Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Mkuu HardMartin Unapo amka asubuhi kabla ya kula kitu kinga mkojo wako mwenyewe kipimo cha glasi moja kila siku kunywa kwa muda siku 7 kisha uje unipe feeback.

nashukuru sana Mkuu baada ya hzo siku 10 ntakuja kufunguka jukwaan kutoa matokeo lakin kipndi hcho chote ntakachokuwa natumia hii cjajua kama natakiwa niwe katka life style gan? hasa kwa upande wa chakula na vtu vingine
 
Last edited by a moderator:
nashukuru sana Mkuu baada ya hzo siku 10 ntakuja kufunguka jukwaan kutoa matokeo lakin kipndi hcho chote ntakachokuwa natumia hii cjajua kama natakiwa niwe katka life style gan? hasa kwa upande wa chakula na vtu vingine
Mkuu HardMartin Kawaida tu tumia dawa hiyo haina masharti yoyote tumia kwa muda wa siku 10 kisha nenda kapime utakuta huna vidonda vya tumbo vitakuwa vimekauka kabisa inshallah ukimaliza njoo uje hap utupe maendeleo yako umepona au bado?
 
Last edited by a moderator:
Maoni zaidi yanahitajika wanajamii. Lengo ni kukabiliana na tatizo la kiafya na kuzidi kupata elimu zaidi na jamii husika inayotuzunguka pia
 
hakuna swali hapo bro!Ila unataka kukamua maziwa beberu!

Jamaa anaitwa "AFYA" au "Health" anauza "supplements" toka ughaibuni (UYOGA wa INDIA) kwa gharama kubwa lakini cha kusikitisha bado watanzania wengi wanatumia gharama kubwa kwenda INDIA kwenye matibabu.. kwa nini hivi vichupa kama vinatibu msiwauzie MSD au mpeleke pale Muhimbili ikawa nafuu kwa wagonjwa wengi??
 
Jamaa anaitwa "AFYA" au "Health" anauza "supplements" toka ughaibuni (UYOGA wa INDIA) kwa gharama kubwa lakini cha kusikitisha bado watanzania wengi wanatumia gharama kubwa kwenda INDIA kwenye matibabu.. kwa nini hivi vichupa kama vinatibu msiwauzie MSD au mpeleke pale Muhimbili ikawa nafuu kwa wagonjwa wengi??

Huo ni mtazamo wako
 
ndugu wana jf heshima kwenu na heri ya mwaka mpya
nina dawa nzuri ya vidonda vya tumbo ni ya kienyeji inakutibu baada ya wiki3 mpaka mwezi tatizo lako linakuwa limekwisha.kwa maelezo zaidi nitafute kwa namba 0714074040
 
Habari zenu wakuu,
kama wk 2 zlzopta nilitumia chlorophenical vdnge 84 na ulaji wangu haukua mzri sana sasa hv tmbo halko swa kuna namna lnauma uma hv so nahsi labda ni vdnda, naomba kma kna mtu anajua dall zake na hata tba ansaidie
nawaslsha
 
UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCER DISEASE)
peptic-ulcer.jpg

Image Source: MedicineNet, Inc.



Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu.

Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo.

Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama Helicobacter pylori. Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non Steroid Anti-inflamatory Drugs kama Aspirin au Diclofenac huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu.

Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (stomach). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama duodenum.

Makundi ya PUD

Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu
1. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo (Gastric ulcers)
2. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (Duodenal Ulcers)
3. Vidonda vinavyotokea kwenye koo (Oesophageal ulcers)
4. Vidonda vijulikanavyo kama Merckel’s Diverticulum ulcers.

Visababishi vya PUD
Vidonda vya tumbo husababishwa na

Maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori: Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo (gastric ulcers) na zaidi ya asilimia 90 yaduodenal ulcers.

Hali hii husababishwa zaidi na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili. Matokeo ya kushindwa huku husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo (chronic active gastritis), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya Gastrin, ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali.


