Nilitamani ungekuwa na uwezo wa kujibu swali langu, badala ya kunipelekea theories ambazo hata wewe huzijui.
Mada yetu mimi na wewe ilikuwa ni kupona kwa njia ya maombi. Wewe ukasema wanaoshauri aende kwenye maombi wanadanganyana kwa kuwa vidonda vya tumbo haviwezi kupona kwa kuombewa.
Ninachofahamu, mtu akiwa mgonjwa akapewa dawa sahihi na mwili wake ukakubali kushirikiana na ile dawa kupambana na ugonjwa ule, huwa anapona. Na ndiyo sababu watu huambizana kutumia dawa mbali mbali kwa matatizo ya afya kwa kuwa wanashuhuda kwamba zilishawahi kuwasaidia watu wakapona. Ama wana uhakika zinauwezo wa kupambana na tatizo husika katika mwili wa mwanadamu.
Mtu anapokwenda kwenye huduma za maombi, ni nnini huwa kinawaponya?