Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!

Ugonjwa wa kifafa usikilizeni redioni. Simulizi yake ni ya kutishaa!

Primary nilisoma na jamaa tens jirani, alikuwa anaanguka though sio sana. Mara ya kwanza kumuona nilishangaa sana, sikujua ni kitu gani. Shule ya upili nililala dom moja na jamaa alikuwa anaanguka balaa, yani karibia kila mwezi mwamba alikuwa anaanguka, hilo povu analotoa sasa ni balaa.

Sad sana
 
Primary nilisoma na jamaa tens jirani, alikuwa anaanguka though sio sana. Mara ya kwanza kumuona nilishangaa sana, sikujua ni kitu gani. Shule ya upili nililala dom moja na jamaa alikuwa anaanguka balaa, yani karibia kila mwezi mwamba alikuwa anaanguka, hilo povu analotoa sasa ni balaa.

Sad sana
Daaahh... Huzunii sana
 
Ads
Pole sna kiongozi nami nilikuwa na Mama mdogo wangu naye alikufa kw a kuungua moto zamani mwaka 1996 ndo alikufa huu ugonjwa ni hatari Sana Ila ,nilisimuliwa kuwa huyu Mama mdogo alilogwa
A
Pole sna kiongozi nami nilikuwa na Mama mdogo wangu naye alikufa kw a kuungua moto zamani mwaka 1996 ndo alikufa huu ugonjwa ni hatari Sana Ila ,nilisimuliwa kuwa huyu Mama mdogo alilogwa .
ANte sana mkuu
 
Ina
Primary nilisoma na jamaa tens jirani, alikuwa anaanguka though sio sana. Mara ya kwanza kumuona nilishangaa sana, sikujua ni kitu gani. Shule ya upili nililala dom moja na jamaa alikuwa anaanguka balaa, yani karibia kila mwezi mwamba alikuwa anaanguka, hilo povu analotoa sasa ni balaa.

Sad sana
Instisha sana
 
Nakumbuka ilikuwa mwaka 1986 nikiwa na ufahamu na akili timamu .sikuwa naelewa kifafa ninini . ila nilikuwa na maswali mengi sana Kila nikimtazama mama yangu mzazi ambaye asilimia kubwa mwili wake ulitawaliwa na vidonda. Nakumbuka Kuna wakati tukiwa kisimani mama alitumbukia kisimani si mara Moja na kupata vidonda na siku nyingine anadondoka kwenye moto nakupata majeraha makubwa sana .kutoka kisimani au Mahali alipoanguka ilikuwa ni mpaka wasamalia wamtoe !! Nilikuwa najiuliza Sana kwamba ninini kinamdondosha mama yangu niliekuwa nampenda sana. Kuna wakati niliona waganga wa asili wanapishana nyumbani kumtibia ! Kwa kuwa nilikuwa mdogo sikuweza kufuatilia hasaa ninini kinamsibu mama! Siku nyingine alidondoka sokoni katikati ya umati wa watu ! Watu wakajaa kushangaa na wasamalia wema wakasaidia kutoa huduma ya kwanza ilikuwa ni hatari angeweza kudondoka Kwa siku hata mara tatu !! Wakati huo nilikuwa darasa la tatu! Alipata ujauzito akafanikiwa kujifungua mapacha WAWILI lakini haikupita miezi tatu alitumbukia nao kisimani hii ni kutokana na baba hakuwa mtu wa kukaa nyumbani muda mwingi alikuwa minadani nakumbuka siku Ile mvua kubwa ilikuwa Ina nyesha!! Mama aliokolewa akiwa hai lakini watoto wale wote walipoteza maisha!! Ilimlazimu mama kuhamishiwa kijijini Kwa Babu mzaa mama na mimi pia nikatakiwa nikakae nae! Kwa kuwa ilikuwa kumtazamia Hali yake Kwa muda mfupi, nilombewa kusoma shule mojawapo hapo kijijini Kwa muda huku tukiendelea kumuuguza ! Babu na bibi walikuwa ni wanywaji wazuri wa pombe hivyo ikifika jioni tu huwezi kuwakuta nyumbani ,,bibi pia alikuwa mkorogaji mzuri sana wa pombe ,hivyo pale nyumbani muda mwingi mizigo ya Kuni ilikuwa haipungii!! Sasa siku Moja niliamka asubuhi mapema kuwahi shule ulipofika muda wa mapumziko nilitoloka shule kurudi nyumbani , Kiukweli siku Ile sikuwa na hamu ya kukaa dalasani kabisa ! Nilipofika nyumbani nikakuta bibi ametenga mapipa makubwa pombe na moto mkali wa makuti akiipika pombe kama kawaida yake .alipiniona tu kaniwakia sana Kwa nini nimetoloka shule ? Akanikatia mahindi shambani nikachoma fasta na kuniamuru haraka niludi shule!! Japo sikutaka kurudi shule lakini kishingo upande nililejea tena shuleni!! Siku hiyo kukawa na michezo tukachelewa kidogo kurudi nyumbani !! Nilifika nyumbani jioni kabisa ila nilishangaa kuona Moshi mzito sana ndani na hakukuwa na dalili ya kuwepo mtu !! Nilizowea kumkuta mama amekaa nje ,lakini hakuwepo .nikajaribu kumuita hakuitika kabisa ! Nilijitahidi kuiingia ndani nikaona Kuna Moshi usio wa kawaida na harufu nzito kama vile mtu amechoma ngozi ya ng'ombe, harufu mbaya mnoo na kulikuwa Giza !! Nikalisogelea dirisha Ile kulifungua tu la haula!! Nikaushuhudia mwili wa mama ukiwa umeteketea kabisa!! Kilichobaki ni miguu ambayo ilikuwa nje ya makaa ya ule moto mkali sana !! Nilitoka mbio kuelekea kilabuni huku nikiwa nimechanganyikiwa hata kuongea siwezi ,nilishindwa kumueleza Babu kilichotokea nyumbani zaidi ya kumshika mkono na kuanza kumvuta Kwa ishara ya kukimbia kuelekea nyumbani Kila mtu pale kilabuni aliduwaa !! Mama ameungua:: hilo ndio neno pekee nililoweza kulitamka hakuna aliyebaki pale kilabuni ! Kufika nyumbani Kila aliekuwa anaingia ndani alitoka meangua kilio huzuni kubwa ilitanda pale nyumbani .Kwa nini mliacha moto bila kuuzima? Watu wengi walikuwa wanahoji swali hilo huku wazee wakianza kuutoa mwili motoni, lakini tayari yalishakuwa majivu !! Nakumbuka wazee wakiwa wanakusanya majivu na kuyatia kwenye kiroba kikubwa hivi!! Lawama zote wakizielekeza Kwa bibi na Babu ! Kwamba Kwa nini hawakuuzima moto baada kumaliza kupika pombe!?? Hakuna tulichookoa !! Tulimzika mama akiwa kwenye kiroba ! Tulizika majivu ! Naweza kusema nauchukia sana ugonjwa huu !! Na usimpuuze mtu yeyote mwenye ugonjwa huu! Popote pale iwe nje au ndani ya familia yenu !!ugonjwa huu Hauna tiba ya Moja Kwa Moja !lakini wagonjwa wake wanahitaji sana uangalizi maalumu !! Katika miaka yangu nimejitahidi Sana kufanya utafiti kuhusu ugonjwa huu !! Nimejifunza mengi na sasa na weza kusema nipo karibu sana na wagonjwa wa kifafa kuwapa elimu na namna ya kuishi Kwa tahadhari na kuepuka hatari zinazowahusu watu Hawa ! Iwe una ndugu ,rafiki au jirani wa karibu ambae anateseka na ugonjwa huu tafadhali njoo dm yangu nitakupa elimu ya jinsi ya kumsaidia ,na jinsi anavyoweza kupona kabisa !! Usiupuuze ugonjwa huu ni hatari kupita kiasi!
Dahh, Pole sana mkuu. Mungu amrehemu mama yetu mpendwa [emoji120][emoji120][emoji120]
 