Kwa kawaida, kazi ya gastrin ni kuchochea utolewaji wa tindikali (gastric acid) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Parietal cells. Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa gastrin pia uharibika, na hivyo kusababisha gastrin kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa gastric acid kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo.


Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs:
Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo

na tindikali ya utumbo (gastric acid) kwa kuwa na utando laini (mucus) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Prostaglandins. Dawa hizi za kundi la NSAIDs huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani prostaglandins na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo.


Uvutaji wa sigara:
Uvutaji sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike tu kuwa uvutaji sigara pekee hausababishi vidonda vya tumbo.


Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu:
Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.


Watu walio katika kundi la damu la O:
Imeonekana pia kwamba kundi la damu lijulikanalo kama blood group O, halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo.


Unywaji wa pombe:
Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya Helicobacter pylori huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo.


Vitu vingine:
Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo (major abdominal surgeries), kuungua kwa moto (burns), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini.


Dalili au viashiria vya PUD

Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo (epigastic pains): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo (gastric ulcers) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada

ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula.


  • Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara.
  • Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua.
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
  • Kutapika damu
  • Kupata haja kubwa cha rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali
Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa za kupunguza maumivu (NSAIDs) kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo.

Vipimo vya kutambua Ugonjwa wa vidonda vya tumbo

Vipimo vinavyotumika katika kutambua tatizo la vidonda vya tumbo ni pamoja na

1. Vipimo vya kuangalia ndani ya utumbo ambavyo ni pamoja na


  • Kipimo cha oesophagogastroduodenoscopy (EGD) au Upper GI endoscopy au gastroscopy. Kwa kutumia kipimo hiki, daktari huangalia moja kwa moja ndani ya utumbo wa mgonjwa kuona sehemu iliyo na vidonda pamoja na ukubwa wa tatizo lake. Aidha vipimo hivi humuwezesha daktari kuchukua sehemu ya utumbo iliyoathiriwa kwa ajili ya kuchunguza zaidi maabara ili kutambua uwepo wa vidonda au tatizo jingine linalomsumbua mgonjwa tofauti na vidonda vya tumbo.
  • Kipimo kingine kijulikanacho kama Barium meal kina uwezo pia wa kuthibitisha uwepo wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo.

2. Vipimo vya kutambua uwepo wa uambukizi wa bakteria aina ya Helicobacter pylori kama


  • Kipimo kiitwacho Urea breath test
  • Kipimo cha kuotesha kinyama kilichochukuliwa kutoka katika kipimo cha OGD (culture from an OGD biopsy specimen).
  • Kipimo kinachoitwa Rapid Urease Test ambacho hufanywa kwa kutumia kinyama kilichochukuliwa kutoka kwenye utumbo wakati wa kufanya OGD. Kipimo hiki huangalia tabia ya vimelea hawa wa H. pylori.
  • Kipimo cha damu kwa ajili ya kutambua kiwango cha maambukizi ya vimelea wa H. pylori (antibody levels).
  • Kipimo cha haja kubwa kwa ajili ya kutambua kama bacteria wapo hai au wamekufa (stool antigen test). Kipimo hiki ni cha uhakika zaidi na nafuu kuliko kipimo cha Urea Breath Test.
  • Kipimo cha kimaabara cha kuchunguza kinyama kilichochukuliwa wakati wa kipimo cha OGD.

3. Vipimo vingine maalum vya kitaalamu zaidi kama


  • Kiwango cha homoni ya gastrin katika damu
  • Kipimo cha kuangalia uzalishaji wa homoni ya secretin ambayo uhusika katika uchocheaji wa homoni yagastrin
  • Kupima kiwango cha tindikali inayozalishwa katika tumbo.
Hata hivyo vipimo hivi ni vya gharama zaidi na ni aghalabu hutumika mara kwa mara.

