Ugomvi wa zuberi mtemvu na julius nyerere 1958

Ugomvi wa zuberi mtemvu na julius nyerere 1958

One thing for sure Mtemvu alikuwa mzalendo kupita wwatu wengi mno
 
Maashallah,mwandishi umenisaidia kupata
elimu ya ziada ambayo sitoipata pengine,Allah akuweke na akupe siha njema utupe vitu kama hivi
 
Ni yapi yalikuwa maisha ya Mtemvu baada ya kuanzisha chama chake, na ilikuwaje akapotea kwenye siasa za Tanganyika, na kipi kilifanyika baada ya kufutwa vyama vingi

Asante

achcha kumtabiria zitto mabaya sio vizuri banaaaaaa
 
Ule mkutano uliofanyika Tabora ulipo-mention kuwa umefayika Parish ya katoliki unamaanisha kuwa kuna influence yoyote ya sehemu ulipofanyika mkutano na maamuzi yaliyofikiwa au ndo kama kawaida yako na nyimbo zako za udini?

Captain Phillip,
"Nyimbo za udini" zangu mimi ndiyo zipi?

Ungependa kuwajua wadini?

Msome Njozi (2012).
Msome Bergen (1981)
Msome Sivalon (1992)

Kwa makusudi sikumweka Said (1998)

Ukishawasoma rudi hapa Majlis tujadili udini.

La hukuweza kupata hivyo vitabu au umeshindwa kwa njia yoyote
ile kusoma nieleze nikuwekee hapa ushahidi wa huo udini na viongozi
wake wakuu.
 
Hakika hii ni elimu tosha.Jazaaka LLAHU KHAYRAA.
 
Kwanini Abbas Mtemvu hakufwata nyayo za babake na akajiunga na hao hao TANU (CCM)... Kama sio unafki ni nini??
 
Kwanini Abbas Mtemvu hakufwata nyayo za babake na akajiunga na hao hao TANU (CCM)... Kama sio unafki ni nini??

Kaka haya mambo kuyasema ni rahisi hivi wewe ulishafanya kitu ukakosea?, ama unajua ni shida zipi baba yake mzee zuberi mtemvu alizipitia?,

najua hata yeye alirudhia mwanae kuingia ccm kwan sidhan aliingia ccm baada ya baba yake kufa mwaka 1998..........

ccm siipendi nacho jaribu kusema hapa si kazi rahisi kuwa mpinzani hasa kwenye hizi nxhi ambazo demokrasia zake bado ni za kuunga unga.
 
Kwanini Abbas Mtemvu hakufwata nyayo za babake na akajiunga na hao hao TANU (CCM)... Kama sio unafki ni nini??

Kumbuka enzi za Mh.Abbas Mtemvu chama kilikuwa kimeshika hatamu (CHAMA KIMOJA)
Na ili uendelee kimasomo lazima uwe mwanachama wa CCM. Pia kupata scholarship,Passport n.k.

Baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi Mh.Abbas Mtemvu aliwahi kujiunga na chama cha upinzani kabla ya kuanza kuona mambo yanamuendea MRAMA ndio aka-ufyata na kurudi CCM.
 
Kaka haya mambo kuyasema ni rahisi hivi wewe ulishafanya kitu ukakosea?, ama unajua ni shida zipi baba yake mzee zuberi mtemvu alizipitia?,

najua hata yeye alirudhia mwanae kuingia ccm kwan sidhan aliingia ccm baada ya baba yake kufa mwaka 1998..........

ccm siipendi nacho jaribu kusema hapa si kazi rahisi kuwa mpinzani hasa kwenye hizi nxhi ambazo demokrasia zake bado ni za kuunga unga.

Mbona kuna kijana wa Nyerere alikuwa upinzani na hata Ubunge aliupata??

