Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

Ugonjwa wa kifafa: Chanzo, Dalili, Huduma kwa Mgonjwa na Ushauri wa Matibabu

pole sana domy. ila jitahidi sana kumfuatilia mtoto kwa karibu. ukiona badiliko kidogo waone wataalam. watoto wanabadilika kama vinyonga take care sana.

Asante kiongozi....
 
Pole sana kaka. Mungu amemponya. Hilo ni somo kwetu kuhusu afya za watoto wetu.
 
Habari Wadau,

Leo asubuhi nimejikuta katika wakati mgumu pengine kuliko siku yoyote ile,Nilikuwa nimekaa na mtoto wangu akawa ananiambia baba macho yanauma,mara kichwa kinaniuma nikamgusa akawa amechemka sana mwili,nikamwambia tulia nikupeleke hospitali

Tukaendelea kupiga stor na utani mwingi,ghafla akakamaa kama mti huku akitetemeka sana,nikamwita jina akawa haitiki tena, nikamkumbatia,Nilichanganyiwa sana,Ndipo nikamkimbiza hospital lakini ametibiwa.

Nimeona si vibaya kuwashirikisha magumu yangu ya leo
Pole sana mwaya, kulea kazi. Usisahau uzazi wa mpango mwaya.
 
pole sana mpendwa kweli hiyo hali ni ngumu sana .degedege hutokana na homa kali ikipanda kuzidi 40 huwa ubongo unapata short. na hapo ndipo degedege hutokea.
Je alipoteza fahamu kwa muda wa dk ngapi?
mwanao ana umri gani?
je umepewa dawa gani?
je uko mkoa gani?
nipe majibu ya haya maswali ndipo nitakushauri la kufanya
Ndg we ni doctor au daktari?
 
Ilimchukua kama dakika kumi kupata fahamu..! Ana miaka mitatu,niko Mbeya,Dawa nilizopewa ziko mbali kidogo nimetoka nyumbani,

Kama waamini ktk mitishamba hapo mbeya mitaa ya Isanga njia ya kuelekea chunya kuna mtaalam wa hzo mambo anatibu hilo tatzo kabisa. Nashuhudia haya kuna ndugu yangu alihangaika sana hospitali hadi alipoenda pata tiba hiyo kwa mtaalam huo. Kama hali hii itaendelea waweza ulizia na kizuri zaidi hatumii shirki.
 
Hiyo ni degedege kaka, atapona tu.lakini kuwa makini sana na sindano kuna dawa za kienyeji tu simple anapona haraka tu. Watoto wengi hupitia hiyo hali usipanic sana
 
Dah pole sana mkuu yameshanikuta hayo chalii yangu alipatwa na dege dege 2004 akiwa na mwaka m1 ila tulipoenda hosp alikuwa na malaria kali na homa ilikuwa juu akatibiwa akapona na yuko poa stnd 4 sasa,kwa ushauri wangu mchek vizuri huyo chalii lazima atakuwa na ugonjwa uliosababisha
homa kupanda kwa hiyo jaribu kuchek uti na mengineyo.
 
Kamanda,huu ugonjwa usikie tu kwa watu. Juzi usiku wa manane ulimshka mtoto wangu hakika nilidhan nimempoteza!
 
Mimi mwaka jana mtoto wangu akiwa na mwaka 1 alipatwa na hali hiyo (fit) ilimtokea kama mara 7 kwa siku moja,nilimpeleka aga khan alipimwa kila kitu malaria,uti,meningtis etc lakini zote zilikua negative! Ikagundulika sababu aliharisha sana kwa hiyo madini yalipungua sana mwilini,alipewa drips na ors mambo yakawa safi,namshukuru MUNGU mpaka saizi yupo safi,pole sana Domy
 
Last edited by a moderator:
Pole ndugu.pamoja na dawa ulizopewa mtafute bingwa wa watoto amcheki mtoto toncilis na UTI hakikisha anamaliZa dozi ya dawa atakazokuwa amepewa.
pili endelea kumchunguza mwanao kama kuna madhara yaliyompata alipopatwa na hiyo degedege.

degedege ikitokea kama imechukua mda ubongo unakosa oksigen hivyo yaweza kuleta madhara kwa mtoto.

madhara hayo unayachunguza kwa kuwa karibu nae kumcheki kama inamrudia au anakuwa kama anazubaa kuliko kawaida yake.anakuwa na hasira kupita kawaida..

jitahidi kuwa na panadol(paracetamol) yumbani kila ukimuona mwanao ana joto mpe kirobo kila baada ya masaa 6 njia nyingine rahisi mwanao akiwa na homa mkande kwenye mapaja na taulo lenye maji ya vuguvugu au muogeshe ndo muwahishe kwa daktari.

usimpeleke kwenye dawa za mitishamba kama degedege litamrudia daktari atakupa phenobabiton ambayo atazitumia kila siku kwa muda wa miaka isiyopungua miwili hadi daktari atakapokuambia aache
 
Habari Wadau,

Leo asubuhi nimejikuta katika wakati mgumu pengine kuliko siku yoyote
ile,Nilikuwa nimekaa na mtoto wangu akawa ananiambia baba macho
yanauma,mara kichwa kinaniuma nikamgusa akawa amechemka sana
mwili,nikamwambia tulia nikupeleke hospitali

Tukaendelea kupiga stor na utani mwingi,ghafla akakamaa kama mti huku
akitetemeka sana,nikamwita jina akawa haitiki tena,
nikamkumbatia,Nilichanganyiwa sana,Ndipo nikamkimbiza hospital lakini
ametibiwa.

