Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Mkuu hii dawa ni yakweli? Kuna aliewahi kufanya na akapona? Jee kwa imani yetu (uislam) kunywa mkojo (najis) itakuaje?
Dawa ya Mkojo wako mwenyewe kwa ajili ya kutibu Vidonda vya tumbo inasaidia

ikiwa mkojo wako hauna maradhi ya Zinaa. Kwanza kabisa inatakikana kabla ya kunywa mkojo wako uende Hospitali

ukapime Mkojo wako hauna maradhi ya Zinaa (UTI) ikiwa kama huna maradhi yoyote yale ya zinaa unaweza kunywa

Asubuhi kabla ya kula kitu au kunywa kitu chochote kile. Unakinga mkojo wako kipimo cha glasi moja unakunywa mkojo wako

sio sumu wala hauna madhara kwa binadamu.Kuhusu kama kuna mtu aliyewahi kutumia mkojo wake kutibu vidonda vya

Tumbo yupo kuna Mwanachama humu ndani ya Jamii forums anayeitwa kwa jina hili cc ngoshwe atakuja hapa

kukujibu kuwa mkojo wake mwenyewe ulimsaidia kutibu vidonda vya tumbo alitumia kwa muda wa siku 10 na alipokwenda

kwa Daktari kupima Vidonda vya tumbo vipimo vilionyesha kuwaa amepona hivyo vidonda vyake vya tumbo hebu

bonyeza hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/203168-umetenda-maajabu-siwezi-kueleza.html Kuhusu Suala

la mkojo ni najsi hatuzungumzi humu ndani ya JF. Doctor mambo ya Dini Au Udini mkuu samahani siwezi kukujibu hilo Swali lako.
 
Mwenye kufaham dawa ya vidonda vya tumbo.hasa za asili anijuze!

Rx:
Triple therapy regime itakufaa achana na miti shamba
2 drug combinations za antibiotcs kwa ajili ya kumuua Helicobacter pylori e.g flagiyl na 1 drug kuzuia acid production
Behaviour change e.g acha kula vyakula vyenye acid,3 meals per day,acha kutumia aspirin ambayo uzuia utoaji wa mucus ambayo ulisaidia tumbo lisichomwe na acidi
 
Dah labda lakini siamini

Mh! Mziz hii dozi nitaanza leo ole wako nife coz nasikia mkojo n sumu shaur yako.

Wala sishangai! Nimewahi kusoma (ila sikumbuki ni wapi) kuhusu maajabu ya kunywa matone kadhaa ya mkojo wa asubuhi ili kuimarisha afya. Nimekuwa nikifanya hivyo. Kinga ni bora kuliko tiba, siwezi kusema kama nimepata mafanikio, ila sijaugua, namshukuru Mungu kwa hilo

[h=1]Mkojo na maajabu yake kwa jamii duniani![/h]


Johannesburg, Afrika Kusini. Jiulize, je, umeenda haja ndogo leo asubuhi au la?
Kama jibu ni ndiyo, basi ujue umemwaga kiasi kikubwa cha nishati ambacho pengine kingeweza kuokoa kiasi cha fedha za kulipia bili ya umeme nyumbani kwako. Pia, mkojo una manufaa zaidi kwako ambayo huenda hukuyajua.

Wanayansi na watafiti nchini Uingereza wamevumbua nguvu za mkojo katika kuzalisha nishati ambayo inaweza kuchaji simu kwa muda wa dakika 25 na pia kumwezesha mteja kutuma ujumbe na kuperuzi intaneti.

Watafiti hao kutoka Chuo Kikuu cha Watafiti cha Bristol wakishirikiana na wenzao wa Maabara ya Robot wanasema kuwa nishati hiyo ya mkojo ni mapinduzi ambayo yatasaidia katika upungufu wa nishati wakati wowote badala ya kutegemea jua au upepo.

Timu ya watafiti hao iliweka mkojo katika chombo maalumu ambao baada ya muda ulizalisha bakteria.

