Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!

Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!

Dah pole sana, inasikitisha sana.

katika tembea yangu katika pilika za kutafuta maisha nimewai fanya kazi na mjerumani mmoja mgonjwa wa kifafa, nilichoona jamaa alikuwa anavuta bangi, na alivyosema yeye inamsaidia sana, akivuta anakuwa sawa na anafanya kazi.

Kwa wenye ndugu wenye kifafa labda mujaribu, siyo kuvuta msokoto mzima kwa mara moja, msokoto mmoja anauvuta mara tatu hivi kwa siku, Maybe inaweza ikasaidia.
 
Duh pole sana. Umesema ugonjwa huu hauna tiba lakini labda ni kwa nchi zetu za Kiafrika. Nilikuwa na rafiki yangu mmoja kwa jina Faisal nchi Uingereza miaka ya mwanzo 2000. Yeye alikuwa ni mkimbizi kutoka Somalia, siku moja hatuna hili wala lile tukiwa tunafurahia maisha mara jamaa kadondoka chini anatapatapa mapovu yanamtoka na haja ndogo inamtoka.

Ikaitwa ambulance kufika pale akafanyiwa huduma ya kwanza, wakaona hali alivyokuwa nayo hawaiwezi wakaita air ambulance. Chopa ikaja akapeleka St Thomas hospital London sisi tulikuwa tuna Kaa Canterbury Kent. Kufika St Thomas hospital, jamaa akafanyiwa operation ya kichwa. Alikaa hospital kama miezi 2. Miaka 8 baada ya operation jamaa Hajawahi tena anguka kifafa.

Alikuja twambia kuwa alikuwa na ugonjwa huo toka azaliwe huko kwao Somalia ila mara ngingi alikuwa ana sikia dalili zake hivyo anajizuia shughuli zozote za nje ndio maana hatukujua kuwa ana ugonjwa huo. Pamoja na kupona jamaa amewekwe kwenye scheme ya Disabled allowance hivyo hafanyi kazi yoyote ya kuajiriwa analipwa £ 200 kwa week. Huku kwetu utaziona nyingi saana lakini huko ni pesa ya kawaida sana.
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1986 nikiwa na ufahamu na akili timamu .sikuwa naelewa kifafa ninini . ila nilikuwa na maswali mengi sana Kila nikimtazama mama yangu mzazi ambaye asilimia kubwa mwili wake ulitawaliwa na vidonda. Nakumbuka Kuna wakati tukiwa kisimani mama alitumbukia kisimani si mara Moja na kupata vidonda na siku nyingine anadondoka kwenye moto nakupata majeraha makubwa sana .kutoka kisimani au Mahali alipoanguka ilikuwa ni mpaka wasamalia wamtoe !! Nilikuwa najiuliza Sana kwamba ninini kinamdondosha mama yangu niliekuwa nampenda sana.

Kuna wakati niliona waganga wa asili wanapishana nyumbani kumtibia ! Kwa kuwa nilikuwa mdogo sikuweza kufuatilia hasaa ninini kinamsibu mama! Siku nyingine alidondoka sokoni katikati ya umati wa watu ! Watu wakajaa kushangaa na wasamalia wema wakasaidia kutoa huduma ya kwanza ilikuwa ni hatari angeweza kudondoka kwa siku hata mara tatu! Wakati huo nilikuwa darasa la tatu!

Alipata ujauzito akafanikiwa kujifungua mapacha WAWILI lakini haikupita miezi tatu alitumbukia nao kisimani hii ni kutokana na baba hakuwa mtu wa kukaa nyumbani muda mwingi alikuwa minadani nakumbuka siku Ile mvua kubwa ilikuwa Ina nyesha!! Mama aliokolewa akiwa hai lakini watoto wale wote walipoteza maisha!! Ilimlazimu mama kuhamishiwa kijijini Kwa Babu mzaa mama na mimi pia nikatakiwa nikakae nae! Kwa kuwa ilikuwa kumtazamia Hali yake Kwa muda mfupi, nilombewa kusoma shule mojawapo hapo kijijini Kwa muda huku tukiendelea kumuuguza!

