Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

hii dawa inasemekana ni ya kiasili na inatibu vidonda vya tumbo kwa mujibu wa matangazo ya kwenye tv.
Ambaye ametumia na kupona naomba a-confirm tafadhali kabla sijamwanzishia mama yangu dozi.
Aksanteni.

"haya sema maneno haya wajinga ndio waliwaoo*2" dawa ya kweli ya vidonda vya tumbo ni kula kwa wakati kama tumbo limeshaanza kuuma kula sana mboga za majani na matunda ila epuka matunda yenye acid..punguza futa sana kwenye mboga zako mabo ya nyanya nya inabidi upunguze au uyasahau kwa muda..na haya mashariti ukiyafuata huna haja ya dawa..usisahau maziwa kila unapopata nafasi..mbona utanipa jibu muda si mrefu ukifanya haya na mengine machache basi muda mfupi tu utanambia.. Acha
 
Hii dawa inasemekana ni ya kiasili na inatibu vidonda vya tumbo kwa mujibu wa matangazo ya kwenye tv.
Ambaye ametumia na kupona naomba a-confirm tafadhali kabla sijamwanzishia m
ama yangu dozi.
Aksanteni.[/QUOT

ubavu wangu ulitumia vyupa 90 na sasa amepona kwa maana wale bacteria hawaonekani kwa hospitali alizopita kupima. Pia, maumivu hakuna tena na dalili hazipo. kuna wakati anatumia dawa hali ilikuwa inazidi na kooni kunakuwa na vidonda. hata hvo utatakiwa kufuata masharti wakati wa kutumia dawa. now anakula kila kitu. Sasa sijaelewa kwanini wameifungia.
 
Tanzania hakuna uzalendo kuanzia wamiliki wa vyombo vya habari.wao wanajali fedha tuu bila kujali tangazo lina madhara gani kwa jamii.

Kuna baadhi ya magonjwa yametangazwa na mashirika ya afya kuwa tiba yake haijapatikana lakini unakuta vyombo vya habari vinakubali kupokea promo za matapeli wanaokariri dalili za magojwa kwenye vitabu na kuzitangaza kwa wagonjwa kuwa yanatibu lakini hakuna kitu.

Akina Ndodi na waganga mbalimbali wa kienyeji wameibia sana wagonjwa kupitia kwenye magazeti na sasa wameingia mpaka kwenye Tv tulizoziheshimu.

Hii ni hatari sana ukipita miji yote Tanzania utakuta matapeli wamebadika matangazo yao ya magonjwa sugu , mara wanatoka Sumbawanga, mara Tanga, mara Mombasa mara Malawi. Je mamlaka za miji zinazotyakiwa ziangalie usafi wa mji ziko wapi?

Ndugu yangu ukiunugua uwe makini kwani kuna watu mabingwa wa kuelezea dalili za magonjwa na utaamini kuwa wana uwezo wa kutibu, uongo mtupu watakutapeli fedha zako na tatizo lako linabaki palepale
 
Kupitia jukwaa hili napenda kupiga hodi na moja kwa moja kuhitaji kujua ni lishe ya aina gani kuanzia asubuhi hadi usiku ambayo inamfaa mtu mwenye tatizo la vidonda vya tumbo. Nawasilisha.

hakikisha unakula matango 7 kwa siku, baada ya wiki 4 utaona matokeo
 
Ndugu zangu naomba kuvifahamu vyakula ambavyo mgonjwa au mtu mwenye matatizo ya vidonda vya tumbo hatakiwi kuvitumia katika maisha yake.
 
Mafuta ya Alizeti yabainika kuwa tiba mbadala kwa magonjwa ya Kansa, TB, Presha na Vidonda vya Tumbo.

Na Frank Mbunda, Singida.

Mafuta ya kula yatokanayo na zao la Alizeti linalopatikana kwa wingi mkoani Singida, yamebainika kuwa dawa muhimu na mbadala ya kukabiliana na maradhi ambayo wataalamu wa tiba za kisasa wanayaita ni sugu.
Habari za uhakika

zilizopatikana mjini Singida, zimesema kuwa tayari baadhi ya makampuni makubwa ya ndani yaliyoanza kununua zao hilo kinyemela, yalipata soko kwa baadhi ya nchi za mashariki ya mbali na kujinufaisha bila wadau husika kujua.
Mbali na mkoa wa Singida, zao hilo pia

hulimwa kwa uchache katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Shinyanga, Iringa na Ruvuma, na hii ni kulingana na takwimu zilizopo katika