Matibabu ya Ugonjwa wa vidonda vya tumbo


Habari nzuri ni kuwa ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo unatibika. Hata hivyo tabia ya baadhi ya wagonjwa wengi kuacha kumalizia dawa au kutumia dawa chini ya kiwango tofauti na walivyoshauriwa na madaktari husababisha kujirudia kwa tatizo au kufanya tatizo kuwa sugu zaidi.


Iwapo itagundulika uwepo wa H. pylori tiba inayotumika ni kuchanganya dawa za antibayotic (antibiotic) za aina tofauti kama Amoxicillin, Tetracycline, Clarithromycin au Metronidazole na dawa zenye uwezo wa kupunguza uzalishaji wa tindikali kwa wingi au kwa kitaalamu Proton Pump Inhibitors (PPI). Wakati mwingine daktari anaweza pia kuongeza dawa ya Bismuth Compound.


1. Kwa wagonjwa sugu, dawa za antibioc za aina tatu tofauti zinaweza kutumika. Dawa hizi ni pamoja naAmoxicillin + Clarithromycin + Metronidazole ambazo hutumika sambamba na dawa yeyote moja kutoka kundi laPPI kama vile Omeprazole au Pantoprazole pamoja na Bismuth Compound.


2. Kwa mgonjwa wa kawaida ambaye si sugu tiba bora inayoshauriwa ni kuchanganya dawa za antibiotic za aina mbili kama Amoxycillin + Metronidazole sambamba na dawa yeyote moja ya jamii ya PPI kama Pantoprazole.


3. Iwapo hakuna ushahidi wa kuwepo kwa uambukizi wa bacteria, dawa yeyote moja ya jamii ya PPI yaweza kutumika kwa muda mrefu zaidi bila kuchanganya na antibiotic yeyote.

Kwa kawaida kitendo cha kutibu na kuwaondoa Helicobacter Pylori humaliza na kuponyesha kabisa vidonda vya tumbo.

Hata hivyo, inawezekana kabisa ugonjwa huu kujirudia tena, hali ambayo hulazimisha kurudiwa tena kwa matibabu kwa kutumia aina nyingine ya antibiotics.

Aidha msomaji, inashauriwa si vyema kwa mgonjwa kujitibu mwenyewe bila kufuata ushauri wa daktari ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo dawa hazitatumiwa inavyopaswa.

Ni kweli Maziwa ya ng’ombe yanaponyesha vidonda vya tumbo?


Kinyume na dhana iliyozoeleka ndani ya jamii, maziwa ya ng'ombe hayaponyeshi vidonda vya tumbo, bali huongeza madhara yatokanayo

na ugonjwa huu. Hii ni kwa sababu, maziwa huwa na tabia ya kutengeneza aina fulani ya kinga au ukuta (protective coat) kwa vimelea vya Helicobacter Pylori ambayo huvikinga vimelea hivi dhidi ya mashambulizi ya dawa na hivyo kufanya dawa kushindwa kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hivi.

Kinachotokea ni kuwa, maziwa huondoa tu kwa muda maumivu ya tumbo kwa kupunguza makali ya tindikali iliyopo tumboni. Pindi maziwa haya yanapoisha, maumivu hurejea tena na kuwa makali kama hapo awali.

Matibabu ya vidonda vya tumbo kwa njia ya upasuaji


Zipo aina nyingi ya upasuaji unaofanywa ili kutibu ugonjwa huu. Kuvuja damu ndani ya mwili kupitia vidonda vya tumbo ni sababu mojawapo ya kufanyiwa upasuaji kwa vile ni hatari sana hata kupelekea kifo iwapo mgonjwa hatapata tiba haraka.