Bakteria hao baada ya kuwa na njaa huzalisha nguvu za kielektroni na kuwa nishati. Elektroni hizo hudondoshwa katika kontena maalumu kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Mmoja wa wahandisi aliyevumbua nguvu za mkojo, Dk Ioannis Ieropoulo wa Chuo Kikuu cha West of England (UWE), Bristol anasema, mkojo ni bidhaa ambayo haiwezi kutupungukia tofauti na bidhaa nyingine kama maji, upepo au jua.

Wavumbuzi hao wanasema mkojo ni nishati inayopatikana wakati wowote hivyo hatua hiyo inasaidia kuwa na uhakika wa kutopungukiwa na nishati hata kwa watu wa vijijini.

Anaongeza kuwa madhumuni hya uvumbuzi huo ni kupata nishati inayopatikana wakati wowote, rahisi kuiunda na itakayowasaidia watu wengi wa matabaka mbalimbali.

"Tumevumbua na tumehakikisha kuwa inafanya kazi. Kilichobaki sasa ni kuangalia uwezekano wa mkojo kutumika katika matumizi ya nyumbani," anasema mhandisi huyo.

Mpaka sasa betri iliyoundwa kwa nishati ya mkojo huo ina uwezo wa kuchaji simu itakayoweza kudumu kwa dakika 25, kutuma ujumbe na kupiga simu kwa sekunde 20.
Pia, utafiti uliwahi kufanywa na Profesa Frederick Mwanuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitengo cha Mazingira na kubaini kuwa binadamu anazalisha kilo 50 za kinyesi na lita 400 mkojo kwa mwaka.
Profesa Mwanuzi anaeleza kuwa mkojo na kinyesi vinaweza kutumika kuzalisha nishati kwa mamilioni ya Watanzania.

Profesa huyo anasema walifanya majaribio katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam na katika vyoo mbalimbali na kuzalisha umeme katika baadhi ya nyumba hizo.

Watafiti hao wa Uingereza kwa upande wao wanasema hii ni mara ya kwanza kwa mkojo kuonyesha uwezo wa kutoa nishati ya kuchaji betri na ni mapinduzi makubwa.

Wanasayansi wanaamini kuwa teknolojia hiyo ina manufaa makubwa katika jamii kwani huenda ikatumika katika bafu na vyoo na kuzalisha nguvu ya umeme kwenye mabomba ya bafuni, taa na kuchaji simu.

Hata hivyo mkojo hauna manufaa katika nishati pekee, bali wanasayansi mbalimbali wamewahi kuthibitisha kuwa mkojo unaweza pia kutumika katika tiba.

Mkojo na tiba

Mkojo ni mchanganyiko wa asilimia 95 za maji na asilimia tano za madini yanayotoka baada ya mmeng'enyo wa chakula kufanyika mwilini. Madini hayo ni pamoja na urea, chloride, sodiamu, potassiamu na chuma.

Baada ya kula na mmeng'enyo kufanyika, maji pamoja na mabaki yaliyomeng'enywa husafirishwa katika kibofu cha mkojo.

Maji hayo ndiyo husaidia kufanya usafirishaji wa mabaki hayo hadi katika kibofu cha mkojo.

Nchini India, kwa mfano tiba ya mkojo inaitwa ‘shivambu'. Jina hilo likimaanisha ‘dawa ya hekima' ambayo ilitangazwa zaidi na Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Morarji Desai ambaye alidiriki kuutangazia umma kuwa anakunywa mkojo wake wa asubuhi kila siku na hiyo ndiyo siri ya afya njema na maisha marefu.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa mkojo una utajiri wa protini na madini mengine ambayo huweza kutumika katika matibabu na pia ni miongoni mwa vichanganyo katika dawa nyingi, kwa mfano dawa za ureacini, urecholin na urowave.
Inaelezwa kuwa mkojo wa mwanamke ambaye ndiyo amemaliza mzunguko wake wa hedhi na wajawazito una utajiri wa madini ya gonadotropin ambayo yanaweza kusaidia kuamsha vichocheo na kusaidia katika ugumba.
Hapo zamani mkojo ulitumika viwandani kwa kutengeneza unga wa bunduki.