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Tayari kuliibuka mvutano mjini Dodoma ambako kikao cha Bunge la Bajeti la mwaka jana lilikuwa likinaendelea kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Paseko Konne, aliyekuwa akilalamikiwa na baadhi ya wabunge wa mkoa

huo kuhusu suala hilo.
Konne alidaiwa kutoa zuio kwa wafanyabiashara kuacha tabia ya kuzunguka vijiji kununua zao hilo kwa hatua za ulaghai kwani hatua hiyo inaweza kumkosesha haki ya kujua hali ya soko la siku mkulima.Aidha, alitaka kama utaratibu huo utaonekana kuwa na athari zaidi na kwa nia ya kuongeza ari ya kilimo, wakulima wa zao hilo washauriwe kuuza mazao hayo kwenye vyama vya

ushirika vya msingi kwenye vijiji, kata au Tarafa zao.
Hata hivyo, wakati hayo yakiendelea, mtafiti mmoja wa tiba za asili Mkoani Singida

Dk. Raelk Mhlinyo, amesema amekuwa akitumia mafuta ya alizeti kwa ajili ya kutibia watu magonjwa mbalimbali yanayowakabili.
Lakini pia Dk. Mhlinyo amesema mkoa huo wa Singida, umekuwa ukipokea wageni kutoka mikoa mingine ya kanda ya ziwa, wanaokwenda

kununua mafuta ya alizeti kwa ajili ya kupeleka kwenye maeneo yao kwa ajili ya tiba.
“Mimi nina imani kubwa, hata vita zinazoendelea katika suala hili ni kwa wadau kutambua ndani ya alizeti kuna nini zaidi ya kupata mafuta kwa ajili ya kupikia kwenye chakula,”

amesema Dk. Mhlinyo.
Dk. Mhlinyo ameongeza kusema kuwa alipata utaalam na elimu kuhusu matumizi ya mafuta ya alizeti kama dawa ya kutibu maradhi ya binadamu kutoka kwa mtaalam wa tiba za asili nchini Botswana Dk. Banaye Mwililowe.“Huyu jamaa alikuja Tanzania mwaka ya 1998 kwenye maonyesho na aliona nikihangaika kushawishi watu kununua dawa zangu, ambazo kwa wakati huo

hata sikubahatika kusogelewa kirahisi,” amesema Dk. Mhlinyo.
Alifafanua baada ya kuanza mazungumzo, Mwililowe alimpa moyo na kumtaka kuongeza jitihada zaidi na hasa katika kuwasaidia watu kama huduma badala ya kutaka kupata faida ya haraka.“Kwa hiyo

alinisaidia sana, nami kwa kutaka kujua zaidi nilifanya safari mpaka Zambia, ambako Mwililowe amefungua ofisi eneo la Ndora, na kukutana naye, hivyo tulifanya safari mpaka Botswana ambako nilimsaidia kazi kwa kipindi cha miezi mitano,” amesema.
Amesema

alifanikiwa kubaini mafiuta ya alizeti kuwa ni dawa muhimu kwa maradhi yanayozumbua maisha ya watu wengi na hasa wenye umri mkubwa, hivyo aliondoka huko na kurejresha nchini akiwa amenufaika.
Dk. Mhlinyo amesema mafuta hayo huchanganywa na dawa mbili

za miti shamba kwa ajili ya kutibu magonjwa kama TB, Kansa ya Damu, Vidonda vya Tumbo na Shinikizo la Damu, kwa jamii na kusema hatua hiyo inaendelea kusaidia zaidi watu wenye matatizo.
“Ninatibia watu hapa, na mafuta ya alizeti ni moja kati ya viungo dawa

muhimu kwa kazi hii, ninayapenda sana kwa vile yameendelea kusaidia wagonjwa na kutokana na hali hiyo nimelazimika kulima hekari kadhaa ili kuwa na malengo zaidi,” amesema Dk. Mhlinyo.
Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Tiba Asili katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Paul Mhame, alipoulizwa kuhusu uwezekano wa mafuta hayo yenye virutubisho muhimu vya asili kuweza kutibu magonjwa ya

aina hiyo, alisema ‘hakuna ubishi hilo linawezekana kabisa’.
“Ninachoweza kusema hapa ni kwamba miti shamba ni miti dawa, na kutokana na hali hiyo, mafuta yeyote yatokanayo na mazao ya asili na yasiyo na mchanganyiko wa kemikali, yanaweza kuwa dawa

