Je hiyo ni bei ya kichupa hicho kimoja tu? Au ndiyo full dose? Kuna verification yoyote ya mgonjwa kupona? Au ni loliondo style! Je muna utaratibu wowote wa kufuatilia maendeleo ya mgonjwa? Au akishanunua product yenu ndio hakuna kujuana tena,afe, apone ni shauri yake!! Kiasi cha pesa nilichotumia mpaka sasa kujitibu vidonda vya tumbo ni sawa na gharama ya kujenga dispensary ya kijiji,na bado tatizo liko palepale, je hii ya kwako ina tofauti gani kimsingi na nyingine nilizotumia? Hadi sasa nimeshabugia KIKOMBE cha loliondo,fiterawa,vitunguu swaumu,juice ya kabeji nyekundu,asali na maziwa ya ngamia nk,nijibu hayo nitakuja mbio kupata tiba yako, asante.