Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Híi ndo tabu ya wajasiriamali wa kibongo,weka bei hapa watu waone.
wataalamu wanadai maziwa hayafai kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo japo imani ya watu ni kuwa yanafaa,ningekua na mda ningeweka link.Mmh nivea mimi hatua yangu ilikuwa ndefu kidogo sijui kama maelezo yangu yatakusaidia ila kifupi kipindi hicho nilishikika kisawasawa hadi nikawa natembea kama ninakibyongo kwa ajili ya maumivu.
Basi baada ya kupata vipimo hospitali na dk kuona jinsi matatizo yalivyoniathidhiri, daktarii aliniandikia dozi kama ya miezi miwili baadhi ya dawa kwa kweli sizikumbuki ila ninazozikumbuka ni kama zantac, amoxiline, flyghl (sinahakika na spelling) na hizi dawa huwezi amini nilizitumia kwa kipindi hicho ingawa kuna baadhi zilikuwa za mwezi mmoja na nyingine nimesahau jina maana ni siku nyingi.
Pamoja na hayo kufuata mashariti ya daktari maana katika hizo dawa kuna ambazo nilikuwa nakunywa kabla ya kula, nyingine katikati ya mlo, nyingine baada ya kula. Vile vile vyakula vyote ambazo nilizuiliwa kula sikugusa hata shule nilikuwa naenda na chupa langu au la maziwa au uji lishe.
Baada ya kumaliza nilijisikia nimepona ila kutokana na mihangaiko vikawa vinanishtuashitua so kuna dada mmoja akaniambia nichukue kiini cha yai la kienyeji nichanganye na asali mbichi ikiwa ni ya nyuki wadogo ni nzuri zaidi nikafanya hivyo kama wiki kweli niliona matokeo mazuri, pia kutumia juisi ya Karoti inasaidia sana, vitunguu swaumu pia waweza kuchangania kwenye saladi na kama u buheri wa afya waweza kunywa mkojo wako ule wa asubuhi glasi moja hata siku tatu mpaka tano kabisa.( zingatia uwe mzima wa afya usiwe na uambukizo wa STD).
Kiukweli hayo yote mie nimeyapitia ni kipindi kirefu sasa maumivu ya vidonda kwangu ni ndoto na nala kila nipendacho na ni mpenzi wa pilipili.
La muhimu ukiwa kwenye matibafu fuata masharti ili kurahisisha kupona vizuri ukisha pona unarudia hali yako ya kawaida vidonda vinasumbua, vinatesa na vinaumiza sana na ni hatari hasa vinapofikia steji mbaya kupona ni shida sana nakumbuka wakati nasumbuliwa nilifikia hatua ya kuvutwa na glass yaani nawashiwa moto (wenyewe wanaita chembe moyo) kisha nafunikwa na glass kisha wana-pull maana tumbo lilikuwa kama limehamia mgongoni nikitembea nimeinama kama bi kizee, maumivi yasipoa, siku zote niko kama mgonjwa wa malaria, nikiumwa njaa nikichlewa kula najiona kama nafa, kila siku kuumwa kichwa, kichefuchefu kisichoisha kweli nilikuwa na taabu, nikienda kwa watu lazima nihakikishe nyumbani nimekula maana siwezi kula chochote hasa nikikuta wamepika maharage au jamii yoyote ya kunde lakini GOD IS GREAT LEO HII NANYATANYATA NIKIWA NJIANI, NAIMBA KWA SAUTI NIWAPO NA FURAHA, NALIA KWA MAJONZI NIWAPO NA MASIKITIKO, HATA KICHEKO CHA UMBEA NATOA NIKIWA NATETA, YOTE MAISHA.
POLE SANA KWA KUUGULIWA. ANAWEZA JARIBU HIZO TIBA MBADALA NILIZOORODHESHA HAPO KWA IMANI ATAPONA. AIKIAMUA KUANZA NA YA YAI AHAKIKISHE MAYAI ANAYASAFISHA KABLA YA KUVUNJA KUEPUKA UAMBUKIZO NA LAZIMA YAWE YA KUKU WA KIENYEJI. BWANA AMPONYE.
Nafikiri wanasema hhayafai kwa ajili ya umengenyaji wake (hasa kwa mtu ambaye tumbo lake linamgogoro) unachukua muda sasa ule muda mrefu wa kumengenywa tumbo linakuwa tayari limetengeneza gesi kitu ambacho kitazidi kusumbua kama unavidonda.wataalamu wanadai maziwa hayafai kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo japo imani ya watu ni kuwa yanafaa,ningekua na mda ningeweka link.
Hamnaga dawa ya kuondoa vidonda vya tumbo zaidi ya kufuata masharti tuu.Hii dawa inasemekana ni ya kiasili na inatibu vidonda vya tumbo kwa mujibu wa matangazo ya kwenye tv.
Ambaye ametumia na kupona naomba a-confirm tafadhali kabla sijamwanzishia mama yangu dozi.
Aksanteni.
Hamnaga dawa ya kuondoa vidonda vya tumbo zaidi ya kufuata masharti tuu.
​nimezitumia hizo dawa vichupa 10 ila baada ya wiki kadhaa vikaanza tena nikaamua nirudi kwenye omeprazole tsh 1000/= dozi alafu zinasaidia sana tuu wakati netragen ni tsh 5000/kichupa
Mkuu.@Fundifundisho Mimi ninakupa Dawa ya Vidonda vya Tumbo fanya hivi kila unapo amka asubuhi kabla ya kula kitu
nenda chooni kakinge mkojo wako kipimo cha glasi moja kisha unywe kila siku kwa muda wa siku 10 kisha nenda kapime
vidonda vya tumbo utakuta vimekwisha pona kabisa. Tumia hiyo dawa kisha uje hapa unipe feedback.
Muhimu unapotumia hiyo Dawa hakikisha huna maradhi ya zinaa mwilini mwako huna maradhi yanyotokana na (UTI)
kwanza kapime mkojo wako kisha ndio uanze hiyo Dawa ninakuhakikishia utapona kabisa. Hakuna Dawa ya kutibu Maradhi ya Vidonda
Vya Tumbo Ma-Hospitalini.
Hamnaga dawa ya kuondoa vidonda vya tumbo zaidi ya kufuata masharti tuu.
​nimezitumia hizo dawa vichupa 10 ila baada ya wiki kadhaa vikaanza tena nikaamua nirudi kwenye omeprazole tsh 1000/= dozi alafu zinasaidia sana tuu wakati netragen ni tsh 5000/kichupa