Mdau wa JamiiForums.com ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa UTI kwa wanawake.
Anahoji inakuwaje sababu kubwa inayotajwa kuwa ni uchafu ipate mashiko kwa nyakati hizi, kwani wanawake wa zamani ndio walikuwa wasafi zaidi kuliko hawa wa sasa?
Mdau huyu anashauri wataalam wa afya waingie upya maabara kuchunguza nini hasa chanzo halisi cha kuongezeka kwa maambukizi ya UTI. Kwake hoja ya kuwa ugonjwa huu unaweza kusababishwa na uchafu anaona kama haina mashiko.
Sayansi inasemaje juu ya hoja hizi za mdau?
Anahoji inakuwaje sababu kubwa inayotajwa kuwa ni uchafu ipate mashiko kwa nyakati hizi, kwani wanawake wa zamani ndio walikuwa wasafi zaidi kuliko hawa wa sasa?
Mdau huyu anashauri wataalam wa afya waingie upya maabara kuchunguza nini hasa chanzo halisi cha kuongezeka kwa maambukizi ya UTI. Kwake hoja ya kuwa ugonjwa huu unaweza kusababishwa na uchafu anaona kama haina mashiko.
Sayansi inasemaje juu ya hoja hizi za mdau?
- Tunachokijua
- UTI ni ufupisho wa maneno Urinary Tract Infection, au kwa kiswahili ikiwa ni maambukizi ya sehemu yoyote ya mfumo wa mkojo ambao huhusisha figo, kibofu cha mkojo, mrija wa mkojo pamoja na mrija unao unganisha figo na kibofu cha mkojo.
Maambukizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na bakteria jamii ya E. coli, lakini katika mazingira machache fangasi na virusi wanaweza kuwa chanzo cha maambukizi haya.
Maambukizi ya mfumo wa mkojo yanaweza kugawanywa kwenye makundi mawili yaani maambukizi ya sehemu ya chini ya mfumo, yakihusisha mrija wa mkojo na kibofu cha mkojo au maambukizi ya sehemu ya juu ya mfumo yakihusisha figo au mrija unaounganisha figo na kibofu.
Maambukizi ya sehemu ya juu ya mfumo huwa ni machache ikilinganishwa na maambukizi ya sehemu ya chini ya mfumo. Huwa pia na dalili na madhara makubwa zaidi.
Wanawake huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuugua ugonjwa huu kuliko wanaume kwa sababu mrija wa mkojo huwa ni mfupi, pia tundu la uke huwa karibu sana na sehemu ya haja kubwa. Ni rahisi kwa bakteria kutoka kwenye choo kuingia ukeni.
Katika hatua hii, JamiiForums imebaini mambo yafuatayo;
- Matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, kondomu, kemikali kali kusafishia uke hasa zile zenye lengo la kuua mbegu za kiume huongeza uwezekano wa wanawake kuugua ugonjwa huu.
- Sababu zingine kama kufikia umri wa ukomo wa hedhi, ushiriki wa tendo la ndoa ambao huweka msuguano mkubwa unaoweza kuingiza bakteria kutoka kwenye tundu la haja kubwa pamoja na ujauzito ambao hubana kibofu cha mkojo huwa ni baadhi ya sababu zinazoongeza uwezekano wa wanawake kuugua ugonjwa huu kuliko wanaume.
- Uchafu unaweza pia kuwa sababu ya kuugua ugonjwa huu kutokana na ukaribu wa sehemu ya haja kubwa na tundu la uke. Kutokujisafisha vizuri, kubakiza mabaki ya choo kwenye nguo ya ndani pamoja na kuchamba vibaya kutoka nyuma kuja mbele kunaweza kusababisha ugonjwa wa UTI.
Pamoja na uwepo wa sababu hizi zote, njia kubwa zinazoweza kumfanya mwanamke asiugue mara kwa mara ugonjwa huu ni kutunza usafi wa mwili wake kwa kusafisha sehemu za siri kutoka mbele kwenda nyuma (frontal to back wiping), kunywa maji mengi walau lita 2.5 kila siku pamoja na kuvaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba 100%.
Pia, kuacha tabia ya kudeki uke (vaginal douching) kwa kutumia sabuni na manukato yenye kemikali kali husaidia kuepusha UTI ya mara kwa mara.