nxon
JF-Expert Member
- Jul 16, 2011
- 1,162
- 407
sijawahi tumia ila ndo vile vile zoteJe Fiterawa ya Rahab iko vipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sijawahi tumia ila ndo vile vile zoteJe Fiterawa ya Rahab iko vipi?
Ufunguke wewe usiyejuwa kuwa mkojo wako mwenyewe unaweza kukutibu maradhi mengi tu sio tu Vidonda vya tumbo Tembelea hapa ujionee wewe mwenyewe bonyeza hapa Urine Therapy: A cure for all diseasesMKuu hiyo kali. Hebu funguka mkojo unawezaje kumponya mgonjwa?
hii dawa inasemekana ni ya kiasili na inatibu vidonda vya tumbo kwa mujibu wa matangazo ya kwenye tv.
Ambaye ametumia na kupona naomba a-confirm tafadhali kabla sijamwanzishia mama yangu dozi.
Aksanteni.
Hii dawa inasemekana ni ya kiasili na inatibu vidonda vya tumbo kwa mujibu wa matangazo ya kwenye tv.
Ambaye ametumia na kupona naomba a-confirm tafadhali kabla sijamwanzishia m
ama yangu dozi.
Aksanteni.[/QUOT
ubavu wangu ulitumia vyupa 90 na sasa amepona kwa maana wale bacteria hawaonekani kwa hospitali alizopita kupima. Pia, maumivu hakuna tena na dalili hazipo. kuna wakati anatumia dawa hali ilikuwa inazidi na kooni kunakuwa na vidonda. hata hvo utatakiwa kufuata masharti wakati wa kutumia dawa. now anakula kila kitu. Sasa sijaelewa kwanini wameifungia.
Kupitia jukwaa hili napenda kupiga hodi na moja kwa moja kuhitaji kujua ni lishe ya aina gani kuanzia asubuhi hadi usiku ambayo inamfaa mtu mwenye tatizo la vidonda vya tumbo. Nawasilisha.
Hatarihakikisha unakula matango 7 kwa siku, baada ya wiki 4 utaona matokeo
Embu weka hiyo tiba hapa tuwasaidie na wengine mkuu...

Nyama na pilipili
Ndugu zangu naomba kuvifahamu vyakula ambavyo mgonjwa au mtu mwenye matatizo ya vidonda vya tumbo hatakiwi kuvitumia katika maisha yake.
VYAKULA TIBA KWA WAGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO
Ili kupunguza makali au kujiepusha kabisa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, unapaswa kujiepusha na tabia ya kula na kushiba kupita kiasi, kwa sababu kushiba sana huchochea uzalishaji wa asidi nyingi wakati wa usagaji chakula tumboni.
Mbali na hilo, vyakula vyenye mafuta na sukari nyingi na vyenye kiwango kidogo sana cha kamba lishe, imethibitika kuwa husababisha madhara mengi tumboni. Katika makala ya leo, tutaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuviepuka mgonjwa ili kupata nafuu na kuishi bila kusumbuliwa nao:
VYAKULA VYENYE VIUNGO VINGI
Epuka ulaji wa vyakula vilivyopikwa na kuungwa viungo vingi vya aina mbalimbali, kama vile pilipili kali za aina zote na viungo vingine vyenye ladha ya ukali ambavyo hutiwa ndani ya mboga ama chakula ili kuongeza ladha.
POMBE NA KAHAWA
Pombe na kahawa au vinywaji vingine vyenye caffeine, vinaweza kuleta matatizo kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na kwa mtu asiye navyo anaweza kupatwa na tatizo, hivyo ni vyema kuepuka au kutumia kwa kiasi kidogo vinywaji hivi. Kimsingi vinywaji hivi huongeza asidi tumboni na hivyo vinaweza kusababisha vidonda au kuzidisha maumivu kwa anayeumwa.
ULAJI CHUMVI
Utafiti uliowahi kufanywa nchini Marekani umeonesha kuwepo kwa uhusiano kati ya ulaji chumvi na vidonda vya tumbo. Mgonjwa anashauriwa kuepuka ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi, hususan vyakula vya kusindika ambavyo huwekwa chumvi nyingi ili visiharibike haraka. Pia jiepushe na kuongeza chumvi kwenye sahani wakati wa kula.
MAFUTA YA SAMAKI
Baadhi ya utafiti unashauri wagonjwa wa vidonda vya tumbo wale mafuta yatokanayo na samaki (Omega-3 fats) ambayo yameonekana kutoa ahueni kwa wagonjwa. Na kwa mtu ambaye si mgonjwa atakuwa anajiwekea kinga dhidi ya vidonda vya tumbo na magonjwa mengine ya tumbo.
VITAMINI NA MADINI
Ulaji wa vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi husaidia sana kuleta ahueni kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo na kutoa kinga kwa wale ambao hawajaathirika. Wataalamu wa lishe wanashauri kupenda kula matunda na mboga za majani kama vile karoti, juisi ya kabeji, ndizi mbivu, na matunda mengine yenye vitamin C, halikadhalika maziwa ya mbuzi, jibini na cream za maziwa huleta ahueni.
STAILI YA MAISHA NA VIDONDA VYA TUMBO
Licha ya kusabisha Saratani, uvutaji sigara pia huongeza hatari ya mtu kupatwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo, hivyo ni sababu tosha ya kuacha uvutaji sigareti. Japo msongo wa mawazo unaweza kuwa vigumu kuuhusisha moja kwa moja na vidonda vya tumbo, lakini maisha ya wasiwasi, ukichangaya na ulaji mbovu, huweza kusababisha ugonjwa huu, hivyo kama unataka kujiepusha au kupunguza makali ya ugonjwa huu, ni muhimu kuzingatia ulaji sahihi na kuishi maisha ya furaha
Kabeji ndio inayotakiwa sana uwe unakula inasaidia kwa vidonda vya tumbo. Wewe kama unavyo Vidonda vya Tumbo unataka upone Jaribu Dawa yangu hii ya Kienyeji kwanzakabeji inaruhusiwa kula?
Ushahidi kuwa waliotumia Mkojowao wenyewe kujitibu Vidonda Vya Tumbo Hebu bonyeza hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/203168-umetenda-maajabu-siwezi-kueleza.htmlMZIZIMKAVU vp kuhusu mrejesho wa wagonjwa wa vidonda vya tumbo waliowahi kupona kwa kutumia mkojo.!!
Feedback ni chache sana hasa ukizingatia tatizo hili ni la wengi sana.
Vp mkuu kuna dawa ya asili nyingine mbadala inayotibu vidonda vya tumbo.??
Nipo Serious Mkuu Linamo kama ni kweli wewe una Vidonda vya Tumbo na umetumia Dawa za HospitaliniNami ndo tatzo langu kubwa,jaman tuwe serious ni kweli mkojo ni dawa ya vidonda vya tumbo?