Dah pole sana nimejikuta mpka chozi limenitoka aisee pole sana mkuu
 
Ndugu me binafsi na mdogo wangu ambaye amekuwa akitesela na huo ugonjwa ni muda sasa kifafa kimemfanya ad adhoofike afya tumeshajarib kila namna apone lakin imekuwa ni kaz bure hasa kikifika kipindi cha mwezi kuchomoza limekuwa ni tatzo kubwa ndan ya familia kama unaujuz wowote kuhus huo ugonjwa tujuzane
 
Sitokuja kusahau mwaka 1998 nasafiri na basi dogo DCM toka Tukuyu kwenda Ushirika, nimekaa siti ya mlangoni ghafla nikamuona konda anakakamaa ameshika chuma cha pembeni ya mlango na mlango upo wazi na gari ipo kwenye spidi ya kawaida, anauma ulimi wake anatoa mate anakakamaa kashika chuma kile cha kushika kama unapanda kwenye daladala bahati alikuwa amegeuka anaangalia ndani ya gari anahesabu pesa zake.
Nilichomoka kama komandoo kipensi kabla hajaachia chuma kumdaka na kumshikilia kwa nguvu sana huku nikimpeleka kwa ndani ya gari asianguke nje na kugonga kichwa chini na gari kumpitia na tairi ya nyuma.
Alinishika kwa nguvu sijawahi ziona toka nazaliwa alinishika mikono chini ya mabega lakini mimi nilishika shingo badae akaachia mikono akashika nguo kwa nguvu za ajabu mpaka zikatatuka mifuko ya kifuani.

Kuna mama mmoja akamwekea kanga mdomoni mimi nimemshika yule jamaa kama dakika 15 hizi nikaona ameanza kulegea. Shati lake limetapakaa mate na mimi nimetapakaa mate na mambo mengine ya kibinadamu.

Niliambiwa nimuache pale pale atulie na tukafika ushirika stendi jamaa akiwa bado amepoteza fahamu. Lakini lile tukio siwezi kulisahau maishani mwangu. Nilipewa sifa nyingi sana kwa tukio lile. Kuna jamaa alikuwa anaitwa Mwakibete alininunulia shati pale ushirika maana la kangu lilichanika kwenye kwapa ile vuta nkuvute na kidogo nilitapakaa mate ule mgusano wa nguvu kama tunacheza mieleka vile.

Jamani kifafa ni ugonjwa hauna mfano kwa kuogofya,kustua na kutesa watu wa Mungu.

Mwenyezi Mungu atusaidie sana sisi waja wake. Amina
 
Back
Top Bottom