  1. Endoscopy: ni njia inayotumika kutibu uvujaji wa damu unaotokana na vidonda vya tumbo. Aina hii ya tiba hutegemea sana aina na sehemu vilipo vidonda vya tumbo. Tiba hii yaweza kufanyika kwa kuchoma sehemu inayovuja damu ndani ya tumbo au utumbo kwa lengo la kusitisha uvujaji wa damu (cautery) au kwa kuvifunga vidonda kwa kutumia vifaa maalum (clippings). Aidha tiba hii ni nzuri na haina madhara yeyote yale.
  2. Madaktari wengi hupendelea upasuaji ujulikanao kitaalamu kama simple oversewing sambamba na tiba ya kuondoa bakteria. Aidha, mgonjwa pia hushauriwa kuacha matumizi ya dawa za NSAIDs kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa damu kuendelea kutoka kwa vile kama ilivyoonekana hapo awali, matumizi ya dawa hizi huweza kusababisha uvujaji wa ndani kwa ndani ya mwili.
  3. Wagonjwa sugu, hufanyiwa baadhi ya upasuaji ambao huitaji utaalamu wa hali ya juu katika kuondoa neva na mishipa ya fahamu yenye kuhusika na uzalishaji wa tindikali katika tumbo.

Madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo


  1. Uvujaji wa damu ndani ya utumbo: Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja. Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura.
  2. Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo (abdomen) Hali hii huitwa peritonitis na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura. Aidha, kuenea huko kunaweza pia kuathiri tezi kongosho na kusababisha madhara katika tezi hiyo, ugonjwa unaojulikana kama pancreatitis.
  3. Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani kama vile ini au kongosho (pancrease)
  4. Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yasababishwayo na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo (stomach) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo (duodenum) hali ambayo kitaalamu huitwa gastric outlet obstruction.
  5. Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na H. pylori, kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata kansa ya tumbo (stomach cancer). chanzo.http://www.tanzmed.com/component/k2/item/87-ufahamu-ugonjwa-wa-vidonda-vya-tumbo-peptic-ulcer-disease.html
 
Hivi ni kweli hakuna tiba kwa wanaumwa vidonda vya tumbo?

na je dawa zipi ni best?

na huyu DR Rahabu tiba yake ikoje?

wapo waliopona?

gharama zake?

Na kuna mtu anaejua tiba zingine za vidonda vya tumbo?

au maelezo yeyote ya kusaidia?
 
The Boss mama yangu anataabika sana na hivi vidonda katumia dawa ya Rahabu miezi 6 imepita na alifuata masharti mpaka huruma aliumwa malaria akapewa dawa zikatibua na alipimwa akaambiwa vipo bado kapewa dozi tena mi hata nashindwa kuamini hizi tiba mbadala watu wanatumia afya za watu kwa interest zao
 
The Boss mama yangu anataabika sana na hivi vidonda katumia dawa ya Rahabu miezi 6 imepita na alifuata masharti mpaka huruma aliumwa malaria akapewa dawa zikatibua na alipimwa akaambiwa vipo bado kapewa dozi tena mi hata nashindwa kuamini hizi tiba mbadala watu wanatumia afya za watu kwa interest zao

Siyo kweli kuna namna ya kuondoa kabisa tatizo ili mradi tu unazingatia maagizo. Fuatilia maelezo ya hapo chini kuhusu kutibu vidonda vya tumbo.
 
Siyo kweli kuna namna ya kuondoa kabisa tatizo ili mradi tu unazingatia maagizo. Fuatilia maelezo ya hapo chini kuhusu kutibu vidonda vya tumbo.

REISHI
Bidhaa hii inatokana na uyoga mwekundu unaotoka Asia ya mashariki, China, Japan. Uyoga(Ganoderma licidum) unaaminika sana Asia ya mashariki kuwa ni mmea ambao unawapa urefu wa maisha.
FAIDA YA REISHI

  • Kuimarisha mfumo wa kinga mwilini
  • Inapunguza kasi ya kuzeeka
  • Inaimarisha utendaji kazi wa moyo
  • Inaondoa uchovu mwilini
  • Inaimarisha ubongo,kumbukumbu na usikivu
  • Inatibu presha ya kushuka
  • Inatibu vidonda vya tumbo
  • Inatibu pumu, allegy
  • Inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kukupa usingizi mzuri
  • Inapambana na maambukizi ya bacteria na fungus
  • Inasaidia mwili kujikinga na kansa
  • Inatibu matatizo ya candida
CA + FE + ZI PLUS

