Nyie ndo mnaotuulia watanzania kabisa!
Asilimia 90-100% ya watu wenye vidonda vya tumbo lazima wamesabibishiwa na bacteria anaitwa H.Pyroli.
Rejea hii tafiti
The prevalence of Helicobacter pylori in peptic ulcer disease. - PubMed - NCBI
Katika visababishi vyako vya vidonda vya tumbo haujataja huyo mdudu umeishia kutaja vitu kama msongo wa mawazo ambavyo vilishaacha kuaminika kuleta vidonda vya tumbo.
Katika tiba zako hizo hakuna tiba inayoweza kumuua H.Pyroli hivo unawaua watanzania wazi wazi maana complication ya hivo vidonda ni kwamba kuna siku vinaweza toboka usipovi control au kuvitibu na unajua tumbo likitoboka usipofanyiwa upasuaji wa ku repair unakwenda na maji...Majirani zako wanaishia kusema utakua ulilogwa kumbe haukutibu vidonda vya tumbo inavyotakiwa.
Kuna dawa kama Diclopa ambazo watanzania wengi wanazitumia na wnegine huzitumia kwa mda mrefu labda wale wenye joint pain au maumivu ya mgongo.
Dawa hizi jamii ya NSAIDS zinapunguza ile mucus/ute unaolinda kuta za tumbo dhidi ya acidi inayotolewa kwenye mfumo wa chakula!
Hivo ukiondoa ute huu kwa kutumia hizo dawa unazidi kujimaliza!
Nafikiri itabdi niandae somo kwa ajili ya vidonda vya tumbo ili watanzania walioko humu jukwaani waache kudanganyika!