Babu na bibi walikuwa ni wanywaji wazuri wa pombe hivyo ikifika jioni tu huwezi kuwakuta nyumbani ,,bibi pia alikuwa mkorogaji mzuri sana wa pombe ,hivyo pale nyumbani muda mwingi mizigo ya Kuni ilikuwa haipungii!! Sasa siku Moja niliamka asubuhi mapema kuwahi shule ulipofika muda wa mapumziko nilitoloka shule kurudi nyumbani , Kiukweli siku Ile sikuwa na hamu ya kukaa darasani kabisa. Nilipofika nyumbani nikakuta bibi ametenga mapipa makubwa pombe na moto mkali wa makuti akiipika pombe kama kawaida yake .alipiniona tu kaniwakia sana kwa nini nimetoroka shule?

Akanikatia mahindi shambani nikachoma fasta na kuniamuru haraka nirudi shule!! Japo sikutaka kurudi shule lakini kishingo upande nilirejea tena shuleni!! Siku hiyo kukawa na michezo tukachelewa kidogo kurudi nyumbani !! Nilifika nyumbani jioni kabisa ila nilishangaa kuona Moshi mzito sana ndani na hakukuwa na dalili ya kuwepo mtu !! Nilizowea kumkuta mama amekaa nje ,lakini hakuwepo .nikajaribu kumuita hakuitika kabisa ! Nilijitahidi kuiingia ndani nikaona Kuna Moshi usio wa kawaida na harufu nzito kama vile mtu amechoma ngozi ya ng'ombe, harufu mbaya mnoo na kulikuwa Giza !! Nikalisogelea dirisha Ile kulifungua tu la haula!! Nikaushuhudia mwili wa mama ukiwa umeteketea kabisa!! Kilichobaki ni miguu ambayo ilikuwa nje ya makaa ya ule moto mkali sana.

Nilitoka mbio kuelekea kilabuni huku nikiwa nimechanganyikiwa hata kuongea siwezi ,nilishindwa kumueleza Babu kilichotokea nyumbani zaidi ya kumshika mkono na kuanza kumvuta Kwa ishara ya kukimbia kuelekea nyumbani Kila mtu pale kilabuni aliduwaa. Mama ameungua:: hilo ndio neno pekee nililoweza kulitamka hakuna aliyebaki pale kilabuni. Kufika nyumbani Kila aliekuwa anaingia ndani alitoka meangua kilio huzuni kubwa ilitanda pale nyumbani .Kwa nini mliacha moto bila kuuzima?

Watu wengi walikuwa wanahoji swali hilo huku wazee wakianza kuutoa mwili motoni, lakini tayari yalishakuwa majivu !! Nakumbuka wazee wakiwa wanakusanya majivu na kuyatia kwenye kiroba kikubwa hivi!! Lawama zote wakizielekeza Kwa bibi na Babu. Kwamba Kwa nini hawakuuzima moto baada kumaliza kupika pombe? Hakuna tulichookoa !! Tulimzika mama akiwa kwenye kiroba ! Tulizika majivu.

Naweza kusema nauchukia sana ugonjwa huu. Na usimpuuze mtu yeyote mwenye ugonjwa huu! Popote pale iwe nje au ndani ya familia yenu !!ugonjwa huu Hauna tiba ya Moja Kwa Moja !lakini wagonjwa wake wanahitaji sana uangalizi maalumu !! Katika miaka yangu nimejitahidi Sana kufanya utafiti kuhusu ugonjwa huu.

Nimejifunza mengi na sasa na weza kusema nipo karibu sana na wagonjwa wa kifafa kuwapa elimu na namna ya kuishi Kwa tahadhari na kuepuka hatari zinazowahusu watu Hawa. Iwe una ndugu ,rafiki au jirani wa karibu ambae anateseka na ugonjwa huu tafadhali njoo dm yangu nitakupa elimu ya jinsi ya kumsaidia ,na jinsi anavyoweza kupona kabisa !! Usiupuuze ugonjwa huu ni hatari kupita kiasi!
Daaaa huu uzi bora ningeupita tu
 
Pole sana kwa yaliyokukuta

Kuhusu njia za kumsaidia mtu mwenye huo ugonjwa kwanini usiweke hapa kwa faida ya wasomaji wa sasa na wa baadae(miaka ijayo)

Naamini sio siku zote utapatikana PM lakini nyuzi za JF huwa zinaishi
@mgaguzi Husika na kichwa cha habari hapa juu
 
Huu ugonjwa usikie tu, unanisumbua almost miaka miwili Sasa. Ikinitokea mkono wa kulia ndo naumia sana na kujing'ata.
Kitu kingine nilichonotice hivi karibuni ni kuwa ikinitokea huwa nakaa kama wiki hivi nakuwa sina kumbukumbu vizuri.
Ee Mungu naomba uniponye!!
 
