Acheni kumdanganya mwenzenu huwezi pona vidonda vya tumbo kwa maombi.
...neno lamsalaba kwa wanaopotea ni upuuzi mtupu, lakini kwetu sisi ni nguu ya Mungu iletayo wokovu...!
Ni magonjwa gani yanayopona kwa maombi? Naomba utuorodheshee, na nani anaweza kuyaponya hayo utakayoorodhesha. Pengine ukiweza unaweza kuzungumza hayo yasiyoweza kupoona kwa maombi yanapona wapi?
Wadau ninasumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa wiki Ya pili Sasa na maumivu yake hayavumiliki, nimeenda hospitali nimeishia kupewa antacid lakini hali ndo imezidi kuwa mbaya kuna ndugu aliniambia juice Ya kabeji inasaidia nayo nimejaribu lakini bado nafuu sijaipata naombeni ushauri kwa madaktari waliomo humu nifanye nini ili niweze kupima kabisa tatizo hili. Naombeni Kuwasilisha.
Ngoja nimwite mchungaji Peter Msigwa aje atoe ufafanuzi.
Ninakupa Dawa ya Muda tumia hii kwa muda wa siku 7 usipopona nitafute kwa wakati wako dawa ninayo ya
kuweza kukuponyesha Vidonda vya tumbo. Tumia hii Dawa kwanza:
Fanya hivi: Chukua viazi vya mviringo (vya chipsi) kama vitatu halafu uvikoshe na kuvimenya. Baada ya kuvimenya upate juisi yake kwa kuvisaga kwenye blenda. Kunywa vijiko vitatu vikubwa vya chakula kutwa mara mbili kila siku asubuhi na jioni kabla ya kula kitu kunywa hiyo dawa kwa muda wa siku 7.
Juisi ya Viazi mbatata.
Usipopona kwa muda wa siku 7 Nitafute mimini nayo Dawa ya kuweza kukuponyesha Vidonda vya Tumbo ukihitaji dawa bonyeza hapa.Mawasiliano
Nipo dar Mkuu Ila unaweza nielekeza nikamtumia mtu hapo makambako
Kaka sio kila kitu ni maombi tu, Mchungaji Gwajima pamoja na unguli wake wa "kufufua watu" alishindwa kujiomnea wala kuomnewa na alikimbilia hospital...neno lamsalaba kwa wanaopotea ni upuuzi mtupu, lakini kwetu sisi ni nguu ya Mungu iletayo wokovu...!
Peter Msigwa ndiye aliyeandika hapa? Nakutaka wewe mwenyewe mtz daima uje ujibu hoja. . Wewe unaandika halafu unataka Peter Msigwa akujibie.
Ninaomba ujibu hoja yangu bila kupotezea!.
By Tabby
Ni magonjwa gani yanayopona kwa maombi? Naomba utuorodheshee, na nani anaweza kuyaponya hayo utakayoorodhesha. Pengine ukiweza unaweza kuzungumza hayo yasiyoweza kupoona kwa maombi yanapona wapi?
By mtz daima
Acheni kumdanganya mwenzenu huwezi pona vidonda vya tumbo kwa maombi.
ni miti shamba au vidonge?
Ili utibu ugonjwa wowote lazima kwanza uelewe theories behind huo ugonjwa na uzuri ni kwamba tayari wataalamu wameshaandika hayo yote kuanzia visababishi, dalili na namna ya kutibu au kupunguza makali yake. Vidonda vya tumbo unapona kama utawahi maana nao una stages zake.
Kwa hiyo ili kumsaidia huyu ndugu yetu lazima akafanye vipimo kujua tatizo lake lipo hatua gani na kupewa matibabu stahiki kulingana na hatua hiyo (see specialist). Meanwhile mchanganyiko wa maziwa fresh na asali ya nyuki wadogo inasaidia sana kupunguza madhara/maumivu zaidi.
Hayo mengine ya maombi na magonjwa nenda youtube tafuta clip ya msigwa utaelewa vizuri
Nilitamani ungekuwa na uwezo wa kujibu swali langu, badala ya kunipelekea theories ambazo hata wewe huzijui.
Mada yetu mimi na wewe ilikuwa ni kupona kwa njia ya maombi. Wewe ukasema wanaoshauri aende kwenye maombi wanadanganyana kwa kuwa vidonda vya tumbo haviwezi kupona kwa kuombewa.
Ninachofahamu, mtu akiwa mgonjwa akapewa dawa sahihi na mwili wake ukakubali kushirikiana na ile dawa kupambana na ugonjwa ule, huwa anapona. Na ndiyo sababu watu huambizana kutumia dawa mbali mbali kwa matatizo ya afya kwa kuwa wanashuhuda kwamba zilishawahi kuwasaidia watu wakapona. Ama wana uhakika zinauwezo wa kupambana na tatizo husika katika mwili wa mwanadamu.
Mtu anapokwenda kwenye huduma za maombi, ni nnini huwa kinawaponya?