NADHARIA Ugonjwa wa UVIKO-19 unadaiwa kurejea kwa kasi nchini

NADHARIA Ugonjwa wa UVIKO-19 unadaiwa kurejea kwa kasi nchini

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Source #1
View Source #1
Salaam Ndugu zangu,

Zipo tetesi zimesambaa katika maeneno mbalimbali kwamba ugonjwa wa Covid-19 umerejea nchi. Kwa sisi tunaoishi Dar tunashuhudia kulipuka kwa mafua makali yakiambatana na kikohozi fulani na homa.

Je kuna ukweli kiasi gani kwenye hili?

Jamiiforums tunaomba mtusaidie kuuliza kwa mamlaka ili tahadhari ichukuliwe mapema.

1683960668068.png
 
Tunachokijua
Kutokana na kusambaa kwa tetesi ya kuibuka wa wimbi la Uviko-19 ambazo zimechochewa na kuwapo kwa sintofahamu ya Watu kuugua Homa za Mafua Makali, Kifua na Kichwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imetoa ufafanuzi wa awali kuhusu madai hayo:

Wizara ya Afya imesema inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka Hospitali na Vituo vya Afya ndani ya Wiki hii.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kati ya Wagonjwa 288 waliopimwa UVIKO-19 kati ya Mei 6-12, 2023, 6 walithibitishwa kuwa na Corona. Idadi hiyo ni pungufu ikilinganishwa na waliopima kati ya 29 Aprili hadi 5 Mei 2023 na hakuna kifo chochote.

Zaidi ya hayo, Ummy amewataka Wananchi kuondoa hofu kwa kuwa Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye Hospitali mbalimbali na itatoa taarifa rasmi kuhusu tetesi za Uviko-19.

Kutokana na ufafanuzi huo wa Wizara Jamiiforums itasubiri uchunguzi wa wizara na taarifa kutoka mamlaka husika ili kujua kama hali hii ya mafua, homa na kikohozi ni wimbi la Uviko-19.

Aidha, kutokana na Wizara kuthibitisha kwamba bado kuna wagonjwa wa Uviko-19 nchini japo kwa idadi ndogo ya watu Jamiiforums inashauri wanajamii tuendelee kuchukua tahadhari wakati wote.
Watu wasirudishe namba kwa Mola? Ati korona. Ina maana uko ulipo hamna misiba? Au ni hii miwili ya watu maarufu ndio ikushtue?
 
Kumbe waliokufa hapa nchini ni watu wawili pekee? Na huu msiba uliopo hapa mtaani kwetu si wa Mtanzania?!
 
Salaam Ndugu zangu,

Zipo tetesi zimesambaa katika maeneno mbalimbali kwamba ugonjwa wa Covid-19 umerejea nchi. Kwa sisi tunaoishi Dar tunashuhudia kulipuka kwa mafua makali yakiambatana na kikohozi fulani na homa.

Je kuna ukweli kiasi gani kwenye hili?

Jamiiforums tunaomba mtusaidie kuuliza kwa mamlaka ili tahadhari ichukuliwe mapema.

Hii homa imezuka hadi Ulaya..
si utani to be honest ni kali ilinishikia Amsterdam nilivyorudi nchi nnayoishi niliogopa nikajua ndo safari.
Kwasababu ilikua inabana sehemu zote za hewa haiskii dawa ya kupuliza wala chochote.
Tangawizi nilikula Kama chakula.
Mwishoni hadi makamasi yalitoka ya damu.
Chamsingi tu ukiona dalili wahi kutumia dawa hata Zile za maji then inaweza ondoka na tangawizi tafuna na chai yenye limao na tangawizi, asali.
 
Salaam Ndugu zangu,

Zipo tetesi zimesambaa katika maeneno mbalimbali kwamba ugonjwa wa Covid-19 umerejea nchi. Kwa sisi tunaoishi Dar tunashuhudia kulipuka kwa mafua makali yakiambatana na kikohozi fulani na homa.

Je kuna ukweli kiasi gani kwenye hili?

Jamiiforums tunaomba mtusaidie kuuliza kwa mamlaka ili tahadhari ichukuliwe mapema.

Kipupwe uviko tumeuvika
 
Back
Top Bottom