Anneth Wilbroad, mfamasia katika kituo cha Udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza (IDC) anasema, katika taaluma ya dawa, hakuna somo linalofundisha kuwa mkojo ni dawa kwa sababu ni taka mwili zisizohitajika mwilini.

"Zile ni taka mwili zisizohitajika, zimetolewa mwilini kwa kuwa hazina umuhimu,kitaalamu ni uchafu. Labda mkojo utumike kama tiba mbadala lakini siyo tiba ya hospitali," anasema Wilbroad.

Anasema ingawa mabibi zetu waliamini kuwa mkojo una manufaa katika kutibu vidonda au kuponya sikio, lakini kitaaluma mkojo si dawa.

"Ni kweli kuwa mkojo una madini ya urea na potassiamu, lakini si kwa ajili ya tiba," anasema.

Hata hivyo, Wilbroad anakiri kuwa mkojo unaweza kutumika kama nishati kutokana na madini uliyonayo.

"Kwa jumla, mkojo na kinyesi vyote vinaweza kubadilishwa na kuwa nishati nzuri," anasema.
Source: Mwananchi



 
Kama mkojo ni tiba, kwanini isiwe mkojo wowote anywe mtu yeyote kwani lazima uwe wangu? Yaani mtu kama mkojo wake una maradhi ya zinaa basi anaweza kunywa wa mwenzake maana wakwake haufai
 
kuna siku mtaambiwa na 'kubwa' nayo dawa ya kuongeza 'nguvu' tehe tehe, sipati picha
 
If you like v2 vya asili, use this combination, it realy works coz I used it after long way with all those triple therapy but with reccurency. Mahitaj;Asali iwe asali kweli, either of small bee or da common one, raw egg, fresh milk. Chemsha maziwa kikombe 1 cha chai kisha acha yapoe yawe vugux2, changanya asali vjiko vya chai 2-3, koroga yai kwa kikombe tofaut, kisha changanya kwa ile mix ya maziwa. Hakikisha maziwa hayana joto la kuivisha na kuharibu yai au asali. tumia cku 3-5 mara 2/cku. NB huo mchanganyko unaeza kukera kwa wale wasozoea mayai mabich, tiba hi kwa wale ambao vdonda vyao havija advance sana
 
Mimi ninavyo hadi nilifikia hatua ya kulazwa, lakini hadi sasa sichagui chakula. Liwe kande, pilipili, harage vyote napitia tu. Tatizo la watu wengi wakishaambiwa kuwa wana ugonjwa huo, basi huishi kwa hisia za hofu tu! Hebu jaribu kuishi kama haunavyo uone! na kama unazidiwa sana meza bilauli ya maziwa.
 
usitumie vyakula au vinywaji vyenye asidi. ukitaka dawa ipo just pm nikupe mawasiliano.
 
Pole sana na vidonda!
sasa mimi nilipata vidonda vikali sana mpaka ikafikia naharisha damu tib
yake ya haraka ilikuwa ni hii ila namshukuru mungu nimepona kabisa
sasa...

tumia amoxycilline caps 1g yaani asubuhi tembe 4 za 250gm na jioni tembe
4 za 250gm kwa siku 10 Metronidazole 400mg for bid for 10 days yaani
asubuhi tembe 2 za 200gm na jioni 200gm na Omeprazole 20gm bird for 10
days ukimaliza endelea na omeprazone for 8 weeks asubuhi kimoja jioni
kimoja...utapona and you will find me...all the best pole...

Ndugu nina kama miezi miwili nimetumia ushauri wako huu lakini mambo ni magumu kiuno kinauma,tumbo,na kujaa gesi,haijanisaidia..
 
