Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Me ninatatizo hilo tokea 2008

Kwa kweli ni changamoto sana hasa kwenye ushauri, kunamtu utamfuata Atakwambia tumia pilipili sana na rimao mwingine atakwambia achakabisa hivyo vitu
Wengine wanasema maziwa yanasaidia na wengine wanasema yaathiri zaidi
Wenye tatizo hili tunapata ushauri mwingi mmno tena huwa unakinzana kiasi kwamba huelewi kipi ni sahihi.
 
Mie dawa siijui ntashare nanyi nini sasa.. nilichosema ni kwamba aje nimpe mawasiliano nae, kwani akija pm ndio nitawafanya nini, kama ningehitaji kitu mimi ndio ningewafata huko pm kwanza..

Siwez kuweka namba hapa.. samahanini kwa hilo.
Sikukulenga wewe braza, kwani maelezo yako yalijitosheleza na hongera sana kwa hilo,

Ila kuna watu walimuita pm ukisoma comments utaona.
 
Mkuu Ni kama Nimeyasikia Maumivu Yako.Mimi Niliumw Kipindi Flani Nyuma..Mpaka Stage Ya Kutapika Damu.Nikatumia legalkick.Bado Mambo Yakawa Bado na Dozi Ilikuwa ndefu Nikawa nashidwa Kuimaliza..Ilikuwa ni Kama Mgojwa wa Kutumia Arvs..Nika achana Nazo Na Kuanza Kutumia Dawa za Kienyeji.

Sasa Fanya Hivi
.CHUKUA asali Ya Nyuki wadogo,Changanya Na Maziwa Fresh,Na parachichi,Na mayai Ya Kienyeji,Changanya Mchanganyiko kwa Pamoja.Kunywa Asubuhi,Mchana na Jioni.One week Utaona dalili Nzuri.
ILA kwa Maelezo Yako..stage Uliyofikia.Tumia Hii dawa Uku Ukitumia Dozi Ya hospital.Pole Sana Mkuu
 
Ninyi mnao muita inbox kwann msitoe hapa hiyo tiba ili na wengine wanufaike nayo??? huko inbox mnataka kuwafanya nini wenzenu.....
sio vizuri kama unajua kitu flani ukashare kwa wenzio hata baraka zinaongezeka.
Ukishaona msg ya njoo inbox jua tu huyo ni tapeli
 
Baada ya kuona pm nimefatwa na wtu kadhaa, nimejaribu kuonhea na dada, akanipa maelezo ya dawa.. nimeamua kushare nanyi hii msg niliyomtumia ndugu Mu7 maana waliokuja pm no wengi tofauti na matarajio, so msg niliyomjibu pm ndio nitaweka hapa.
 
Kwanza ndugu yangu yangu tumshukuru mwenyezi mungu kwa kila jambo, imani yangu inaniambia kila jambo Allah analotupa ni mtihani aidha tumshukuru ama tumkufuru, sasa mimi napenda tuwe wenye kumshukuru yeye, tusifeli mtihani wake..

Dada nimeongea nae kwa kirefu, kanieleza dawa yake na tumuombe mwenyezi mungu kupitia dawa hii upate afya.. labda nikueleze kisa kifupi, nabii mussa a.s alipata maradhi sikumbuki ni maradhi gani, tiba hakuwa akiijua, akamuomba mwenyezi mungu ampe dawa ya maradhi yake, mungu akamuelekeza dawa, akatumia na akapona, mungu akampa tena maradhi yale yale mussa akaenda kuchukua dawa ile akanywa na hakupona, akangeza dozi akatumia wee na hakupona akamlalamikia mola wake mbona haponi, mungu akamwambia dawa ni sababu tu ila akuponyeshae ni mimi, kwa maana ya mungu.. sisi tumeumbwa kisayansi na aliyetuumba ndio anajua zaidi.. hili ni somo refu kidogo


Sister kanieleza dawa hii.. asali na mdalasini.. nakupa maelezo ya lita moja

Matayarisho
Chukua asali yenyewe, asali halisi sio haya masukari ya mjini(asali fake) ikiwa ya nyuki wakubwa inapendeza zaidi.
Chukua magome ya mdalasini, ni vyema kupata magome maana unga wake wajanja wajanja huwa wanauchakachua na kusaga na magome mengine.
Katika lita moja ya asali tia vijiko 5 vya unga wa mdalasini.

Matumizi
Asubuhi nusu saa kabla hujala chochote changanya vijiko viwili vya dawa yako katik maji moto unywe
Mchana kabla ya kula meza vijiko viwili hapa si lazima uchanganye na maji, hapa ni vikavu
Na usiku ni hivyo hivyo kama mchana tu


Nyongeza: chai yako tumia mdalasini usitumie majani ya chai, usinywe maziwa na vyakula vyote ambavyo serikali walikukataza, epuka juice ya ukwaju na nyinginezo kama hizo.

Amesema yeye alitumia kwa muda upatao miezi mi3 hiv ndio akaanza kuona matokeo chanya..

Kila la kheri ndugu yangu, mwenyezi mungu atakufanyia wepesi katika hili, akupe afya njema inshaallah.
 
Niliupoteza huu Uzi

Kiboko ya Dawa zote hizi ni Juice ya Kabichi au Cabbage wazungu wanaiita.

•Cabbage/Kabichi
•Muwa au Apple
•Maji Safi

Saga mchanganyiko huu kwa Blender hadi upate Juice nzito nzito.

Kaza Moyo maana ladha yake Mhhh Kunywa Juice hii Glass kubwa 2 au 1 kutwa mara tatu. Alafu njoo tupe mrejesho.


Dawa nyingine nzuri pia ni Juice ya mboga za majani na matunda ( Detox )

•Mboga yoyote Ya Majani isiyokuwa na Acid
•Muwa
•Mtindi
•Maji Safi
•Apple

Saga huo Mchanganyiko kwenye blender kunywa utakavyoweza itakusaidia sana.


Katika zote hiyo ya Cabbage ni nzuri zaidi.

Angalizo: Usiweke Sukari hata kidogo. Uwepo wa Muwa na Apple ni kuleta hiyo ladha ya Utamu hata mtindi ni vizuri ukitumia ule wenye ladha za matunda.
 

Niliupoteza huu Uzi

Kiboko ya Dawa zote hizi ni Juice ya Kabichi au Cabbage wazungu wanaiita.

•Cabbage/Kabichi
•Muwa au Apple
•Maji Safi

Saga mchanganyiko huu kwa Blender hadi upate Juice nzito nzito.

Kaza Moyo maana ladha yake Mhhh Kunywa Juice hii Glass kubwa 2 au 1 kutwa mara tatu. Alafu njoo tupe mrejesho.


Dawa nyingine nzuri pia ni Juice ya mboga za majani na matunda ( Detox )

•Mboga yoyote Ya Majani isiyokuwa na Acid
•Muwa
•Mtindi
•Maji Safi
•Apple

Saga huo Mchanganyiko kwenye blender kunywa utakavyoweza itakusaidia sana.


Katika zote hiyo ya Cabbage ni nzuri zaidi.

Angalizo: Usiweke Sukari hata kidogo. Uwepo wa Muwa na Apple ni kuleta hiyo ladha ya Utamu hata mtindi ni vizuri ukitumia ule wenye ladha za matunda.
 
Asante sana ndugu kwa mchango wako.
 
Muuone dokta kingu ifakara morogoro anakupa dawa moja local siku mbili tu Keisha hizo habari .Mimi hata pilau nilikuwa sili ila sasa hivi nakula hadi pilipili.
 
Ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…