  • CA – Madini ya Chokaa
  • FE – Madini ya Chuma
  • ZI – Madini ya Zinki
FAIDA ZA MADINI YA CHOKAA

  • 5% ni uzito wa mwili wa binadamu na ni 2% ya uzito wa binadamu ni madini ya chokaa.
  • Madini ya chokaa yanaimarisha mfumo wa kinga mwilini
  • Madini haya yanasaidia utendaji wa kazi mwilini
  • Madini ckokaa yanaimarisha mishipa ya hisia na ubongo
  • Madini chokaa yanasaidia kugandisha damu mtu anapopata majeraha
FAIDA ZA MADINI CHUMA

  • Hutumika kutengeneza damu hasa Red blood cells ambazo husafirisha oxygen
  • Huimarisha mfumo wa mishipa ya hisia mwilini
  • Huongeza uwezo wa kufikiria na nguvu ya ubongo kwa binadamu
  • Huongeza nguvu mwilini
FAIDA ZA MADINI YA ZINKI

  • Inaimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume
  • Inaimarisha milango ya fahamu
  • Kutibu vidonda vya ndani na nje wa binadamu
  • Inatunza ngozi na kulinda ngozi na nywele
  • Inaondoa matatizo ya macho.

GOLDEN HYPHA
Bidhaa hii inatokana na uyoga wa njano na uyoga mweupe wa kawaida.
FAIDA ZA GOLDEN HYPHA

  • Inasaidia kujikinga na saratani(kansa)
  • Kuzuia kuenea kwa saratani(kansa) ya mwili
  • Kujenga upya mfumo wa kinga mwilini na kuuimarisha
  • Inaondoa madhara ya baadaye na matibabu ya kansa
  • Inaondoa uvimbe mwilini
  • Inatibu matatizo ya ini
  • Inaongeza ute ute tumboni, puani,machoni na ukeni
  • Kutibu matatizo ya ngozi
  • Kupambana na bacteria na virusi

Kwa yeyote anayehitaji kuuliza swali au kutaka ushauri anaweza kunipigia kwa namba 0776491294 pia anaweza kuniandikia ujumbe kupitia email ishealthy@hotmail.com
Gharama za REISHI ni Tsh 85000/-, GOLDEN HYPHA ni 72000/- na CA+FE+ZI Plus ni 51000/-
 

Attachments

  • GOLDEN HYPHA.jpg
    GOLDEN HYPHA.jpg
    16.2 KB · Views: 106
vidonda vya tumbo vinatibika na mimi mwenyewe ni shahidi maana nimepona. tatizo ni kwamba watu wengi hawafuati masharti ya dawa au madaktari huwaandikia dozi isiyo na mlolongo mzuri.vidonda hivi asilimia zaidi ya tisini husababishwa na bakteria waitwao helicobacter pylori. ni asilimia chache husababishwa na stress au matumizi ya dawa kama asprin. dalili kubwa ni maumivu kwenye tumbo la juu ambalo mara nyingi hutulia baada ya kula. pia mtu hupata kinyesi cheusi ambacho hutokana na damu iliyo meng'enywa tumboni (ukiona damu kwenye kinyesi ujue ni tatizo lingine). matibabu ya vidonda huusisha dawa tatu na hulenga zaidi kuua hao wadudu. 1.metronidazole (flagyl) 2. clarithromycin 3. omeprazole. badala ya metronidazole mtu anaweza kutumia amoxicillin lakini clarithromycin lazima iwepo.