Pole sana na vidonda! sasa mimi nilipata vidonda vikali sana mpaka ikafikia naharisha damu tib yake ya haraka ilikuwa ni hii ila namshukuru mungu nimepona kabisa sasa...

tumia amoxycilline caps 1g yaani asubuhi tembe 4 za 250gm na jioni tembe 4 za 250gm kwa siku 10 Metronidazole 400mg for bid for 10 days yaani asubuhi tembe 2 za 200gm na jioni 200gm na Omeprazole 20gm bird for 10 days ukimaliza endelea na omeprazone for 8 weeks asubuhi kimoja jioni kimoja...utapona and you will find me...all the best pole...

Dawa ulizotoa ni sahihi ktk kutibu ulcers inayoitwa H pylori associated ulcer .na therapeutic goals ni heal the ulcer and eradicate the organism kwan aina hyo ya ulcer imesababshwa na bacteria wa H.pylori. Na hiyo treatement tunaita triple therapy.lakin dawa huwa hazitolewi kama ivo kwan ni hatar kuliko ajali ya barabara kwan dawa ulizotoa zipo katika prescription ya dr. Yan ni daktar ndo anatoa baada ya kumchunguza mgonjwa wake na kujua ni aina gan ya ulcer inayomsumbua kwan mda mwngne huenda ni stress tu zilizopelekea vdonda vya mda , au labda anapaswa kutumia tu anti acid simple, kwan huenda tatzo lko na yeye ni tafaut.kwa mfano dawa ya omeprazole(ppi) hapasw kutumia mama anaenyonyesha kwan inatabia ya kupita kwnye maziwa ya mama hivo kumuathir mtoto kiafya,pia mtu mwenye matatzo ya ini hapasw,na dawa ya amoxicilin kuna watu wana allerg na iz dawa ,ni daktar au pharmacist ndo anaweza ruhusu kutoa dawa baaada ya mahojiano na mgonjwa.tusitumie madawa kiholela kwan hakuna dawa isiyokua na madhara .either yatajitokeza sasa iv au baada ya miaka( there is no rose without a thorn) ,kwa AFrica ajali ya madawa ni mara mbili ya ajali za barabarani.ivo kabda hujatumia dawa muone pharmacist wako au daktar
 
Hali ya mgonjwa ipoje baada ya ushauri uliopata?

Ndg zangu nikikosa kusema asanteni nitakuwa sina shukulani tena sio mungwana kwani mmetumia muda wenu kunishauli/kutujuza bado tunahitaji msada wenu na ushauli.asanteni kwa ushilikiano wenu msisite kama mumepata habari au tiba kutujuza tupate hiyo elimu
 
Maji hukinga na kutibu vidonda vya tumbo
VIDONDA vya tumbo ni uharibifu wa kuta za ndani ya tumbo. Kwa maneno mengine, ni majeraha ndani ya tumbo.

Vidonda vya tumbo vimegawanyika sehemu mbili; vidonda vya ndani ya tumbo (gastric ulcer) au sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenal ulcer).

Vidonda vinavyotokea katika utumbo ndivyo maarufu sana na huonekana zaidi kutokea kwa wanaume, na vidonda vya ndani ya tumbo huwashambulia wote wanaume na wanawake. Kutokana na tafiti za hivi karibuni, takribani mtu mmoja kati ya watu kumi atakuwa na vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo hutokeaje mwilini?

Chakula kinapoingia tumboni kwa ajili ya kusagwa, tumbo huzalisha majimaji mbalimbali, miongoni mwayo yaliyo muhimu zaidi ni asidi hidrokloriki.

Asidi hii huanza kula kuta za tumbo/doudeni. Aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi.

Utokeaji wa vidonda vya tumbo hutegemea zaidi juu ya vipengele viwili. Kwanza, vitu ambavyo huongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vyakula vya mafuta, uvutaji wa sigara, utumiaji pombe, chai, kahawa na baadhi ya dawa kama corticostisteroids, caffeine, reseprine, n.k.

Pili, udhaifu wa ute au kuta za tumbo/duodeni kuzuia ushambuliaji wa asidi. Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kuongeza kinga ya ute au kupunguza uzalishaji wa asidi.

Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha

Mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vikuu vinavyosababisha vidonda vya tumbo.
Mfadhaiko huongeza utiririkaji wa asidi ndani ya tumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo imetengenezwa kwa ajili ya kukisaga chakula chochote haraka iwezekanavyo.

Lakini kama hakuna chakula cha kufanyiwa kazi, asidi hii humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.
Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi karibuni umeonesha kuwa akili hutumia biokemia katika mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangakia sana katika kutokeza kwa magonjwa mengi.

Utafiti wa kisayansi unasema hisia zetu na hali zetu na jinsi tunavyomudu kudhibiti mifadhaiko inaweza kutusaidia kuelewa ni kwa kiwango gani afya zetu zilivyo madhubuti au zilivyo dhaifu.

Ingawa utafiti katika uwanja huu ni mpya, lakini utendaji kazi wa mfumo wa kinga ya maradhi ya mwili unaweza kukandamizwa na mfadhaiko wa akili/mawazo yatokanayo na shida za maisha.

Majaribio yaliyofanywa kwa watu wenye mifadhaiko sana kama wajane, wenye kupewa talaka na wenye kupambana na adui yalionesha kuwa watu hao huweza kupata maradhi mara kwa mara kutokana mfumo wao wa kinga ya maradhi kugandamizwa.

Mfano katika kukabiliana na adui, akili hutambua hofu na ubongo hupata taarifa; neva zenye kujiendesha zenyewe hupanda juu ili kukutana na adui. Hapo moyo huenda mbio, msukumo wa damu nao hupanda na damu huvimba kwenye misuli kwa ajili ya maandalizi ya tendo.

Oksijeni na virutubishi vingine hukimbilia kwenye ubongo vikimfanya mtu awe hadhiri zaidi, na hapo myunyizo wa adrenalini, homoni yenye nguvu huongezeka.

Kadiri mfadhaiko unavyokuwa mfupi, ndivyo pia athari yake inavyokuwa fupi. Lakini pindi mfadhaiko unapokuwa mrefu, kama vile kipindi cha ndoa isiyo na amani au katika hali ya matatizo, athari yake huendelea.

Dalili za mfadhaiko

Ikiwa bila ya sababu yoyote, zaidi ya dalili sita katika hizi zifuatazo zitatokea, basi mtu amwone daktari kuhusiana na mfadhaiko.
Kujisikia huzuni sana kiwango cha kutokuwa na matumaini yoyote, kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi, kupoteza hamu ya tendo la ngono na kupoteza hamu ya chakula (au kula sana).

Nyingine ni kukosa usingizi (au kulala sana), wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia pamoja, kushindwa falakinika, kushindwa kukumbuka na kushindwa kuamua, kughadhibishwa na vitu vidogo, kujiona huna thamani na kujitenga na marafiki na ndugu.

Kujifunza zaidi kuhusu mfadhaiko/stree bonyeza hapa.

Haraka haraka

Haraka! Haraka! Lazima tufike mahala haraka na turudi haraka! Haraka hizi husababisha vidonda vya tumbo. Mbanano wa ratiba pia husababisha matumbo nayo kubanana.

Malalamishi makubwa leo ya wagonjwa kwa madaktari wao ni: "Tumbo langu linanisokota na kuniletea matatizo, husikia kiungulia baada ya kula". Haraka na wasiwasi ni baadhi ya sababu ya matatizo haya.

Tumbo ni kama kioo cha akili. Akili ikihangaishwa, basi wasiwasi na msukosuko wa hisia hufungia breki kwenye viungo vya ndani. Akili iliyohangaishwa na kukimbizwa mbio mbio hupeleka hisia kwenye tumbo na kusababisha mkazo wa ghafla wa misuli na hapo husababisha kiungulia na maumivu.

