Ugumu kwa NATO kuingiza majeshi moja kwa moja katika mgogoro baina ya Urusi na Ukraine

Kuna swali moja Dogo sana ambalo Mnaulizwa na mara zote mnalikwepa....je ni kwa nini maka sasa NATO haijapeleka majeshi uwanja wa vita kuipiga Urusi?
kwasababu Ukraine siyo mwanachama wa NATO
 
Hujagusia uwezo wa kulitawala anga duniani,,hapa NATO ndo wanajikojolea.
Anga la Ukraine ambayo haina air defense systems imeshindwa kukitawala sembuse anga la NATO ! hizi nchi ni overrated tu. Moskova tuliyoambiwa inalindwa sijui na mitambo gani imezamishwa na kombora la kienyeji kabisa. Urusi zaidi ya nuclear na idadi kubwa ya askari hana cha kuwazidi nchi nyingine.
 
bongo tuna vichaa weng sema hamjijui tu , uvamiwe hlf ubembelez aman huku mwenzio anakudunda tu
Kwa hiyo majambazi wakikuvamia kwako na wanasilaha za moto utaenda kupambana nao kwa panga. Sometimes tumia akili kidogo
 
Kuna swali moja Dogo sana ambalo Mnaulizwa na mara zote mnalikwepa....je ni kwa nini maka sasa NATO haijapeleka majeshi uwanja wa vita kuipiga Urusi?

jibu:
Hakuna maslahi ya kimkakati ya Nato pale Ukraine. NATO hawapigani kiboya. Lengo ni kumuondoa rusia kwenye reli bila wao kupata athar kubwa sana. na kwa 78% wamefanikiwa.
 

Hayo ni mawazo yako au nato ndo wamekutaarifu kuwa ugumu ni huo ulioutaja kupeleka jeshi ukraine?
 
Mhmm jamaa yupo vitani na Dunia?
Naona ushawishi wa US kijeshi utaporomoka.
 
Pia kasema askari wake kati ya 160 - 240 wanauwawa kila siku kwenye mapigano.
Lakini hajaona sababu ya kusimamisha vita
Atasimamishaje hajaambiwa Malaya wake wanaume wake wanaomsaidia. From the very beginning nilisema lawama zote kuiingiza nchi vitani, kusababisha vifo, homeles, refugee ni zelensky, he is very stupid. Wkati wa vita barid tulichagua NAM(NON ALIGNMENT)

Ye alishindeaje kuniweka Kandi na Hawa wanagharibi IL Hali yeye alikuwa Soviet zamani??

Wkati mwingine tunachagua kutogombana na majirani zetu ni Kwa sabb tunatakiwa tuchague kukaa kimya.

Moja ya Siri ya kivita ambayo wengi hawaitambui NATO kila anachompa Ukraine kinashambuliwa, the most paramount target is to destroy every item brought to Ukraine wherever it comes from.

Russian ilitoa chance mapema kwa wananchi kuondoka maana wakati wa kutupia vitu vizito umeshawadia.

West actually kama wangetaka wangejitokeza mapema, Kwa Sasa it's like Russia ameelekeza kila missile upande unaotakiwa, alitumia Muda wake vzr kujiandaa na Hawa waliodhani ataushiwa nguvu.

Russia hajaomba msaada wowote japo majirani knows it's like wanatakiwa wajue wajibu wao. Siri sirini, hatujui wameongea nini.

Alichoonya ni West kuisaidia ukraine.kwa sabb hajavamia, ni operation as USA has done lot of it.

Ukrainian Head of state ameikosea Sana jamii ya mashariki.

Russian haikutaka tu,kumkamata. Ingeshamla kichwa. International law don't allow.

 
Urusi kuivamia ni ngumu kwa sasa kwa kua pumzi bado anayo ila trust me watainyong'onyeza kwa njia za ki intelligence mpk atachuchumaa tu ndipo watampiga akianza kuhema kama kuku aliyetoka kukimbizwa.
 
Kuna swali moja Dogo sana ambalo Mnaulizwa na mara zote mnalikwepa....je ni kwa nini maka sasa NATO haijapeleka majeshi uwanja wa vita kuipiga Urusi?
Kwa sababu Ukraine sio mwanachama wa NATO. Urusi akavamie mwanachama wa NATO halafu wakishindwa kupeleka jeshi ndio uje kuwananga humu.
 
Mkuu ukubwa na sifa ulizozimwaga kwa jeshi la Russia je umewahi kaa na kujiuliza suali hili? na je ulipata jibu gani kwenye kichwa chako? mana nakumbuka JK alisema ukiambiwa na wewe jiambie. mimi nadhan kuna walakini
maana:-

1. Sasa ni inaingia mwezi wa 5 nchi kama ukraine kwa sifa ulizomwaga ilitakiwa hardly operation ichuku japo wiki 2 hadi hadi 3 biashara imemaliza.

2. Nikifuatilia vita vingi sana huko nyuma vilivyopigwana naona mpaka vita vinaisha kwa tabu Majenerali hufa 1 au 2 tu tofauti nilivyoshuhudia kwa Russia sasa ata mwaka bado zaidi ya 25 wameenda na maji., kuna nini hapa?

4. Russia mwenyewe mara kadhaa amekuwa akijipambanua kama ulivyoeleza lakini mbona huwa hamalizii? Alisema atapiga nuclear sweden na Finland wakijiunga NATO lakini amekuwa kimya wakati maombi yamefanyika mchana kweupe

5. Jana naangalia TV European Leadership wapo Ukraine kumalizia mchaka wa Ukraine kujiunga umoja wa ulaya ambapo Russia alisema hilo halitawezekana abadan kwa ukraine kufanya.

6. Putin alisema akigundua mataifa ya magharibi na ulaya wanasaidia silaha Ukraine atashambulia kwenye hayo mataifa lakini naonba mpaka sasa kimya na mizigo inaingia kila leo.

Yako mengi mengi sana ambayo ukiyatathimini yana walakini nguvu aliyonayo Russia kama ulivyopambanua, huenda jeshi na uwezo wa Russia ulisifika kwenye midomo ya watu na makaratasi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…