Kuna Jamaa yangu alipata Ajali mbaya pale Bwawani miaka ya 90 mwishoni aikuwa kwenye Coma karibia miezi mitatu alipopona akarudi kwenye kazi lakini akarudi na Kifafa sema yeye kinakuwa na dalili kwahiyo huwa anapaki Gari na hakimshiki mara kwa mara na anaendesha Petrol Tanker.
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1986 nikiwa na ufahamu na akili timamu, sikuwa naelewa kifafa ninini ila nilikuwa na maswali mengi sana Kila nikimtazama mama yangu mzazi ambaye asilimia kubwa mwili wake ulitawaliwa na vidonda. Nakumbuka Kuna wakati tukiwa kisimani mama alitumbukia kisimani si mara Moja na kupata vidonda na siku nyingine anadondoka kwenye moto na kupata majeraha makubwa sana. Kutoka kisimani au Mahali alipoanguka ilikuwa ni mpaka wasamaria wamtoe!! Nilikuwa najiuliza Sana kwamba ni nini kinamdondosha mama yangu niliyekuwa nampenda sana.

Kuna wakati niliona waganga wa asili wanapishana nyumbani kumtibia! Kwa kuwa nilikuwa mdogo sikuweza kufuatilia hasaa ni nini kinamsibu mama! Siku nyingine alidondoka sokoni katikati ya umati wa watu! Watu wakajaa kushangaa na wasamaria wema wakasaidia kutoa huduma ya kwanza ilikuwa ni hatari angeweza kudondoka kwa siku hata mara tatu! Wakati huo nilikuwa darasa la tatu!

Alipata ujauzito akafanikiwa kujifungua mapacha WAWILI lakini haikupita miezi mitatu alitumbukia nao kisimani hii ni kutokana na baba hakuwa mtu wa kukaa nyumbani muda mwingi alikuwa minadani, nakumbuka siku Ile mvua kubwa ilikuwa Ina nyesha!! Mama aliokolewa akiwa hai lakini watoto wale wote walipoteza maisha!! Ilimlazimu mama kuhamishiwa kijijini Kwa Babu mzaa mama na mimi pia nikatakiwa nikakae nae! Kwa kuwa ilikuwa kumtazamia Hali yake Kwa muda mfupi, niliombewa kusoma shule mojawapo hapo kijijini Kwa muda huku tukiendelea kumuuguza!

Babu na bibi walikuwa ni wanywaji wazuri wa pombe hivyo ikifika jioni tu huwezi kuwakuta nyumbani ,,bibi pia alikuwa mkorogaji mzuri sana wa pombe ,hivyo pale nyumbani muda mwingi mizigo ya Kuni ilikuwa haipungii!! Sasa siku Moja niliamka asubuhi mapema kuwahi shule ulipofika muda wa mapumziko nilitoloka shule kurudi nyumbani , Kiukweli siku Ile sikuwa na hamu ya kukaa darasani kabisa. Nilipofika nyumbani nikakuta bibi ametenga mapipa makubwa pombe na moto mkali wa makuti akiipika pombe kama kawaida yake .alipiniona tu kaniwakia sana kwa nini nimetoroka shule?

Akanikatia mahindi shambani nikachoma fasta na kuniamuru haraka nirudi shule!! Japo sikutaka kurudi shule lakini kishingo upande nilirejea tena shuleni!! Siku hiyo kukawa na michezo tukachelewa kidogo kurudi nyumbani !! Nilifika nyumbani jioni kabisa ila nilishangaa kuona Moshi mzito sana ndani na hakukuwa na dalili ya kuwepo mtu !! Nilizowea kumkuta mama amekaa nje ,lakini hakuwepo .nikajaribu kumuita hakuitika kabisa ! Nilijitahidi kuiingia ndani nikaona Kuna Moshi usio wa kawaida na harufu nzito kama vile mtu amechoma ngozi ya ng'ombe, harufu mbaya mnoo na kulikuwa Giza!! Nikalisogelea dirisha Ile kulifungua tu la haula!! Nikaushuhudia mwili wa mama ukiwa umeteketea kabisa!! Kilichobaki ni miguu ambayo ilikuwa nje ya makaa ya ule moto mkali sana.