Vyakula vya kusisimua

Vyakula vya kusisimua ni hatari kwa neva za tumbo. Uchunguzi wa kitabibu unabainisha kuwa vyakula vya kusisimua kama vile kachapu, haradali, achali, pilipili na vingine vingi huchangia kwa kiwango fulani kudhuru neva za tumbo na havitakiwi kuliwa hasa kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo na mwenye tatizo la kutosagika chakula tumboni. Sababu ni kuwa, visisimuaji huchoma. Tumbo linahitaji kupozwa na si kusasuliwa.

Dalili za vidonda vya tumbo

Vidonda vya tumbo huambatana na maumivu ya kuchoma, kuwaka katika sehemu ya juu ya tumbo. Kwa kuwa aina mbili zote za vidonda vya tumbo hutofautiana, ni vizuri zaidi kuelezea kila kimoja.

(a) Vidonda vya tumboni
Maumivu ya vidonda vya tumboni mara nyingi hukaa katikati, takribani kati ya nusu ya chini na kwenye kitovu na mara nyingi kula huifanya kuwa mbaya zaidi. Tofauti na maumivu ya vidonda vya utumbo, maumivu ya vidonda vya tumbo mara nyingi hayaishi mara moja pindi yanapoanza.

(b) Vidonda katika utumbo
Maumivu ya vidonda vya katika utumbo pia hukaa pale pale (kama katika vidonda vya tumboni). Tofauti na vidonda vya tumboni, katika vidonda vya utumbo mara nyingi kula husaidia kupunguza maumivu.

Tofauti nyingine ni kuwa, wakati katika vidonda vya tumboni maumivu huongezeka haraka baada ya kula chakula, katika vidonda vya utumbo inaweza kuchukua saa mbili au tatu. Tabia nyingine ya vidonda vya utumbo ni kupotea kwa majuma au hata miezi bila sababu ya wazi.

Mtu anaweza kulalamika kuwa anapata maumivu baada ya chakula. Hii ni kutokana na msisimko wa mnyunyizo wa asidi ambao hububujika kwenye kidonda. Katika vidonda vya duodeni, huchukua takribani saa mbili hadi tatu ili asidi ifike sehemu ya kidonda.

Utambuzi wa vidonda vya tumbo

Utambuzi wa kubainisha vidonda vya tumbo hujumuisha X-Ray. Upimaji wa tumbo na vilivyomo ndani yake unaweza pia kufanywa na njia inayojulikana kama ‘endoskopy' au ‘biopsy', ambayo huyakinisha hali halisi.

Matibabu ya vidonda vya tumbo


Matibabu ya vidonda vya tumbo hujumuisha lishe na kubadilisha mitindo ya maisha na kutumia dawa maalumu.

Ikiwa matatizo kama kuvuja damu au vitobo sehemu ya kidonda yatatokea, basi hapo upasuaji huwa muhimu.

Katika vidonda vya tumbo ambavyo ni vikali, matibabu yake hutumia maziwa kwa mwanya wa dakika 15 hadi saa mbili kwa kutegemea ukali wa ugonjwa; kwa wiki moja. Maziwa hutumiwa pamoja na dawa.

Maziwa si kwamba hupambana na asidi tu, bali pia huchelewesha muda wa tumbo kuruhusu dawa kufanya kazi kwa muda mrefu. Vidonda vya tumbo kwa ujumla hupona ndani ya wiki 4-6 za matibabu.

Kuzuia mfadhaiko

Kila mtu ana matatizo na kila mtu hufeli katika mipango yake na kila mtu hupata hasara. Tofauti ni kwamba wakati baadhi ya watu wanaweza kumudu kudhibiti mvurugiko wa mawazo, wengine hawajui kabisa nini cha kufanya na matokeo yake hupatwa na mfadhaiko ambao huweza kuwasabishia maradhi kama vidonda vya tumbo au maradhi ya moyo, n.k.

Mfadhaiko unaweza kuwa wa muda au wa kudumu. Matokeo yake yana madhara makubwa kama hautadhibitiwa. Ni vipi unaweza kudhibiti mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha?

