Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

[emoji524]UHUSIANO KATI YA VIDONDA VYA TUMBO NA NGUVU ZA KIUME[emoji524]

[emoji298]Wanaume wengi wanaougua vidonda vya tumbo kwa muda mrefu hutokewa pia kuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwahiyo ikiwa mwanaume una tatizo la kushindwa kuhimili tendo la ndoa na unaumwa vidonda vya tumbo, basi cha kwanza utatakiwa ujitibu vidonda vya tumbo.

Hili linakuwa kweli hasa tukiziangalia baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo kama zifuatazo;

Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo zinazopelekea pia upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na zifuatazo:

[emoji117]1. Kuchoka choka sana bila sababu maalum
[emoji117]2. Kuumwa mgongo au kiuno
[emoji117]3. Kizunguzungu
[emoji117]4. Kukosa usingizi
[emoji117]5. Kiungulia
[emoji117]6. Tumbo kujaa gesi
[emoji117]7. Tumbo kuwaka moto
[emoji117]8. Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
[emoji117]9. Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
[emoji117]10. Kusahahu sahau na
[emoji117]11. Hasira bila sababu.

Dalili au matatizo yote hayo hapo juu yanayompata mgonjwa wa vidonda vya tumbo ndizo ambazo kwa namna nyingine kama matokeo yake zinapelekea tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume wengi.

Kwa ushaur na tiba za magonjwa mbalimbali wasiliana nami

+255 655 821 550
Sulayman Sangida
 
Nimeshakucheki pm kwa msaada zaidi Bosi.
 
Naomba uniambie mkuu inatengenezwaje
 

Vidonda vya tumbo watu hawaponi kwasababu ya KUKIUKA MASHARTI. Mimi niliumwa vidonda vya tumbo kutoka 1999 Hadi 2006, nikapona, nililazwa Hindu Mandal. Nilichogundua ktk ugonjwa huu baadhi ya madaktari wanashindwa kutoa MASHARTI kwa mgonjwa wa vidonda.
Mfano mtu amemeza sawa za vidonda, labda Omeprazole au Gatrocides au Heligo Kit au Metronidazole akitoka hapo anakunywa chai na chapati ama maandazi ama ugali na mchuz wa kuunga au chpsi na NYAMA choma au Pombe, soda, pilipil au mtu anakuwa na hasira au mawazomengi. Sasa Mimi nimepona kwa sawa hizohizo za Omeprazole Limit na Heligo kits, tangu nimepona saiv miaka 13. Naomba niwashauri hivyo kula ugali na mboga ya isiyo na viungo vingi, mgonjwa wa vidonda haruhusiwi kunywa maziwa yenye gas
 
Mkuu hebu pangilia vizuri maelezo yako.kuna kitu tunaweza jifunza hapa.

Mimi nimetoka Aghakhan last week.Wamenifanyia kipimo cha Endoscope.Nina michubuko kama yote.Wamechukua vinyama flani(sample)kutoka tumboni.Wamepeleka Nairobi so wiki ijayo nakwenda kwa ajili ya kupata majibu kamili.pia wamesema safari hii watanipatia dawa itakayoniponyesha sababu inaezeka helicobacter(sina uhakika na spelling)wamekua sugu hawasikii dawa ndio mana siponi.
 

Nitumie namba yako nikupigie. Vidonda vya tumbo ni ugonjwa ambao haukawii kupokea dawa na kupona lkn watu hawaponi sababubya KUKIUKA MASHARTI, mfano hio X-ray uoiopiga OGB/umeiita Endoscope ni nzuri unaweza kuona vidonda ktk utumbo mpana Doudenum au X-ray ya Barium meal. Ok call me
 

Tungeanza kuwasiliana mapema nisingekwambia uende agha Khan ningekwambua ununue dawa na MASHARTI tu
 
Mkuu naumwa mda mrefu nimeshajaribu dawa za kila aina hadi mitishamba sipati nafuu.Nimejichokea sasa.Kama kuna namna ya kupata msaada ungeweka hapa kila mtu apate mana wenye matatizo kama yangu ni wengi.No yangu nimekutumia PM
Tungeanza kuwasiliana mapema nisingekwambia uende agha Khan ningekwambua ununue dawa na MASHARTI tu
 
Nichek inbox nikupe dawa utakunywa kama mara 4 hivi utapona kabisa
 
Habari za saa hizi wakuu,

Niende kwenye mada husika. Nina mwaka wa tano naumwa sana tumbo na maumivu yakiwa yanahama sehemu mbalimbali za tumbo wakati mwingine kifuani, kwenye, mbavu na hata kiuno na nyonga. Nimetumia madawa mbalimbali sipati nafuu.

