Habarini wanajamii forums nilitaka kujua ukiondoa dagaa na maharage ni vyakula gani vingine ambavyo mgonjwa wa ulcers hatakiwi kula na pia kwa nini hvyo harusiwi kula?
Kingine nilitaka kujua dawa inayotibu ulcers
Salam,
Kama nimekufahamu itakuwa unakusudia "peptic ulcer" (PU) Vidonda vya tumbo ? kama ni hivyo
Masuala yako limejigawa sehemu 3 ambazo ntachangia kwa ufafanuzi kidogo kama ifatavyo:
UFUNGUZI: Ugonjwa wa PU ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa tumbo aidha kwa kupata vidonda" Ulcer" au michubuko "Gastritis".
SABABU: Ni pamoja na mambo mbali mbali, ikichangiwa na kutokula kwa wakati, kula vyakula vikali/ vichachu, msongomano wa mawazo "tension /enxiety", au uchofu "stress" lakini msingi mkubwa ni kupungua kinga ya tumbo kuhimili tindi kali inayotolewa tumboni kusaga chakula "hydrochloric acid" hivyo badala ya kuyayusha chakula huanza pole pole kuuunguza utumbo aidha kwenye tumbo lenyewe au sehemu ya chini "Duodenum" na ndio maana vidonda hivi vikagawika sehemu mbili ambazo ni i. peptic ulcer na ii. duodenal ulcer.
MATIBABU: yamejigawa katika sehemu kuu kama ifuatavyo
1.Kuachana na sababu inayochangia mfano stress, ugomvi, mawazo, kutokula kwa wakati, kuto pumzika, kuto fanya mazoezi ya mwili.
2. Tabia ya ulaji wa vyakula vikali au vyenye acid, mfano Jamii ya maharage, kunde... nk, Vyakula vya acid kama ndimu , limau, maembe mabichi, ukwaju...nk, achari na vyakula vyoote vichachu,
madawa kama asprin, diclofenac na dawa zote jamiii ya NSAD, mavyakula ya mafuta mengi. (Vidagaa vya kupika visivyo ungwa kwa ukali unaweza kula)
3. Anti acid, ni vyakula au dawa za kukata acid, mfano maziwa, vidonge vya Magnesium trisilicate, dawa za kunywa relcer gel, gastrocid...nk
4. Dawa za kuponesha vidonda na za kuua vidudu, zipo nyingi na za kisasa zinauwezo mkubwa wa kutibu lakini hapa si pahala pake kuzitaja kwani zinahitaji utaalam kwa matumizi yake.
SABABU ZA KUTOKULA VYAKULA HIVYO
Kama nilivyosema hapo juu sababu kubwa ya ulcer ni acid ambayo huunguza utumbo na hivyo vyakula vilivyo katwazwa pia vina kiwango kikubwa cha acid ni kusema vikiendelea kuliwa vitaongeza athari ya maradhi na vitaongeza mda wa kupona, au kusababisha hata kutoboa tumbo/ uchango na kusababisha kuvuja damu ambayo na hatari sana.
Natumai ntakuwa nimechangia angalau kidogo, kwa uchangia zaid karibu tena
Asante