Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Wakuu habari za weekend naomba kujuzwa kama kuna dawa ya kiasili ya vidonda vya tumbo nikapona kabisa asanteni
Dawa ya asili ya kutibu vidonda vya tumbo na ukapona kabisa mimi ninayao ukitaka bonyeza hapa.Mawasiliano

MziziMkavu tafadhali pita pande hizi
Pole sana ninakupa Dawa ya muda wa kutibu vidonda vya tumbo tumia kwamuda wa siku 7 usipo pona nitafute ninayo Dawa itakayoweza kukuponyesha ukapona kabisa kwana tumia Dawa hii hapa chini:

Dawa Ya Vidonda tumbo:

Kula kipande cha papai kisichoiva vizuri kila siku alfajiri, ukimaliza shushia na mbegu moja tu ya kitunguu swaumu. Hakikisha unazidisha kiwango cha kunywa maji siku zote utakazo jitibia vidonda hivyo, na ikifika siku 13 hadi 16 utanipigia simu kunitaarifu kuwa vidonda vimepona.

Kama kipato chako ni kidogo na kupata papai kila siku ni gharama, basi usikonde. Chuma majani mawili ya mpapai kisha katakata kama mboga ya kupikwa, tia katika chupa kubwa ya lita mbili za maji na kunywa kutwa nzima kidogo kidogo hadi yaishe. Waweza kutia vipande vya mapapai machanga yaliyokatwakatwa pia badala ya majani.
 
Attachments

  • vidonda vya tumbo.jpg
    vidonda vya tumbo.jpg
    22.3 KB · Views: 313
Habarini JF members.
Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo viko kwenye stage za mwanzomwazo. Kutokana na maelezo ya watu mbalimbali wanasema kua ugonjwa huu hauponi kabisa ila unatulia tu ukimeza dawa.
Please wadau naomba kujua dawa nzuri inayoweza tibu maradhi haya hata kama ni hizi za asili.
Ahsanteni.
 
Mie kuna dawa nimeambiwa kwani name ni muhanga wa vidonda vya tumbo: chukua nyanya cungu 5 bamia 10 chemsha na maji kama lita 2 acha yachamke sana hadi yapungue usiweke chochote hata tone la chumvi chuja ondoa zile bamia na nyanya chungu hakikisha unapata glass moja kubwa ya maji utakayo chuja acha yapowe kidogo hadi iwe uvuguvugu kuwanya glass yote kwa mkupuo, zoezi hilo lifanye kwa muda wa siku 7 nikimaanisha kila siku unachemsha nyanya chungu na bamia nyingine kwakipindi hicho cha siku 7. Nimeanza hilo zoezi jana
 
Poolee usipopona unitafute
 
matibabu yanategema na sababu za vidonda...
kama ni kutokana na maambukizi ya bacteria tumia anti-acids na antibiotic, na kama sababu nyngne tu mbali na infections tumia anti-acids kupunguza uzalishwaji wa acid na kukipa kidonda nafasi ya kupona chenyewe..
 
Habarini JF members.
Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo viko kwenye stage za mwanzomwazo. Kutokana na maelezo ya watu mbalimbali wanasema kua ugonjwa huu hauponi kabisa ila unatulia tu ukimeza dawa.
Please wadau naomba kujua dawa nzuri inayoweza tibu maradhi haya hata kama ni hizi za asili.
Ahsanteni.

Tafuta dawa inaitwa Helgo kit, tumia kwa muda wa wk mbili kisha ikifuatiwa na lanzoprazole kwa wiki tatu.
Helgo kit ina mchanganyiko wa dawa za kuua bacteria(antibiotics) na kupunguza uzalishwaji wa acidi tumboni.
Ukimaliza hiyo Helgo kit sasa piga lanzoprazole ili kutibu vidonda kwani kwa wakati huo bacteria watakuwa washaondoka.

I'm speaking from uzoefu, ndugu yangu alifanya hivi na sasa n buheri wa afya. Alishasahau kama alipata stomach ulcers!!

Ila sasa ili upone fuata masharti, kama unatumia pombe basi inabidi uacha hasa ukiwa unatumia dawa, na pia pombe ina alcohol ambayo husababisha kuchelewa kupona kwa vidonda.
Pia zingatia kutumia matunda kama ndizi(huongeza ute? Kamasi?) ambazo husaidia kulinda utumbo dhidi ya bacteria, asali(ina hydrogen peroxide ambayo huua bacteria) . Pia waweza tumia vitunguu swaumu(garlic)

Hivyo hivyo mkuu jaribu kunielewa, mana naandika nimechoka, nashindwa ku organize vizuri maelezo.
 
