Tajiri wa kusini
JF-Expert Member
- Nov 28, 2022
- 1,079
- 2,947
UGOMVI WA NYAMA YA KENGE WASABABISHA MAUAJI MASASI MTWARA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limefanikiwa kuzuiya na kutanzua uhalifu kupitia operesheni na misako iliyoendeshwa kati ya tarehe 1 Desemba 2024 hadi 31 Desemba 2024. Katika operesheni hiyo, walikamata wahalifu wakiwemo watuhumiwa wa mauaji, kulawiti, wizi, na uhalifu mwingine, pamoja na kupata pombe haramu na dawa za kulevya.
Miongoni mwa matukio makubwa, watuhumiwa wawili, Danford Steven Seif na Daniel Steven Seif, mapacha wa umri wa miaka 24, walikamatwa kwa tuhuma za kumuua mama yao, Upendo Methew Mayaya, kwa kumshambulia kwa jembe na mwichi. Chanzo cha mauaji hayo kilikuwa ni imani za kishirikina.
Aidha, Renard Godfrey Ndonjima (62) alikamatwa kwa kumua Mohamed Kapile (52) baada ya kutokea ugomvi kuhusu nyama ya kenge, tukio lililotokea tarehe 22 Desemba 2024.
Katika operesheni hiyo, polisi walikamata watuhumiwa saba wakiwa na kete 61 za dawa za kulevya aina ya bhangi, lita 20 za pombe haramu (gongo), na mitambo ya kutengeneza pombe hiyo. Watuhumiwa walifikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara alishukuru wananchi kwa ushirikiano wao na kuwataka kuendelea kutoa taarifa za uhalifu ili kudumisha usalama katika jamii.