Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!


Pole sana Mungu ni mwema [emoji1545]
 
Pole kwa uliyopitia! Hongera kwa kujitolea na kujituma kutoa elimu kwa ugonjwa wa kifafa!
 
Pole sana kaka
Huu ugonjwa
Ulimuondoa baba yangu mzazi

Moja ya vitu huwa sipendi kusikia ni pamoja na huu ugonjwa

Baba alifariki mwaka 2004 aliangukia mahala ambapo watu wa kumsaidia hawakujua wafanyaje, walijua amezimia tu wakamwagia maji mengi sana
Mshua alikufa moja kwa moja bibi anakuja kupata taarifa wameshakosea,

Ile huwa sitamani hata kukumbuka
Anyway kwa kuwa maisha Mungu ndo mpangaji basi hatuna budi kumshukuru kwa yote
 
Pole sana
 

Kaka naomba unijibu pm
 
Kifafa ni hatari mkuu pole sana, kuna dada mmoja alianguka akipika mkono ukawa kwenye moto, msaada aliupata kwa majirani baada ya kuhisi harufu.
Samahani naomba kuuliza,inamaana anapokuwa karibu na moto hisia za kusema mkono ama mguu kuungua anakuwa hana,nauliza sio kwa kejeri ni katika kujua tu
 
Pole sana kwa yaliyokukuta

Kuhusu njia za kumsaidia mtu mwenye huo ugonjwa kwanini usiweke hapa kwa faida ya wasomaji wa sasa na wa baadae(miaka ijayo)

Naamini sio siku zote utapatikana PM lakini nyuzi za JF huwa zinaishi
Kati ya vitu ambavyo babu yetu alikuwa anaweza kutibu ni ugonjwa huu wa kifafa. Babu amefariki mwaka 1996 mungu saidia kuna baba yetu mdogo na binamu yetu wao w alikuwa karibu na babu wanaweza kutibu ugonjwa huu. Sharti kubwa asiwe ameshaanguka kwenye moto. Akiwa mgonjwa hajaanguka kwenye moto anapona. Nimeshuhudia wagonjwa wanne. Kama kuna mgonjwa DM nikuunganishe na huyu jamaa inshallah kama bahati unaweza kupona maana kila kitu ki nategemea na bahati ya mtu mwenzio anapona mwingine ikadunda naomba hili lizingatiwe. Kingine sikuhizi hata hosp kuna dawa hospitali inatuliza huu ugonjwa
 
pole sana ndugu yangu,lakini nakupa ukweli mmoja,sio kwamba nakupa moyo,hapana,ni uhalisia" amini usiamini,mama yako yupo sehemu sahihi huko alipo na ninakuhakikishia,siku ya ufufua{ukitenda mema}utaungana na mama yako mbele ya uso wa MUNGU" nasema ivo kwa sababu mateso aliyopitia sidhani kwamba alikuwa na kiburi au jeuri ya kutenda dhambi,sidhani kwamba alikuwa mzinzi kwa nina uhakika wanaume wengi walimkwepa licha ya kwamba yeye pia alikuwa hataki kutokana na hofu ya MUNGU!!!!!,,,,,,,asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…