muhimu za kutibu na wala sio kutuliza maradhi hayo,” alisema Dk. Mhame.
Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alisisitiza dawa hizo pamoja na kuwa ni utafiti wa kijadi na asili zifikishwe kwenye mamlaka husika ziweze kufanyiwa uchunguzi wa kina na kupewa kibali.Baadhi ya

madaktari waliozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu suala la mafuta hayo, wameonyesha kuunga mkono kauli ya Dk. Mhlinyo, wakisema kuna kasi ya kupungua kwa idadi ya watu wanaohitaji matibabu kwa baadhi ya maradhi.
“Inawekana kabisa, matumizi ya mafuta haya kipekee pamoja na huo mchanganyiko wa dawa zake unaweza kusaidia kutibu maradhi mengi na ndio maana idadi ya

wahitaji wa huduma za afya kwa mikoa ya Tabora, Singira na Shinyanga imepungua,” alisema Dk. Jumanne Abdallah wa Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Mtaalam huyo alisema utafiti zaidi unapaswa kufanyika ili kubaini maradhi mengine yanayoweza kutibika kwa kutumia ushauri wa kubadili mfumo wa mafuta na vyakula bila dawa, na kusema jitihada za makusudi zinapaswa kuchukuliwa kwa ajili ya

kusaidia jamii.
Dk. Mhame hata hivyo, aliwashauri viongozi wa serikali ngazi za wilaya na mikoa, kuhamasisha wananchi kilimo cha zao hilo kwa nia ya kuimarisha hali zao kiuchumi, kwa maana ya kujiongezea kipato na kukabiliana na hali duni ya maisha na umasikini.
 
Ndugu zangu naomba kuvifahamu vyakula ambavyo mgonjwa au mtu mwenye matatizo ya vidonda vya tumbo hatakiwi kuvitumia katika maisha yake.

VYAKULA TIBA KWA WAGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO

Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.

Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni. Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:

VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.

POMBE NA KAHAWA
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye ‘caffeine’, vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.

ULAJI CHUMVI

Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.

MAFUTA YA SAMAKI
Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.

VITAMINI NA MADINI
Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.

STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO

Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha
 
kabeji inaruhusiwa kula?
 
kabeji inaruhusiwa kula?
Kabeji ndio inayotakiwa sana uwe unakula inasaidia kwa vidonda vya tumbo. Wewe kama unavyo Vidonda vya Tumbo unataka upone Jaribu Dawa yangu hii ya Kienyeji kwanza

kabisa nenda Hospitali kapime mkojo wako kuwa huna maradhi ya zinaa yaani Maradhi ya (UTI). Kisha ukionekana huna

maradhi ya zinaa kwenye mkojo wako. Fanya hivi kila asubuhi unapo amka kabla ya kula au kunywa kitu nenda chooni

kakinge mkojo wako (Urine) kwenye glasi 1 kisha unywe kwa muda wa siku 7. UKisha kunywa mkojo wako kaa baada

ya saa 1 kupita waweza

kula au kunywa chai. Fanya hivyo ukimalizika huo muda wa siku 7 kunywa huo mkojo wako mwenyewe nenda Hospitali

kapime vidonda vya tumbo utakuta huna tena hivyo vidonda vyako, vimekwisha pona kabisa ukiweza fanya uje unipe

Feedback.
 
Nami ndo tatzo langu kubwa,jaman tuwe serious ni kweli mkojo ni dawa ya vidonda vya tumbo?
Nipo Serious Mkuu Linamo kama ni kweli wewe una Vidonda vya Tumbo na umetumia Dawa za Hospitalini

hukupona Jaribu kutumia dawa yangu hiyo yaani kunywa Mkojo wako mwenyewe Asubuhi. Glasi 1 kabla ya kula au

kunywa kitu kwa muda wa siku 10 kisha nenda Hospitali kapime hivyo Vidonda vyako vya tumbo kisha uje hapa unipe

Feedback Je bado unavyo Vidonda vyako vya Tumbo?

Tahadhari kabla ya kutumia Mkojo wako Mwenyewe.

Kapime Hospitali kuhakikisha kuwa huna Maradhi ya Zinaa wala Maradhi ya (UTI) ndio waweza kunywa huo Mkojo wako

mwenyewe kwa huo muda nilioeleza hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
Kwa ambae amewah kusumbuliwa na hilo tatizo..naomba anielekeze dawa ambayo alitumia ikamsaidia..au maelekezo kwa yeyote anaefaham tiba..
 
Kwa wale wenye matatizo hayo tuwasiliane. Binafsi nimepona. Dawa 20,000 kwa dozi
 
Back
Top Bottom