(a) Kuridhika na maisha

Kama tutakubali kuyapokea maisha kama yanavyokuja, tukaacha kuyakopa maisha ya jana na tukaacha kuhofu maisha ya kesho, hakika kabisa matumbo yetu pia yatatulia.

Inaelezwa na wataalamu kwamba karibu asilimia 50 ya wafanyabiashara duniani wanasumbuliwa na maradhi ya kutoridhika, kufunga choo, vidonda vya tumbo na maradhi ya moyo. Na wafanyabiashara ambao hawajui namna ya kupambana na wasiwasi au mashaka hufa wakiwa vijana.

Wasiwasi na hofu ya maisha humfanya yeyote kuwa mgonjwa. Mvurugiko wa hisia una matokeo chanya katika kiwiliwili. Unaweza kuleta ugonjwa ambao ni wa kufisha kama ambao hutokana na lishe dhaifu. Baridi yabisi, maradhi ya moyo, tezi, kisukari, vidonda vya tumbo, kansa, yote yanaweza kusababishwa na mvurugiko wa mawazo.

(b) Kutopata usingizi wa kutosha

Ukosefu wa usingizi ni maradhi makubwa katika zama zetu hizi. Haraka na pilikapilika za dunia yetu ya kisasa hazina mfano. Mvurugiko wa mawazo kutokana na mwenendo wa maisha uko kila mahala. Kutokana na mahitaji ya maisha, kuna idadi kubwa ya watu ambao neva zao hazitulii.

Kulala ni moja ya tiba za mwili. Usingizi husaga chakula na huondoa uvimbe katika tumbo, udhaifu na uchovu.

Kukesha usiku kucha husababisha kutosagika kwa chakula tumboni na hudhoofisha akili na pia husababisha akili kuvurugika. Kulala huleta pumziko kamilifu la mwili na akili.

Madaktari wetu wanasema kuwa, kulala ni muda ambao metaboliki ya mwili hufanyika polepole kiasi kwamba sehemu kubwa ya vyanzo vyake vya nishati hupatikana kwa ajili ya makuzi ya afya njema ya mwili na akili.

Sehemu ya kulala inatakiwa iwe ni tulivu na isiyo na kelele, pia iwe na hewa safi na asilia. Hewa asilia ina athari nzuri katika mwili wa mwanadamu, miongoni mwa athari zake ni kuiwezesha akili kufanya kazi barabara, na pia huongeza hamu ya kula.

Kiwango cha wastani cha kulala kinachotakiwa hutegemeana na umri. Katika umri wa miaka miwili, mtu hushauriwa kulala saa 14 hadi 16 kwa siku. Miaka minne saa 12-14 kwa siku, miaka sita hadi minane saa 11-12 kwa siku, miaka minane hadi 11 saa 10-11 kwa siku, miaka 14 hadi 18 saa 8-9 kwa siku. Watu wazima wanahitaji saa za kulala kati ya sita na nane.

Vidonda vya tumbo katika lugha rahisi

Kunywa maji ml 500 kila nusu saa kabla ya kula chakula cha asubuhi, mchana na jioni, kisha unahesabu masaa 2 baada ya kila mlo na unywe maji tena ml 500.

Unapokaribia kutaka kula chakula chochote, au ukiwaza kutaka kula au ukiuona tu msosi kwa macho, TUMBONI MWAKO HUZARISHWA haidrokloriki asidi ili kuuandaa na kuusaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. HAIDROKLORIKI ASIDI hii ni lazima ipunguzwe makali (must be neutralized) kabla hujameza chakula. INAPUNGUZWAJE MAKALI? kwa kunywa maji nusu saa kabla ya kula chakula. KAMA HAITAPUNGUZWA MAKALI, ASIDI HIYO HUENDA KUTOBOA KUTA ZA TUMBO na hatimaye taratibu baadaye hukusababishia VIDONDA VYA TUMBO.

Jaribu hivyo kwa wiki 2 mfululizo, ni bure tu kisha unipe feedback
 
Back
Top Bottom