Nimeona si vibaya kuwashirikisha magumu yangu ya leo

pole sana mpendwa wangu.. nakuelewa sana.
Mwanangu alipata shida hiyo akiwa na mwaka na miezi 4, ilikuwa ni usiku wa saa tisa. Tuliamka kumpa maziwa kabla hatujalala ikatokea, sitakaa nisahau inatisha sanaa sanaa na imekaa kama mtu anakata roho.

siku hiyo nilisali sana.. kila neno nilitoa kwa kinywa changu, hosp ni mbali.. but tulienda usiku huo huo kwa kasi ya ajabu. Wakatuambia ni niumonia(spel za kisw lol) sikuridhika tukaenda aghakan tukashauriwa kumpima kichwa akakutwa ana shida kwa kichwa. yuko ktk matibabu til now.

ni muhimu kwenda kumcheki kichwa ili isimrudie tena, na ikitokea ina madhara yake pia. Unaweza kwenda regency au hosp nyingine.. kipimo wanachofanya kinaitwa EGG.

pole sn
 
Kama waamini ktk mitishamba hapo mbeya mitaa ya Isanga njia ya kuelekea chunya kuna mtaalam wa hzo mambo anatibu hilo tatzo kabisa. Nashuhudia haya kuna ndugu yangu alihangaika sana hospitali hadi alipoenda pata tiba hiyo kwa mtaalam huo. Kama hali hii itaendelea waweza ulizia na kizuri zaidi hatumii shirki.

Asante Mkuu,ushirikina ndio mbaya lakini dawa ya mitishamba kama inatibu nadhani hamna tatizo....
 
Mimi nilivaa viatu halafu
soksi nikaweka mfukoni... Kilichonichanganya zaidi mama yake alikuwa
analia as if mtoto amefariki.Sitaki kabisa hiyo hali
inarudie.....

mkuu nimecheka sio mazuri but .. nakumbuka mimi nguo ya juu nilivalia hosp. hiyo kitu haizoeleki na kama haijakukuta isikie tu kwa watu.
 
Mimi nilivaa viatu halafu soksi nikaweka mfukoni... Kilichonichanganya zaidi mama yake alikuwa analia as if mtoto amefariki.Sitaki kabisa hiyo hali inarudie.....

...Mimi hii ilinipata miaka miiingi nyuma wakati nikiishi mitaa fulani ya Migomigo.
Alikuwa ndio firstborn wangu ambaye sasa yuko chuoni.
Kuanzia jioni mtoto akawa analalamika kichwa na macho vinamuuma.
Lakini kwa vile tukimgusa alikuwa hana joto la kushitua tukadhani ni meno yanaota na lingepita.
Weee! katikati ya msosi wa saa mbili Usiku mtotot pu! chini!
katoa macho, mwili umekauka kaa sijui nini!
Mamaa kakazana kupiga kelele, kijana akatumwa akalete taksi.
Mama mwenye nyumba ambae alikuwa Banda la Uani huko akatia timu na kumtaka mama...AMKOJOLEE MTOTO!
Huwa siyaamini sana mambo haya lakini nikajikuta nami namihimiza mama afanye alichoambiwa!
Halafu kutokana na wasiwasi mkojo wenyewe nao ukawa hautaki kutoka! Patamu hapo!
Yaani kutokana na Woga wangu nikafikia hatua ya kumfokea mama eti wa nini Hakojoi!

Baadae ukatoka na gari likawa limefika.
Tukamkimbiza mtoto hospitali. Njiani akatoa rundo la choo kikubwa mbacho sijapata kukiona hata kwa mtu mzima!
Tukapata matibabu mazuri na sindano za masaa.
Nikamuuliza dakitari kama ule mkojo wa mama ulisaidia kwa namna yoyote ile.
Akajibu kuwa ni Imani tu ila mara nyingi kinachotokea ni kuwa ule mkojo hata kama una moto lakini unakuwa kama umemmwagia maji yule mtoto ambapo kwa kiasi fulaani unasaidia kupunguza lile joto na hivyo mtoto kupata kaunafuu fulani...na watu kuamini kuwa Mkojo wa mama ni dawa ya Degedege!!

Nina watoto Wanne sasa na Ninashukuru Mno kwamba haikutokea tena lakini kwa hakika nisingependa siku ile itokee tena maishani mwangu!
Inashitua Mno.
Kwa hakika ningekuwa na Gari ningelitafuta kwenye Mfuko wa Shati!

 
Hiyo ni degedege kaka, atapona tu.lakini kuwa makini sana na sindano kuna dawa za kienyeji tu simple anapona haraka tu. Watoto wengi hupitia hiyo hali usipanic sana

Asante Mkuu... Namshukuru MUNGU anaendelea vizuri!
 
Dah pole sana mkuu yameshanikuta hayo chalii yangu alipatwa na dege dege 2004 akiwa na mwaka m1 ila tulipoenda hosp alikuwa na malaria kali na homa ilikuwa juu akatibiwa akapona na yuko poa stnd 4 sasa,kwa ushauri wangu mchek vizuri huyo chalii lazima atakuwa na ugonjwa uliosababisha
homa kupanda kwa hiyo jaribu kuchek uti na mengineyo.

Asante sana mkuu kwa ushauri makini...
 
Back
Top Bottom