Ugomvi wa zuberi mtemvu na julius nyerere 1958

Ugomvi wa zuberi mtemvu na julius nyerere 1958

Napenda sana Bw.Mohamed Said unavyoichambua vizuri historia na kufanya msomaji kujisikia kuuvaa uhusika ... Haswa pale ulipotuelezea habari ya msiba wa shangazi yake Ally Sykes. Sipendi watu wanapokukosoa unapoandika ukweli ambao lazima ubebe uhalisia kuwa bila ya jitihada za Wana-Dar es Salaam wengi Waislam... TANU isingeweza kujipenyeza Tanganyika.

Tusker...
Historia hii ni historia yangu.
Nimekua wakati wa historia hii ilipokuwa inajitengeneza.

Hao ninaowataja ni baba na shangazi zangu nikiwajua kwa karibu.
Hakika bila ya wazee hawa uhuru ungechelewa sana.
 
Mzee Mohamed Said hiyo historia uliyoieleza ni kama ilivyo,alivyokuwa anaelezea Zuberi Mtemvu . Mie nina undugu na ukoo wa Mtemvu kwa upande wa mama.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohamed Said hiyo historia uliyoieleza ni kama ilivyo,alivyokuwa anaelezea Zuberi Mtemvu . Mie nina undugu na ukoo wa Mtemvu kwa upande wa mama.
Medisonmuta,
Ahsante kwa kunisadikisha ndugu yangu.

Mimi Mzee Mtemvu ni baba yangu kwa kuwa mwanae Abbas tukifahamiana
miaka mingi na mama yake Abbas Bi. Sitti Kilungo alikuwa shoga wa
marehemu mama yangu na walikuwa majirani udogoni.

Bi. Sitti akiishi Kirk Street (sasa ni Lindi Street) na mama yangu Kipata Street
(sasa ni Kleist Sykes Street).

Kama isingelikuwa udugu kama huu ningelipata tabu sana katika utafiti wa
historia hii na mchango wa Abdul Sykes katika TANU.

Wakati ule watu wakiogopa sana kuhadithia historia ya kweli ya TANU.

Ilikuwa wepesi hawa kuzungumza na mimi kwa kuwa kwa vyovyote walikuwa
na uhakika sikwenda kwao kuwachimba.
 
Back
Top Bottom