twende kwenye dozi.
1.unatumia omeprazole 20mg mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 14
2.clarithromycin 500mg mara mbili kwa siku kwa siku 14
3.metronidazole 500mg kwa mara mbili kwa siku 14 au badala yake waweza tumia amoxicillin 1g mara mbili kwa siku kwa siku 14
kumbuka dawa zote hizi unakuwa unazitumia kwa pamoja
pia ili usikosee angalia uzito wa dawa mfano tembe ya metronidazole (flagy) mara nyingi huwa na uzito wa 200mg hivyo utameza viwili na nusu kufika 500mg.
pia amoxicillin huwa na uzito wa 250mg hivyo utameza vinne kufika 1g na kama unameza mara mbili utameza vinne asubuhi na vinne jioni

mimi nilitumia dozi moja ambayo huchanganya dawa zote nne ambazo nilitumia kwa siku kumi
1.omeprazole 20mg mara mbili kwa siku kwa siku ya kwanza hadi ya kumi
2.amoxicillin 1g mara mbili kwa siku kwa siku ya kwanza hadi ya tano
3.metronidazole 500mg mara mbili kwa siku siku ya sita hadi ya kumi
4.clarithromycin 500mg mara mbili kwa siku siku ya sita hadi ya kumi.
hapa wadudu hawawezi kuchomoka.

nafikiri nimeeleweka, sina njia nyingine rahisi ya kurahisisha (sina fedha wala dhahabu ila kile nipatacho ndicho nikupacho, )
 
REISHI
Bidhaa hii inatokana na uyoga mwekundu unaotoka Asia ya mashariki, China, Japan. Uyoga(Ganoderma licidum) unaaminika sana Asia ya mashariki kuwa ni mmea ambao unawapa urefu wa maisha.
FAIDA YA REISHI

  • Kuimarisha mfumo wa kinga mwilini
  • Inapunguza kasi ya kuzeeka
  • Inaimarisha utendaji kazi wa moyo
  • Inaondoa uchovu mwilini
  • Inaimarisha ubongo,kumbukumbu na usikivu
  • Inatibu presha ya kushuka
  • Inatibu vidonda vya tumbo
  • Inatibu pumu, allegy
  • Inasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kukupa usingizi mzuri
  • Inapambana na maambukizi ya bacteria na fungus
  • Inasaidia mwili kujikinga na kansa
  • Inatibu matatizo ya candida
CA + FE + ZI PLUS

  • CA – Madini ya Chokaa
  • FE – Madini ya Chuma
  • ZI – Madini ya Zinki
FAIDA ZA MADINI YA CHOKAA

  • 5% ni uzito wa mwili wa binadamu na ni 2% ya uzito wa binadamu ni madini ya chokaa.
  • Madini ya chokaa yanaimarisha mfumo wa kinga mwilini
  • Madini haya yanasaidia utendaji wa kazi mwilini
  • Madini ckokaa yanaimarisha mishipa ya hisia na ubongo
  • Madini chokaa yanasaidia kugandisha damu mtu anapopata majeraha
FAIDA ZA MADINI CHUMA

  • Hutumika kutengeneza damu hasa Red blood cells ambazo husafirisha oxygen
  • Huimarisha mfumo wa mishipa ya hisia mwilini
  • Huongeza uwezo wa kufikiria na nguvu ya ubongo kwa binadamu
  • Huongeza nguvu mwilini
FAIDA ZA MADINI YA ZINKI

  • Inaimarisha mfumo wa uzazi kwa wanaume
  • Inaimarisha milango ya fahamu
  • Kutibu vidonda vya ndani na nje wa binadamu
  • Inatunza ngozi na kulinda ngozi na nywele
  • Inaondoa matatizo ya macho.

