Ugumu wa Advanced Physics

Ugumu wa Advanced Physics

Kwa mtazamo wangu advanced physics sio ngumu kiviiile ila huonekana ngumu kwa sababu kadhaa
-topics ni nyingi alafu muda wa miaka miwili hautoshi kucover na kumaster vizuri concepts though watu wanapambana sana wanatoka
-kukosekana kwa walimu wanaofundisha vizuri. ..wengi husoma kwa kuunga unga mara mchiki down mara mapambano ili mradi tafrani
-nn kifanyike nitarudi baadae na wengine wataongezea.

Ni kweli kabisa mkuu...ni moja ya masomo yanayotia radha kuyasoma kama resources zinakuwepo. Vitabu, walimu wazuri, maabara etc...If I have to do it all over again, without any hesitation I will do it.
 
mkuu hatujuani humu..ila kuntajia hzo alama 20-45% ni dharau kubwa sana kwangu...ngoja tu nikupe info kidogo.. o-levo nilisoma benjamin mkapa,advance-mzumbe secondary,chuo-udsm CoET-course- civil engineering 3rd year..naomba utafakari mwenyew kwamba nilikuwa napataga ngapi

mkuu.. Usipanic...vitu vya kawaida hivi...
 
kaka tatizo la physics unaisoma, unaelewa na unaenjoy. njoo kwenye pepa, utaikubali mwenyewe.

ni kweli mkuu..ila mara nyingi hakuna mwalimu anayetunga swali jipya kwenye physcs maswali ni yale yale..kufaulu physics kunahitaji kuelewa na kulipenda somo na pia kufanya maswali mengi uwezavyo yenye kila aina ya concept..ukifata hvo vitu vitatu utafaulu tu...
 
Hivi kuna uhusiano mkubwa kati ya O-level physics na A-level physics????

n kidogo sana, tena sana, kati ya masomo ambayo nilikuwa na uhakika wa kupata A o'lvl ni physics lakin a'lvl nakiri sijawahi kupata A. kimsingi anayetaka kusoma physics advance, ajipange.
 
ni kweli mkuu..ila mara nyingi hakuna mwalimu anayetunga swali jipya kwenye physcs maswali ni yale yale..kufaulu physics kunahitaji kuelewa na kulipenda somo na pia kufanya maswali mengi uwezavyo yenye kila aina ya concept..ukifata hvo vitu vitatu utafaulu tu...

ukitaka kuamini hii ni ngumu na itakuja kuwa janga la taifa siku zijazo, shule yetu B+ hazizidi 10 na shule ni ya kwanza kitaifa kwenye hili somo.
 
Mi sikuona ugumu wowote ila ni kwamba lina vitu vingi sana
 
ukitaka kuamini hii ni ngumu na itakuja kuwa janga la taifa siku zijazo, shule yetu B+ hazizidi 10 na shule ni ya kwanza kitaifa kwenye hili somo.

ni kawaida hiyo..kila miaka inavozid kwenda daraja A kwenye physics linazid kupotea..ila pia hii haimanshi kwamba wanafunzi wengi wanapata F..kwangu mim nahisi labda practical ndo huwa linawangusha watu mana unaweza kuta mmeingia mule baadhi ya vifaa havifanyi kazi...ndo mana wengi wanaangukia kwenye B+,
 
nasikia muundo wa mitihani A level mebadilika,ni tofauti na zamani yaani kuanzia mwaka 2000 kurudi nyuma,je ni kweli ? zamani mitihani ilikuwa na calculation nyingi
 
Haitoshi kusoma sana kwa bidii. Inabidi uwe unafahamu mkubwa wa hisabati(sio hesabu), pia uwe na imagination. Ukweli ni kwamba hivyo vitu viwili kuwa navyo ni zawadi kutoka kwa Mwenyezimungu.

hakika hicho ni kipawa, lakini pia kisipopaliliwa kwa juhudi na mazingira mazuri kinaweza kupotea
 
Haitoshi kusoma sana kwa bidii. Inabidi uwe unafahamu mkubwa wa hisabati(sio hesabu), pia uwe na imagination. Ukweli ni kwamba hivyo vitu viwili kuwa navyo ni zawadi kutoka kwa Mwenyezimungu.

hahahaha..dah..
 
