huyu jamaa naiman ashamaliza kutumia dawa, coz ndo alikua mtu wa kwanza kat ya wale wawili waliopata nasaf ya upendeleo !!
Mzee wa Tit4tat watu wanasubiria feedback uku Mkuu
Yap mkuu nipo sema harakati kibao hivyo nikashindwa kuleta mrejesho kwa Muda muafaka.
Ila tu kwa ufupi tangia siku ya kwanza kutumia nikaona tofauti na hadi sasa shida ya vidonda vya tumbo siisikii maana pia nilikuwa na hofu nikidhani labda dawa imetuliza tu kwa muda na vinaeza kufumuka muda wowote tena Lakini hadi sasa napiga kila chakula kuanzia maharagwe, kauzu ndizi mbivu, wali, maziwa ya mgando na vingine vyote ambavyo hapo awali nilikuwa situmii coz vilikuwa vikinidhuru.
Niseme tu shukrani sana Bob laidoo kwa kunisaidia dawa tena free wala sijainunua Mungu akubariki sana tena sanaaa mkuu kwa hiki alichokifanya kwa ajili yangu na kwa wengine
Maana nimesumbuka sana kwa miaka mingi takribani miaka 6 na nimetuma dawa kibao ila sijawahi kupona zaidi zaidi tu kutuliza maumivu.
Kwa wale ambao bado hawamini kuhusu hii dawa ya huyu bwana mkubwa nawaambia wasiwe nashaka japo hata mm nilikuwa siamini kabla sijatumia, na hii yote ni kutokana na watu tofauti tofauti kuniaminisha dawa fulani inaponya ila haziijawahi kunisaidia.
Na kama pia kuna mtu anadhani Jamaa ni tapeli au mwongo nasema hapana jamaa ni mtu safi sana na anajiamini ndio maana anakupatia dawa bure na anakuambia tumia kwa muda huo wa siku 4 kisha nenda kapime hospitali ili uone kama shida ipo au haipo hii ni moja ya sababu ya mm kumuamini yy.
Bob laidoo ww ndiye umethibitisha ule msemo wa hakuna kinachoshindikana chini ya jua
Kiukweli nilisha kata tamaa ya hivi vidonda coz wengi waliniaminisha ukivipata umepata na huwezi pona zaidi ya kuvitulia tu.
Kumbe kuna mambo tunayakweza tu na kuyapaisha kwa kuona hayatibiki kisa yametutesa kwa muda mrefu.
Hebu fikiria miaka 6 ndani ya mateso ukiangaika huku na kule bila solution halafu anatokea mtu anakutibu ndani ya siku nne.[emoji120].