Nimeshapima magonjwa kama yote. Nimejaza mafile ya makaratasi ya hospital. Natibu vidonda visivyopona. Sina raha nimepoteza ufanisi katika uchakalikaji wa kusaka kipato. Sina raha napata riziki si haba ila siifurahi. Sili ninachokitamani.

Nimeshafanya Endoscope 3 (mpira wenye kamera tumboni) zote zinaonyesha nina vidonda lakini nakunywa dawa siponi. Hii ya tatu nimefanya majibu yametoka baada ya week 3.Dokta kaniandika madozi mengine ila anipi ufafanuzi vizuri kama niko kwenye hali gani.

Niko stage gani? Ananiambia ni michubuko ya kawaida tu nitapona. kweli? mwaka wa tano mnanipa moyo tu? Aisee hata sielewi, nataka ukweli. Picha zinanishangaza nazidi pata wasiwasi zaidi. Na nimechoka kunywa dawa za hospital zinaniongezea maumivu hata sijui nifanyaje.

Tafadhali mtaalam yeyote ama aliyepitia changamoto kama zangu naomba msaada wako wa mali. Nishauri nifanyaje maana nilisikia mpaka mkojo wa asubuhi inaponya. Nilikunywa na sikupona.

Naambatanisha na majibu ya hospital pamoja na picha (OGD). Pia naomba kufahamu kwanini hii picha hapa chini ina vidude vyeusi ni alama ya vidonda kupona au ndio nazidi kulika.

Asanteni.


===

UFAFANUZI WA KITAALAMU KUHUSU TATIZO LA VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda vya tumbo ni nini?
Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana kama maji ya betri.

Vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao HELICOBACTER PYLORI, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non_steroids anti inflammatory drugs kama vile ASPIRIN /DICLOFENAC huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo.


AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE)
Kuna aina nyingi za vidonda vya tumbo navyo ni
(a) vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni
b) vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo
(c) vidonda vinavyotokea katika koo /koromeo la Chakula

HATUA KUU ZA VIDONDA VYA TUMBO
ni vizuri kufaham kwamba huu ugonjwa una hatua nne ambazo ni muhimu

(1)HATUA YA KWANZA ~hatua ya kwanza ya huu ugonjwa ni ule uvimbe sugu unaotokea sehem ya ndan ya tumbo.

(2)HATUA YA PILI~hapa vijidonda hujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hvyo huongezeka na kua vikubwa katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia, tumbo kujaa gesi wakati wote, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu.

Hata hivyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu (CHRONIC DYSPEPSIA) yani kushindwa kufanya Kazi kwa mfumo wa mmeng'enyo wa Chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni huingia Kwenye mzunguko wa dam hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayar iko katika mfumo mzima wa damu.

(3) HATUA YA TATU ~hii ni hatua ambayo ni ya hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa yote midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumbon na kubadilisha rangi ya choo kuwa cyo ya kawaida, pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara, maumivu makali ya tumbo,hupata Homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.

(4)HATUA YA NNE ~katika hatua saratani ya utumbo inahusika kwani katika hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo.

