kupo kwa kila mtu ila namna ya kumalizana ndio swala muhimu. Muhimu jifunzeni namna ya kumaliza mambo yenu mapema kabla hayajafika kwa watu.