Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

 
Yap yap, lazma urud kuwapasha habari !
Mkuu kwema? Nitakribani mwezi sasa tangu unitumie dawa baada ya mm kushida offer yako hapa jukwaani..

Leo napenda kutoa ushuhuda kama ilivyo ada,kiukweli dawa yako ni nzuri sana maana tangu nimeitumia sioni shida zozote maana mwazo nilikuwa nasumbuliwa na tumbo kuuma na kujaa gesi ma kichefuchefu kwa sana lakn tangu nimetumia dawa hiyo mambo yako vzr kabisa na nimechukua mda mrefu kabla sijaja kusema hapa ili nihakikishe hiki ninachokiongea hapa,asanteni sana.
 
Bado sijapona

Tiba ya Vidonda vya tumbo ni kubadili utaratibu wa maisha.

Kula kwa wakati
Usile baada ya mbili usiku
Achana kabisa na vyakula vyenye gesi
Punguza stress
Fanya mazoezi
Kula matunda na mboga za majani
Anza Clinic hospital
Achana na pombe
Achana na Chipsi
Achana na vyakula vya ngano
Gonga sana Tangawizi na Asali
Kunywa maji vya kutosha


Mimi hili tatizo limenitesa sana lakini hayo niliyokuandikia yamenisaidia. Ukitaka Dr Mzuri nenda muhimbili kwa Dr Rwegasha anajua sana.
 
Wakuu habarini poleni namajukum mwenzenu nateseka namadonda yatumbo nimetumia dawa hospitalini nakienyeji hazijanisaidia mpaka Sasa mwenye kujua Tiba Zaid anielekeze
 
Ina maana vidonda tumbo haviponi?
 
Moja kwa moja kwenye mada wanajamii kma nilivyosema hapo juu ninavidonda vya tumbo naombeni msaada jaman kujua dawa hata za asili
 
Kama unasumbuliwa na vidonda vya tumbo njoo inbox. Nakuhakikishia unapona
 
Moja kwa moja kwenye mada wanajamii kma nilivyosema hapo juu ninavidonda vya tumbo naombeni msaada jaman kujua dawa hata za asili
Chukua maji ya vuguvugu kikombe kimoja cha chai kisha chukua kijiko cha chai cha binzari weka kwenye maji hayo na ukoroge vizuri kisha weka kijiko kimoja kikubwa cha asali kwenye mchanganyiko wako huo koroga tena na unywe kikombe
kimoja asubuhi, kingine mchana na kingine jioni. Tumia dawa hii kwa wiki tatu hadi mwezi kwa uwezo wa Mungu utakuwa umepona.

NB: Usile au kunywa vya viwandani na ambavyo vimetengenezwa kwa unga wa ngano
 
Binzari hii tunayoweka kwenye chakula wakati mwingine?

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru, mkuu kwa info. Kiukweli vinakera mbaya. Napenda sana kuwa high nyakati fulani.
Now naona ulcers pita kule. Serengeti lager zinanijua siku hizi. Naweka na kitimoto na pilipili ya kutosha kabisa
 
Jamani wanajamvi naomba msaada wenu nina vidonda vya tumbo vinanisumbua nasikia maumivu mpaka kwenye nyonga,hadi sehemu zinapoishia mbavu,nimetumia dawa za hospital wapi,je kuna tiba mbadala maana nasikia mkojo unatibu ni kweli?
Vipi sasa hivi mkuu umepona vidonda vya tumbo ni dawa gani ume tumia maana nahisi dalili kama zako pia.
 
Nunua pia unga wa majani ya mlonge tumia kwenye kinywaji ni njema sana mimi ndio sehemu ya chakula yangu. Jaribu uje toa feedback
Majani ya mlonge ni machungu au yana ladha gani mkuu ?! Pia ni tiba nzuri kwa madonda ya tumbo ?
 
Dawa gani ya kupunguza acid uli tumia ?!
 
Dawa gani ya kupunguza acid uli tumia ?!

Okay kuna Mizizi flani hivi ukitumia ina matokeo mazuri, hata kwa wale wasio ruhusiwa kula baadhi ya vyakula ila akitumia hiyo dozi imeleta matokeo chanya kabisa… Tumebarikiwa Miti tuitumie… ntakutajia jina ila hapa nalijua jina la huo mti kwakilugha ndo natafuta kiswahili chake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…