Ugumu anaoupitia Harmonize ni kielelezo tosha kwanini sanaa yetu haikui. WCB inaua wasanii nje ya lable yao

mtu yuko nje ya wcb alafu unasema inamuua, kivipi? unataka wao ndo wamsaidia kupost au? sasa hizo chanel kutopost show za harmonze vinaingiliana vp na wcb? au ndo unamtafutia kiki kupitia hiyo wcb?
 
Ye apige kazi tu atakubalika.

Shida inayotokea anataka awe top ghafla huku watu wameshashtukia hawezi kihivyo kama simba.

Kitu nachosema kila siku aache kujilinganisha na simba na kuiga swag zake. Hii itamwangusha. Yani yule simba mi tembo, kila kitu kuiga!


Ye ajenge brand watu wamjue yeye kama yeye.

Hao top wa nigeria ukiangalia kila mmoja ana ka staili tofauti si kuigana igana kila kitu!!!
 
Mkuu umetiririka ataeshindwa kuelewa basi tena
 
Menejment yake inabidi wamwambie asisikilize kabisa nyimbo za mondi na asiangalie kabisa social media za mondi. Ana obsession na mondi na akiendelea kuiga iga hivi hatakuwa na chochote kinachomtambulisha yeye kama brand zaidi ya tofauti ya majina tu. Huku konde music worldwide kule WCB miziki kila kitu kile kile wakati anajua konde worldwide haiwezi kuifikia wcb chiniya mondi!!!
 
kinachomkuza m2 ni his or her perfomance so kukubalika kwa harmonize.... it depends to his perfomance and how he make an interaction to others
Then jarbu kujifunza kuhusu youtube channels... WCB haiwez ku run youtube chennels zote zisipost show ya huyo harmonize...
Note: karudie uchunguz wako then urud hapa useme kitu
 
Ila tukumbuke fan base ya diamond kajenga kwa jitihada kubwa binafsi. Jamaa anatoka kitofauti kila siku watu hawamchoki na ndo maana na fans wanabaki hapo hapo. Hawa wengine wanafurukuta ila wapi kutoka kiupya kila mara inakuwa ngumu.

Nachotaka kusema ni kwamba kukitokea artist mwenye talent kama mondi haitajalisha yuko lebo gani kabaniwa au nini, lazima atatoka tu.
Na brand ya msanii si nyimbo ni pia muonekako, swag zile, nk maana kuna madem wanamfuatilia mondi cause wanampenda tu!!! Jux yule mi sioni anachoimba ila ndo hivo yupo!!!!

Sasa kama kuhujaliwa hivi vitu vingine mbali na sauti utabaki kulaumu tu. Bongo fleva bado ina fan base ndogo kulinganisha na naija au unyamezini. Mtu ana vi-mb vyake kidogo anachagua aangalie kichupa cha nani akiangalia cha mwenzako akiacha chako ujue kuna mengi nyuma ya pazia si kwamba anakuchukia au ngoma yako mbaya!!!
 

binti kiziwi hongera sana sina la kuongeza! Kumbe unatema madini hivi sema huwa una kaa kimya na kutoa like tuu......

Aiseee umenena
 
Bado cjaelewa WCB wanahusika vp hapo.
pia nshawai sikia Harmonize ndiye msanii mkubwa Tanzania anakwamishwa vp na hawa WCB
na vp kuhusu clouds waliompeleka Diamond international wanashindwa kumpiga tafu harmonize..?

Naomba muongozo kwa aliyeelewa
 
Mmeshindwa kujua kinavhomporomosha mnamsingizia Diamond? Muulizeni Diamond mwenyewe alipokubali kuwa Msukule nini kilimtokea, mpaka aliposhituka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aendelee kupambana hapa hakuna atakayemuonea huruma......Diamond babalao yy saaizi ni kati ya wale sugu kawaita wajinga kaenda ccm Aendelee kutunga nyimbo za kumsifu magufuli
 
Kwa maneno mafupi alipokuwa WCB nyimbo zake zilikuwa chache ila ametoka nyimbo zake zinapigwa media zote mpaka Wasafi hivyo wigo wake umetanuka apambane tu
 
Point zako zimeshiba nadhani zimemsaidia hata Komando Jide maana ana mashabiki wake ambao amekuwa nao tangu anaanza muziki pamoja na mashabiki wapya ambao wanapatikana kutokana na uwepo wa wale wengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…