VISABABISHI/ VIHATARISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO
visababishi vya ugonjwa huu vipo vingi sana hivyo yatupasa kuviepuka ili kujiepusha na huu ugonjwa.zifuatazo ni visababishi vya ugonjwa huu
i. Utumiaji wa madawa ya kuondoa maumivu kwa muda mrefu
ii.mawazo na huzuni kwa muda mrefu
iii.kutokuwa na muda maalum wa kula
iv.Utumiaji wa pombe uliopitiliza
v. Utumiaji wa madawa ya kulevya nk

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
~Dalili za vidonda vya tumbo ni nyingi ila sio wote wanaopata Dalili hizi Wana vidonda vya tumbo
i. maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (EPIGASTIC PAINS)
ii. kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi Hali hii huweza kuendana na kucheua na kujamba Mara kwa Mara
ii. kutapika damu
iii. mtu mwenye vidonda vya tumbo (gastric ULCERS) hupata maumivu makali pindi anapokula au amalizapo kula
iv. mtu mwenye vidonda vya tumbo katika utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali pindi anapokua na njaa.
v. kupoteza hamu ya kula
vi. kupata haja kubwa yenye rangi damu Tena chenye harufu mbaya
vii. kupungua uzito

MATIBABU NA JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA HUU
~matibabu ya ugonjwa huu yanapatikana vizuri nchini mwetu ila tatzo ni tiba yenyew kutokua na wataalamu wa kutosha wa kutibu chanzo cha tatizo na kumaliza tatizo pasipo kuleta matatzo mengine kutokana na matibabu yenyewe kuhusisha mfumo wa dawa za kemikal ambazo zina madhara kwa mhusika na pia , hivyo tiba bora kwa vidonda vya tumbo ni mlo kamili na dawa zisizo na kemikal pia tunapaswa kuepuka baadhi ya vyakula na kuzingatia masharti.

MAMBO YA KUFANYA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO
i. epuka kula vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau
ii. epuka kutumia pombe
iii. epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi
iv. kula Chakula kidogo kwa muda maalum
v. kula vyakula vyenye fiber yan vyakula vyenye nyuzunyuzi ambavyo ni jamii ya mbogamboga na matunda
vi. epuka unywaji wa kahawa au kinywaji chochote chenye caffeine kiepuke
===
BAADHI YA USHAURI NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU
---
---
---
---
---
---
---

===
Pia unashauriwa kusoma:
1. Ushauri kuhusu dalili hatarishi za vidonda vya tumbo - JamiiForums

2. naomba kujua dawa asili ya Vidonda vya tumbo - JamiiForums

3. Yajue haya majani ni Dawa ya vidonda vya tumbo - JamiiForums

4. Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

5. Angalizo: Baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo hufanana na dalili za magonjwa ya moyo - JamiiForums
 
Pole mkuu, ngoja wataalamu waje ,ila nauliza tu hayo maumivu na wakati gani hasa hutokea, mfano labda ukila vitu vyenye acids nk?
Yes kama nikila embe, nanasi, (citrus zote) soda, majuis ya dukani, vitu vya baridi, viazi, nyama yaani kifupi sina chema tumbo linanivuruga wakati wote. Nikila kidogo tumbo linajaa gesi.

Nimekua mkali kama pilipili. kila saa mahasira, nachukia vitu vya kijinga hadi wakati mwingine najishangaa.
 
Inabidi uepuke vyakula vya gesi na vinywaji vyenye gesi na vichachu kabisa
Kula tikiti sana au papai lililoiva sanaa huondoa gesi tumboni.
 

Achana na hivyo vyakula kabisa
Je, ukinywa maziwa unajisikiaje
Maziwa fresh namaanisha
 

Mkuu, pole sana kwa changamoto uliyonayo. Usikate tamaa utapona tu.
Kwa ushauri, naomba tuanzie hapa kwenye vyakula. Kama ikiwezekana;

1. Epuka kabisa vyakula vyenye asili ya asidi kama matunda uliyoyataja hapo juu (maembe, mananasi, machungwa, machenza, ndizi mbivu nk pia epuka ndimu, pilipili, nyanya na kachumbari yake nk ) tumia matango kwa wingi na matikiti kwani yana asili ya alkali ambayo husaidia kupunguza asidi tumboni.

2. Epuka kula vyakula kama pilau, Chipsi na viazi kwa ujumla, dagaa, nyama za kukaanga, vyakula vyenye mafuta mengi (tumia mafuta wastani kwenye chakula) nyama choma, mkate na bait zote zenye hamira, maandazi, maharage, nk.

3. Epuka kunywa vinywaji vyote vyenye gesi, mfano soda - hii weka mbali kabisa, pombe zote, juice zote zenye uchachu, maziwa mgando nk.