GOLDEN HYPHA
Bidhaa hii inatokana na uyoga wa njano na uyoga mweupe wa kawaida.
FAIDA ZA GOLDEN HYPHA

  • Inasaidia kujikinga na saratani(kansa)
  • Kuzuia kuenea kwa saratani(kansa) ya mwili
  • Kujenga upya mfumo wa kinga mwilini na kuuimarisha
  • Inaondoa madhara ya baadaye na matibabu ya kansa
  • Inaondoa uvimbe mwilini
  • Inatibu matatizo ya ini
  • Inaongeza ute ute tumboni, puani,machoni na ukeni
  • Kutibu matatizo ya ngozi
  • Kupambana na bacteria na virusi

Kwa yeyote anayehitaji kuuliza swali au kutaka ushauri anaweza kunipigia kwa namba 0776491294 pia anaweza kuniandikia ujumbe kupitia email ishealthy@hotmail.com
Gharama za REISHI ni Tsh 85000/-, GOLDEN HYPHA ni 72000/- na CA+FE+ZI Plus ni 51000/-

Rahabu asiwadanganye kwanza sio daktari, ni sawa na yule anayjiita prof. majimarefu lakini hana dawa yoyote ya kuponya vidonda vya tumbo. kwa taarifa nilizonazo hata dawa zake zilipimwa na Wizara ya Afya na kuonekana hazifai lkn kwasababu ya vifua/mgongo wa wanasiasa bado anauza dawa hizo na kuwadanganya watu. kwa mnaobisha mwabieni awapatie vyeti halali za mamlaka zinazohusika na kuruhus matumizi ya dawa nchini

wajinga wasiotafuta habari ndio waliwao, kwani yeye hana tofauti na kikombe cha Babu wa Loliondo, mwisho wake uko wapi, wengi waliokunywa kikombe cha babu, wamekufa vifo vya aibu

msidanganywe na waganga wa kienyeji na wachawi hawana dawa, ni mbwembwe zisizo na manufaa yoyote kabisa
 
Nieleze kwa ninavyojua.

Ni kweli Rahabu sio Dr. wa kusomea yaana MD lakini sheria za afya zinaruhusu waganga wa tiba mbadala kutumia jina la Daktari.

Rahabu huwa anajitangaza kwamba tiba zake zimethibitishwa na kitengo cha tiba mbadala Muhimbili.

Kuhusu matibabu, mimi ni shuhuda, nilitumia dawa yake nikapona. Ni muda kidogo, mwaka 2009. Ila tatizo la Rahabu ni bei. Nililipa tu kwa kuwa nilishasumbuka sana. Kwa wakati huo dozi ilikuwa ni 180,000/- sijui sasa maana jina lake limekuwa hivyo inaweza kuwa juu sana.

Rahabu asiwadanganye kwanza sio daktari, ni sawa na yule anayjiita prof. majimarefu lakini hana dawa yoyote ya kuponya vidonda vya tumbo. kwa taarifa nilizonazo hata dawa zake zilipimwa na Wizara ya Afya na kuonekana hazifai lkn kwasababu ya vifua/mgongo wa wanasiasa bado anauza dawa hizo na kuwadanganya watu. kwa mnaobisha mwabieni awapatie vyeti halali za mamlaka zinazohusika na kuruhus matumizi ya dawa nchini

wajinga wasiotafuta habari ndio waliwao, kwani yeye hana tofauti na kikombe cha Babu wa Loliondo, mwisho wake uko wapi, wengi waliokunywa kikombe cha babu, wamekufa vifo vya aibu

msidanganywe na waganga wa kienyeji na wachawi hawana dawa, ni mbwembwe zisizo na manufaa yoyote kabisa
 
Siyo kweli kuna namna ya kuondoa kabisa tatizo ili mradi tu unazingatia maagizo. Fuatilia maelezo ya hapo chini kuhusu kutibu vidonda vya tumbo.

Yani hadi alipewa likizo ya ugonjwa miezi 3 na masharti hadi nilikuwa namuonea huruma we hata ukibisha upo kibiashara zaidi bora mtu aniambie tiba mbadala ya matunda au mti asilia maana najua mwili utapata faida lakini hizo chemical equation zenu sina mpango nazo
 
Back
Top Bottom