mi mbona naiona rahisi tu labda uniambie english labda kidogo. xema ni xomo gumu kwa weng jepes kwa wachache xana. 2metofautiana iq,
 
mi mbona naiona rahisi tu labda uniambie english labda kidogo. xema ni xomo gumu kwa weng jepes kwa wachache xana. 2metofautiana iq,
nilikuwa nafuatilia mjadala kwa ukaribu na nikaona kila mtu anaandika points za maana to the extent nikaona nisitie neno katika mjadala huu...mpaka nilipoona comment yako...hivi ni mtu mwenye akili gani anayeweza kuthubutu kusem kuwa English ni ngumu kuliko fizikia????............Mkuu jaribu kutumia kichwa chako vizuri...kichwa si sehemu ya kufugia nywele ni kwa ajili ya tafakuri tanzu
 
Salamu zenu wapendwa
Kutokana na experience ya hapa na pale, watu wameonekana kulalamikia physics ya A-level kuwa ni ngumu sana. Je! Nini kinachofanya advanced physics kuwa ngumu? Nini kifanyike kwa wadogo zenu waione advanced physics ni somo jepesi?

Waiting for your suggestions

Tutafakari kidogo.
Kwa O-level ukipeleka swali kwa mwalim wa physics, utapata msaada wa kutosha; ila kwa upande wa A-level, utafukuzwa kabla ya kufika mlangoni kwa maneno mazuri kama 'mzembe wewe, utafeli!'. Ni kwa sababu mwalimu wa O-level alifaulu vizuri physics alipokua O-level ndio maana anao uweze wa kutosha wa kumuondolea utata mwanafunzi wake pale penye utata, tofauti na mwalimu physics wa A-level ambae wenyewe tu hakufanya vizuri physics alipokua A-level ( sio wote, wapo wachache waliofaulu vizuri na kupata marks kama zangu). Hapa naweza kusema SABABU NI UWEZO MDOGO WA MWALIMU anayefundisha (kumbuka mwanafunzi aliyefaulu somo la phyisics O-level, ni mwenye kujiweza kimasomo, tofauti na aliyemaliza lasaba). Sababu zingine ni upungufu wa walimu na vitabu pamoja na mapungufu ya maabara zetu. Pia hofu ya wanafunzi wetu juu ya phyisics na kutojituma..
Kipi kifanyike?
Mapungufu niliyoyataja hapo juu, yafanyiwe kazi!
Hitimisho.
Wanafunzi anayetaka kusoma somo fulani, ni bora ukawa na tabia ya kuomba ushauri kwa watu waliofaulu somo husika, watakupa mbinu zaidi ili ufanikiwe; na sio kupendelea kuuliza waliofèli, watakukatisha tamaa na hutafikia malengo yako.
 
nilikuwa nafuatilia mjadala kwa ukaribu na nikaona kila mtu anaandika points za maana to the extent nikaona nisitie neno katika mjadala huu...mpaka nilipoona comment yako...hivi ni mtu mwenye akili gani anayeweza kuthubutu kusem kuwa English ni ngumu kuliko fizikia????............Mkuu jaribu kutumia kichwa chako vizuri...kichwa si sehemu ya kufugia nywele ni kwa ajili ya tafakuri tanzu

naunga mkono hoja English ngumu kuliko physics mkuu amepatia
 
naunga mkono hoja English ngumu kuliko physics mkuu amepatia

Hauwezi kulinganisha english na physics kwa sababu english is just a language (medium of communication), kama wanasayansi wanavyotumia mathematics. Nina maana ndani ya physics kuna ugumu wa physics concepts, kuna ugumu wa mathematics, halafu kuna ugumu wa medium of communication inaweza kuwa english, swahili, chinese or whatever language).
Na huyo anayesema english ngumu kuliko physics, kama hiyo physics anaisoma in english basi hata yenyewe itakuwa ngumu kwake lakini hajui kama ngumu.
 
Mi sikupata F ila mwaka mmoja baadaye niliweza kuelezea black body and zile gates tu.

Sikuwahi kumwelewa mwalimu. Angalau kitabu aisee. Sijui engine, mara air conditioner, mara circuit vilikuwa kama madudu hivi.

Hapa bidii tu ndo ilinitoa. Kwenye kuelewa ni bora mwalimu kuliko kitabu.
 
Back
Top Bottom