Wanabodi habari zenu nina mdogo wangu wa kiume ameota tuvipele kwenye eneo la kibofu akaonwa ikasemekana ni genital warts akapewa silver pencil ya kuvichoma ila haviishi na vingine vinaota,je kuna dawa ya kunywa au dawa ipi ingine inafanya kazi vyema kuleta matokeo??
Habari mkuu.
Pole na mdogo wako kuumwa.
Umenitumia Dm na kuniuliza kuhusu CASTOR OIL kama inafaa kweli kuhusu hizo GENITAL WARTS.
Nimeona nikujibu hapa na sio DM ili iwe kwa manufaa ya wengine pia.
Kwanza nikukumbushe tu kuumwa ugonjwa wowote sio AIBU kwa sababu .
Na wahenga walisema MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA.
Sasa basi ikiwa unaumwa wewe au mdogo wako USIONE AIBU.
Nirudi katika mada husika.
Mimi pia miaka inafika 15 nyuma kama sikosei niliumwa GENITAL WARTS.
Zilinitesa sasa, zilikuwa zinawasha tena hasa kipindi cha usiku nikiwa nimelala.
Nilikuwa najikuna mpaka najiumiza na kutoa damu.
Hapo mwanzoni sikujua kama ni Genital warts. Nilihisi nimepata fangas.
Nikaona maduka ya Dawa yaani Famas na kuwaambia nawashwa sana sehemu za siri , walinipa cream za kupaka inaitwa SONADERM nikawa nikiipaka muwasho unaacha na usiku nalala vizuri.
Lakini sikupona na baadae ndo vikaanza kutoka hivyo Viwarts na ndo nikaanza kuviona kwa macho.
Nikaanza kufanya SEARCH kwenye Mitandao kama sikosei enzi hizo nilikuwa natumia YAHOO SEARCH sikumbuki kama Google ilikuwa tayari inawezekani haikuwa maarufu.
Baada kuserch nikagundua ni GENITAL WARTS , nikaanza kusachi tiba zake, tiba zikawa aina tofauti ya kwanza ilikuwa KUVICHOMA Na kuvikata kwa laser.
Tiba ingine nakumbuka nilioiona ilikuwa OPERESHEN.
Lakini nikasoma ushuhuda wa watu wengi waliofanyia hizo Tiba ni kwamba WARTS zilirudi tena.
Nikaogopa.
Nikasema Ngoja niende nikamuona SPECIAL DOCTOR wa magonjwa ya Ngozi.
Nikaenda pale njia ya kuelekea Hospital ya Muhimbili pale kulikuwa na profesa wa magonjwa ya ngozi.
Alinikagua na yeye akasema ni GENITAL WARTS.
Akanipa Dawa za kupaka zilikuwa Cream sikumbuki jina lake hiyo cream na akanipa vidonge vya kumeza pia.
Nilitumia hizo Dawa lakini sikupona.
Isipokuwa tu ilinisaidia muwasho ukapungua na usiku nikawa naweza kulala.
Baada siku kadhaa vilizidi kujaa ni vikawa vingi zaidi , ni nikiacha zile cream basi najikuna kama vile nataka kuchuna ngozi.
Dahh nilichanganyikiwa.
Niliamua kurudi katika mitandao na kufanya search tena.
Nilikesha kwenye kompyuta.
Mpaka nikampata mtu yuko marekani anadai anayo dawa yake.
Nakumbuka huyo mtu alidai anataka malipo kidogo tu kama ya Dola 10 ili anipe hiyo dawa na alisema hanitumii dawa ila dawa nitaipata katika nchi yangu hapa hapa kwa mchanganyiko atakaonipa.
Na akasema pesa nitakapoituma tu akipata atanitumia email namna ya huo mchanganyiko unavyofanya kazi.
Basi nikaanza kuwasiliana nae na nikasema ata akiniibia basi nitashukuru mungu tu .
Nikatuma pesa dola 10 ikachukua kama wiki hivi akaipata.
Alipoipata ile pesa akanitumia email ya ule mchanganyiko.
Akaniambia kwamba hivi.
Anza na dawa hii chukua CASTROL OIL ambayo sio ya viwandani, akimaanisha iwe ya asili ipakaze kwenye hizo warts mara 2 au 3 kwa siku.
Na kama mafuta hayatulii basi weka pamba yenye hayo mafuta halafu funga kitambaa au bandika plasta mafuta yakae pale.
Akaniambia kama warts zako sio sugu utaona ndani ya wiki 1 au 2 .
Na kama sugu fanya hivi
Chukua kitunguu thaumu ( garlic ) kiponde na kitunguu maji (red onion) kiponde changanya na hayo mafuta ya castrol oil halafu pakaza pale mara 2 au 3 kwa siku.
Mimi baada kupata hayo maelekezo nikaenda pale soko la kariakoo pembeni ya stendi ya magari ya mwenge kuna maduka mengi yanauza dawa za asili.
Nikanunua chupa ya nusu lita kwa 2000 elfu mbili tu enzi hizo. Sijui sasa wanauzaje, yananuka lakini nilijikaza sana.
Nikaanza hiyo tiba.
Huwezi amini baada wiki tuu na hata sikumaliza wiki yenyewe nikapona.
Nilifurahi sana.
Nikarudi kwa yule jamaa wa marekani kumshukuru , naye alifurahi.
Lakini sasa sikumbuki tena pale nilipompata kwenye mitandao ningekupa umsome umuone na ndo mana nikazitoa hapa hizo dawa bure mwenye kutaka atumie.
Hii ni dawa ya asili na sidhani kama ina madhara yoyote na pia kwa ushauri ni bora ukaanza kwanza hospitali kuhakikisha nini unaumwa , na ukishapata uhakika nini unaumwa na ukitaka unaweza ukaijaribu hiyo Dawa ambayo ni mafuta tu.
La mwisho mimi sio dokta wala sina ujuzi wowote wa tiba asili.
Nilichofanya nimetoa ushuhuda wangu kwa kile kilichonitesa mimi wakati huo.
Kwa ushauri zaidi waone wataalamu wa afya mahospitalini au wataalamu wa tiba za asili wanaotambulika.
Nakutakia upone haraka ikiwa wewe au mdogo wako.
MUNGU atakusaidia usisahau pia kumuomba MUNGU.
Kama umeowa mtibu na mwenza wako, mpone wote kwa pamoja.
Vinaambukiza , na kwa wanawake vinajificha kwa ndani huvioni.
Nakutakia maisha mema. Ahsante.