4. Pia epuka kula na kushiba sana, kula kidogo kidogo mara nyingi. Kakikisha muda wako wa kula unajulikana na hauchanganyi ratiba ya muda wa kula. Ukiamka asubuhi, kunywa maji ya uvuguvugu walao glasi moja ama kikombe cha robo lita (hii iwe ni sehemu ya maisha yako mapya kama huwa hufanyi hivyo)

5. Epuka baadhi ya vidonge vya maumivu kwani huchangia kuumiza tumbo, utauliza vizuri kuhusu hili kwa madaktari ama wazoefu wengine.

6. Epuka hizo hasira kwani nayo inaongeza madhara kwa sababu unapokasirika kuna hali hutokea tumboni inayotokana na nyongo kumwagika na kuendelea kuunguza utumbo.

7. Sehemu kubwa ya mlo wako viwe ni vyakula vya mchemsho, kama ni supu isiwe na mafuta mengi na usiweke ndimu, wanasema limao ni zuri kwa sababu ni alkali ila kwa hali ya sasa usitumie kwanza.

8. Usile chakula chochote kilichoungua, epuka vitu vya kukaangwa kaangwa.

9. Epuka vyakula vyote vyenye nyanya, hakikisha nyanya sio sehemu ya milo yako kwa kipindi hiki

Wakati unatafuta tiba angalia yafuatayo;

1. Tafuta asali mbichi - ukipata ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi. Utumie kijiko kimoja kikubwa kila asubuhi na jioni. Ukipata mayai ya kienyeji pase, changanya yai bichi na asali kidogo kisha koroga na hakikisha vimechanganyikana, kisha unywe huo mchanganyiko, inasaidia sana tumbo.

2. Tumia mbogamboga kwa wingi, tafuta brokoli, zukini na vinginevyo kama kabichi, jifunze kuandaa bila kukaanga kisha kula na chakula kingine. kama ni wali ama ugali tumia kidogo kwa kipindi hiki kwani navyo huumiza hilo tumbo.

3. Kunywa maji ya kutosha kila siku - angalia pia kuna baadhi ya maji ya kunywa PH scale yake sio nzuri, PH ianzie 7.0 na sio chini ya hapon kama ni maji ya kununua.

4. Ndizi bukoba za kupika ukipata ndio ndizi za kula na si nyinginezo.

Kwenye tiba, tafuta tiba ya hao H.Pilori, vipimo vinaonesha wako wengi. Sijui wewe uko wapi maana kama uko Dar nenda pale Burhani, muone dokta Sidika asubuhi mpaka saa saba, aliwahi nipa dawa ya hao bacteria ikanisaidia.

Kwa sasa naomba tuanzie hapo. nikipata ndondo nyingine nitajitahidi kukuvunjia. ila pole sana Ambition plus.
 
Mkuu nashukuru sana ila baadhi ya vitu ulivyoshauri nimejitaidi kuepuka ingawa vingine nimeshindwa.

Nina rafiki wa kike ni Daktari uko uganda. Nimemtumia picha kama nilivyotuma hapo.

Kwa maelezo yake anasema helicobacter ni wengi sana. Hao ndio wanasababisha hio michubuko. Hata nikifata masharti yote siwezi kupona paisipo kuwaangamiza.

So kwa ushauri wake ameniambia nisile vile vinavyoniumiza kwa mda uku nikitumia dozi.Baada ya hapo ameniambia naweza kula kila kitu.Kwa maelezo yake kama nyanya ikipikwa hanidhuru basi nile ila kama inanidhuru niache kwa mda..

Pia kapendekeza matumizi ya tangawizi,kitunguu swaumu,mtindi,apple vinega,green tea,kabichi,embe tamu (nyuzi nyuzi ni muhimu) asali.Lakini nikigusa asali tumbo linavurugika vibaya sana.

Kwa maelezo yake hivo ni vyakula tiba sio rafiki wa helicobacter. Nimeshanga mana vitu vingine vinapingana.Unashindwa elewa kipi niache kipi nitumie.

Wataalam tafadhali tudadavulieni. Mkuu hakika nashukuru.nitamtafuta huyo daktari siki sio nyingi ama kama uko na mawasiliano yake yatanifaa sana. MWANASIASA HURU,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…