Ndg zangu naomba msada nasumbuliwa na vidonda vya tumbo je tiba yake nini au siluhusiwi kutumia nin.nashukulu kwa ushilikiano wenu
Pole Eric....Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer Disease) vinasababishwa na kutolewa kwa acid nyingi sana tumboni (tumbo kwa kawaida hutoa acid ambayo husaidia kataika kumeng'enya chakula). Acid inapotolewa kwa wingi, na ukuta wa tumbo (gastric wall) ukiwa dhaifu, na mara nyingi akiwepo bakteria anaitwa
helicobacter pylori...baasi utapata vidonda vya tumbo. Vinaweza viakawa tumboni kwenyewe (Gastric Ulcers), hivi mara nyingi vinauma baada ya kula kwani ndio acid hutolewa kwa wingi. Au vikawa mwanzoni mwa utumbo mdogo (Duodenal Ulcers), hivi mara nyingi vinauma ukiwa na njaa..ukila vinapoa!
Umejuaje una vidonda vya tumbo? Mara nyingi vidonda vya tumbo huwa na dalili za maumivu ya tumbo kwenye chembe ambayo unayasikia kama yanaendelea mpaka mgongoni, maumivu yake yanakuwa ya kuchoma (kama kiungulia kikali). Kipimo cha kuthibitisha kinaitwa 'OesophagoGastroDuodenoscopy" au OGD, ambapo unaingizwa kama kampira fulani kadogo chenye kamera mdomoni, so kana piga picha kwenye koo (Oesophagus), tumbo na mwanzo wa utumbo mdogo..na vidonda vinaonekana. Pia kipimo cha damu cha kuangalia kama kuna huyo bacteria
H.Pylori (serology for
H.Pylori).
Matibabu yake mara nyingi ,i dawa za kumeza...inakuwa mchanganyiko wa dawa tatu ukijumuisha anti-acid 1 (Omeprazole, Lansoprazole, Pantoprazole, au Esomeprazole etc.) na antibiotics 2 (mara nyingi Clarithromycin na Amoxycillin). siku hizi kuna dawa ambayo imechanganya zote hizo pamoja inatwa 'Heligo Kit'. Huo mchanganyiko ni kwa siku saba tyhen unaendelea na anti-acid kwa muda mrfu kidogo mpaka utakaposhauriwa na daktari wako vinginevyo.
Japokuwa vidonda vya tumbo vinauma sana, unashuriwa usimeze dawa za kupunguza maumivu aina ya NSAIDs (mfano diclofenac, brufen etc) ambazo zinatumika sana kwa maumivu kwani zinafanya vionda vichimbike zaidi. Pia usitumie Aspirin na Steroids kwa muda mrefu.
Epuka vyakula vyenye asili ya acid mfano matunda yenye uchachu kama embe, machungwa, limau, ndimu, passion etc..navyakula vinasababisha acid itoke kwa wingi kama maharage, viungo vikali kwenye chakula, pilipili etc..