Mie kuna dawa nimeambiwa kwani name ni muhanga wa vidonda vya tumbo: chukua nyanya cungu 5 bamia 10 chemsha na maji kama lita 2 acha yachamke sana hadi yapungue usiweke chochote hata tone la chumvi chuja ondoa zile bamia na nyanya chungu hakikisha unapata glass moja kubwa ya maji utakayo chuja acha yapowe kidogo hadi iwe uvuguvugu kuwanya glass yote kwa mkupuo, zoezi hilo lifanye kwa muda wa siku 7 nikimaanisha kila siku unachemsha nyanya chungu na bamia nyingine kwakipindi hicho cha siku 7. Nimeanza hilo zoezi jana

Hii nzuri
 
Habarini JF members.
Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo viko kwenye stage za mwanzomwazo. Kutokana na maelezo ya watu mbalimbali wanasema kua ugonjwa huu hauponi kabisa ila unatulia tu ukimeza dawa.
Please wadau naomba kujua dawa nzuri inayoweza tibu maradhi haya hata kama ni hizi za asili.
Ahsanteni.

Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.

Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni.

Hebu tuangalie aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:

USHAURI WANGU FANYA HIVI:

VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI

Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.

POMBE NA KAHAWA

Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];caffeine', vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.

ULAJI CHUMVI

Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.

MAFUTA YA SAMAKI

Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.

VITAMINI NA MADINI

Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.

STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO

Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha.

Dawa ya kuponyesha kabisa Vidonda vya Tumbo ninayo ukihitaji Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Wakuu habari ! Je,kuna ukweli kwamba mafuta ya mkia wa kondoo yanatibu vidonda vya tumbo unapoyanywa ? Naomba usahihi.
 
Mie kuna dawa nimeambiwa kwani name ni muhanga wa vidonda vya tumbo: chukua nyanya cungu 5 bamia 10 chemsha na maji kama lita 2 acha yachamke sana hadi yapungue usiweke chochote hata tone la chumvi chuja ondoa zile bamia na nyanya chungu hakikisha unapata glass moja kubwa ya maji utakayo chuja acha yapowe kidogo hadi iwe uvuguvugu kuwanya glass yote kwa mkupuo, zoezi hilo lifanye kwa muda wa siku 7 nikimaanisha kila siku unachemsha nyanya chungu na bamia nyingine kwakipindi hicho cha siku 7. Nimeanza hilo zoezi jana

Ahsante sana mdau. Ningependa pia nipate feedback baada ya kutumiaunaendeleaje sasa? Maana dawa za ugonjwa huu ni nyingi sanaa lakini.
 
Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.

Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni.

Hebu tuangalie aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:

USHAURI WANGU FANYA HIVI:

VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI

Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.

POMBE NA KAHAWA

Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye ‘caffeine', vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.

ULAJI CHUMVI

Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.

MAFUTA YA SAMAKI

Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.

VITAMINI NA MADINI

Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.

STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO

Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha.

Dawa ya kuponyesha kabisa Vidonda vya Tumbo ninayo ukihitaji wasiliana na mimi kwa kubonyoza hapa.
Mawasiliano

Ahsante MziziMkavu nitakucheki.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongezea, dawa kubwa ya vidonda vya tumbo ni kuachana na hofu, hasira, uwe mtu wa kusamehe na kuzingatia mlo usio kuletea maumivu na ule mapema mlo wa usiku kabla ya kwenda kulala yaani kabla ya saa moja usiku.
 
Chukua kokwa za parachichi kata kata vpande anika kisha twanga ili kupata unga raini {chukua yai 1 la kuku wa kienyeji changanya na kijiko k1 cha unga huo kunywa! fanya hivo kutwa mara 3 kwa siku 3} Insha allah utapona!
 
Habarini JF members.
Nasumbuliwa na vidonda vya tumbo viko kwenye stage za mwanzomwazo. Kutokana na maelezo ya watu mbalimbali wanasema kua ugonjwa huu hauponi kabisa ila unatulia tu ukimeza dawa.
Please wadau naomba kujua dawa nzuri inayoweza tibu maradhi haya hata kama ni hizi za asili.
Ahsanteni.

Mkuu ankol mimi nilikuwa na vidonda vya tumbo na ndivyo vilikuwa vinaanza nilitumia Asali mbichi+ Maziwa ya chai tu, kwa muda wa wiki moja mpaka leo hii sijasikia.

Usitumie maziwa haya ya unga.
 
Last edited by a moderator:
Mtu asipopona kwa siku ulizosema utamrudishia pesa zake?
 
Back
Top Bottom