Nilitoka mbio kuelekea kilabuni huku nikiwa nimechanganyikiwa hata kuongea siwezi ,nilishindwa kumueleza Babu kilichotokea nyumbani zaidi ya kumshika mkono na kuanza kumvuta Kwa ishara ya kukimbia kuelekea nyumbani Kila mtu pale kilabuni aliduwaa. Mama ameungua:: hilo ndio neno pekee nililoweza kulitamka hakuna aliyebaki pale kilabuni. Kufika nyumbani Kila aliekuwa anaingia ndani alitoka meangua kilio huzuni kubwa ilitanda pale nyumbani. Kwa nini mliacha moto bila kuuzima?

Watu wengi walikuwa wanahoji swali hilo huku wazee wakianza kuutoa mwili motoni, lakini tayari yalishakuwa majivu !! Nakumbuka wazee wakiwa wanakusanya majivu na kuyatia kwenye kiroba kikubwa hivi!! Lawama zote wakizielekeza Kwa bibi na Babu. Kwamba Kwa nini hawakuuzima moto baada kumaliza kupika pombe? Hakuna tulichookoa !! Tulimzika mama akiwa kwenye kiroba ! Tulizika majivu.

Naweza kusema nauchukia sana ugonjwa huu. Na usimpuuze mtu yeyote mwenye ugonjwa huu! Popote pale iwe nje au ndani ya familia yenu!! Ugonjwa huu Hauna tiba ya Moja Kwa Moja! Lakini wagonjwa wake wanahitaji sana uangalizi maalumu!! Katika miaka yangu nimejitahidi Sana kufanya utafiti kuhusu ugonjwa huu.

Nimejifunza mengi na sasa naweza kusema nipo karibu sana na wagonjwa wa kifafa kuwapa elimu na namna ya kuishi Kwa tahadhari na kuepuka hatari zinazowahusu watu Hawa. Iwe una ndugu, rafiki au jirani wa karibu ambae anateseka na ugonjwa huu tafadhali njoo dm yangu nitakupa elimu ya jinsi ya kumsaidia na jinsi anavyoweza kupona kabisa!! Usiupuuze ugonjwa huu ni hatari kupita kiasi!
Pole sana
 
Huu ugonjwa usikie tu, unanisumbua almost miaka miwili Sasa. Ikinitokea mkono wa kulia ndo naumia sana na kujing'ata.
Kitu kingine nilichonotice hivi karibuni ni kuwa ikinitokea huwa nakaa kama wiki hivi nakuwa sina kumbukumbu vizuri.
Ee Mungu naomba uniponye!!
Mcheki mkuu Mganguzi amesema anatoa ushauri kwani ana uzoefu kupitia mzazi wake
 
  • Thanks
Reactions: Gru
Ndugu me binafsi na mdogo wangu ambaye amekuwa akitesela na huo ugonjwa ni muda sasa kifafa kimemfanya ad adhoofike afya tumeshajarib kila namna apone lakin imekuwa ni kaz bure hasa kikifika kipindi cha mwezi kuchomoza limekuwa ni tatzo kubwa ndan ya familia kama unaujuz wowote kuhus huo ugonjwa tujuzane
Yesu anaponya hii ugonjwa bure, mpelekeni kwenye maombi.
 
Aisee pole sana

Miaka miwili iliyopita Kuna kijana hapa mtaani alikuwa na huo ugonjwa.

Sasa huwa anakata majani ya Ng'ombe.

Siku hio akaenda kukata majani karibu kabisa na bwawa la maji.

Ugonjwa ukamtaiti akaangukia bwawani akafia huo baada sana watu wakaja kumkuta humo.

inasikitisha sana.

Wanasema watu wenye vifafa hawahitsji kukaa sehemu zenye mwanga mwanga.
 
Back
Top Bottom