Mbona akina Mtei walifukuzwa serikalini kwa mitazamo yao kuonekana ni hasi lakini walirudi mtaani na kuanzisha vyama ambavyo sasa vina nguvu kubwa i.e CDM

Huyo Zuberi ambaye hapa anasafishwa kiaina imekuaje akashindwa?? si alikuwa shupavu?? si alikuwa anapendwa na jamii yake?? Hapo ndio napoona kuna unafki mtupu kwenye hii thread ya kutaka kuwachafua watu wengine na kupandikiza kila ambacho huyu mpuuzi anakipandikiza kila anapokuja na hizi hadithi zake..
 
The Boss,
Kuna Sitti Mtemvu Kilungo ambae alikuwa mke wa Mzee Zuberi
Mtemvu
na kuna Sitti Mtemvu binti yake Mheshimiwa Abbas
Mtemvu
.

Napenda sana Bw.Mohamed Said unavyoichambua vizuri historia na kufanya msomaji kujisikia kuuvaa uhusika ... Haswa pale ulipotuelezea habari ya msiba wa shangazi yake Ally Sykes. Sipendi watu wanapokukosoa unapoandika ukweli ambao lazima ubebe uhalisia kuwa bila ya jitihada za Wana-Dar es Salaam wengi Waislam... TANU isingeweza kujipenyeza Tanganyika.
 
Kumbuka enzi za Mh.Abbas Mtemvu chama kilikuwa kimeshika hatamu (CHAMA KIMOJA)
Na ili uendelee kimasomo lazima uwe mwanachama wa CCM. Pia kupata scholarship,Passport n.k.

Baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi Mh.Abbas Mtemvu aliwahi kujiunga na chama cha upinzani kabla ya kuanza kuona mambo yanamuendea MRAMA ndio aka-ufyata na kurudi CCM.

Haswaa huo ndio unafki ninaouzungumzia mkuu.. Kuna watoto wa Nyerere mpaka leo wako upinzani, vipi mambo wao hayawaendie MRAMA??

Akina Mtei walifukuzwa Benki Kuu lakini sasa wana vyama vya siasa imara.. Kuamua kuwa upinzani unatakiwa u sacrifice vitu vingi mkuu, Au walitaka wakiingia Upinzani mara moja wachukue nchi?? Prof Lipumba is a mentor pamoja na Uprof wake angeweza kuwa sehemu kubwa hapa nchini lakini amesacrifice that na kwa miaka 20 sasa bado hajakata tamaa.. Huyo Mtemvu imekuaje?? Ndio hao tunaosema wanasiasa wa kimaslai tu
 
Kwa kweli unanikosha sana na mada zako, Mungu akubariki
 
Mbona kuna kijana wa Nyerere alikuwa upinzani na hata Ubunge aliupata??

Mbona akina Mtei walifukuzwa serikalini kwa mitazamo yao kuonekana ni hasi lakini walirudi mtaani na kuanzisha vyama ambavyo sasa vina nguvu kubwa i.e CDM

Huyo Zuberi ambaye hapa anasafishwa kiaina imekuaje akashindwa?? si alikuwa shupavu?? si alikuwa anapendwa na jamii yake?? Hapo ndio napoona kuna unafki mtupu kwenye hii thread ya kutaka kuwachafua watu wengine na kupandikiza kila ambacho huyu mpuuzi anakipandikiza kila anapokuja na hizi hadithi zake..

Kaka nimekusoma........
ila kila ekimu inafaidazake hatakama kusudio lake ni siri...
 
Stephen Curry,
Hapana haja ya matusi.
Hapa tunashindanisha hoja tu.

Tuko barzani waungwana tunazungumza.
Wala hakuna asiye na akili kiasi apandikizwe fikra.

Ikiwa historia hii ambayo haikuwapo kwa miaka mingi inakuchoma
jiepushe na Majlis hii lakini si adabu wala uungwana kuja hapa
kutukana watu.
 
Ahsante historia nzuri ukitaja mitaa ya gerezani na tabora nakumbuka mengi miaka ya nyuma na mandhari za maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom