Ugumu wa kupambana na ushoga, usagaji, malaya na madada poa uko hapa

Ugumu wa kupambana na ushoga, usagaji, malaya na madada poa uko hapa

Youngblood

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
19,433
Reaction score
56,810
Naongea ukweli na huu ndio ukweli pekee

Vita ya kupambana na ushoga kwa karne hii ya teknolojia na utegemezi wa hali ya juu ni ngumu sana kwa sababu zifuatazo.

1. Mlengo wa serikali zetu-Serikali zetu nyingi zinaendeshwa kidemokrasia, moja ya haki za kidemokrasia ni usawa na haki za binadamu na uhuru wa faragha,hivyo by default ni kwamba tutake tusitake lazima tutafuata haki za binadamu ambazo ni haki ya faragha,ushoga na usagaji-wanaotukopesha wanataka hivyo.



2. Katiba na sheria zetu-katiba nyingi za nchi zetu,hazitambui au hazisemi moja kwa moja kwamba ushoga,umalaya na usagaji ni makosa kisheria.

Sahihishosho: Naona trend ya baadhi ya watu kufunguliwa mashtaka na kufungwa kwa kesi za ushoga na usagaji imeongezeka,heko naona serikali imeamua kufanya kweli.jambo zuri sana

3. Tunapigana kihisia zaidi kuliko uhalisia wa mambo.-Kihisia kwa maana kwamba mara nyingi sababu za kupigana na ushoga,umalaya na usagaji zimekua zile zilezile mfano kulinda maadili ya kiafrika_yapi? ,maadili ya kitanzania__yapi? ,kidini,dhambi, tumesahau kwamba uhalisia wa mambo yamebadilika sana,maadili ya watanzania na watu wote duniani yanabadilika kila siku,kuna watu ambao hawaamini dini,hivyo hawawezi kuacha ushoga na umalaya kwa kigezo kwamba ni dhambi.

Suluhisho.

1. Kupambana kidikteta-nchi au dunia nzima zikiendeshwa kidikteta,kwa maana kwamba kuachana kabisa na demokrasia jambo ambalo ni gumu kwa nchi za kiafrika maaana wafadhili watatukataa mfano, Magufuli,Ruto kwa sasa.

2. Katiba na sheria zionyeshe kabisa kwamba ushoga, usagaji na umalaya ni kosa kisheria___ni ngumu kwenye siasa za kimataifa

3. Kuachana na utegemezi wa kiuchumi,kisiasa,kijamii -mikopo, misaada,ufadhili,vigezo na masharti ni haki za binadamu ambazo ni _ushoga,usagaji,haki za kijinsia pamoja na mambo mengine.

Hii ni sababu kubwa maana hata viongozi wetu hawawezi kutoka hadharani kupinga au kubadilisha katiba maana tunategemea mikopo,ndio mana wamejikita zaidi kwenye sababu namba mbili maadili na dini ambayo kwa maisha ya sasa haiwezi kumaliza hili tatizo.

Karibuni sana kwa maoni na michango.
 
Baadhi ya wenye mamlaka nao hunufaikia humo
Kama masharti ya wafadhili ni ushoga na wanatupa fedha,inamaanisha kwamba tunafaidika kwa kupata fedha kama taifa lakini upande mwingine tunapata hasara kwa kukubali vigezo na masharti ambavyo hatuvitaki ila hatuna jinsi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119]
Kwani uongo,kama tunapewa ARV,misaada..means hata mtanzania wa chini anafaidi,ni ujinga kumeza ARV za bure huku unapinga ushoga[emoji1787]
 
Kweli hatutaki ushoga na ushoga ni dhambi kubwa, lakini cha ajabu tunakula na tunapenda vya "MASHOGA" mikopo karibu yote tunayokopa inatoka kwa hao mashoga na taasisi zao.... huku tukijisifu safari hii wametupa mikopo yenye masharti nafuu, nani Wamarekani na ndo mashoga wenyewe.. wazungu iko akili aisee wana jua kona gani watatukamata... wanatukopesha fedha badala yakutupa mbinu za kuzalisha, wanajua itafika wakati tutaishi kwa misaada, hadi chakula kitatuishia, hatutalima, viwanda vyote vitakufa, tutaishi kwa misaada yao.. ikifika hapo.
 
Russia mashoga na wasagaji ni wengi sana,tena wengi wako marekani,kumbuka marekanj ni taifa ambalo halina mwenyewe ni taifa lenye mchanganyiko wa watu toka mataifa mbalimbali,unaposema wamarekani ni mashoga tambua hilo
 
Huwezi kupambana na hayo mambo , sababu unaingilia Uhuru wa mtu , yaani haiwezekani , haya mambo yapo tangu Enzi na Enzi hata kwenye biblia Yamo , wanaume kuwakiana tamaa , na makahaba walikuwepo akina mariamu walikuwa makahaba , akina Yuda mtoto wa Yakobo alitembea na kahaba anayejiuza , kama ambavyo Mungu hakulazimishi usiwe mwizi au usiwe mzinzi vile vile Mungu hakulazimishi usiwe shoga , cha msingi waleeni watoto wenu kwenye maadili ya dini ndo kitakachowaokoa , na wote tudumu kwenye maadili ya dini hyo ndo sehemu pekee hubadri fikra za mtu
Lakini utumiaji wwte wa nguvu kulazimisha dhamiri ya mtu hauwezi fanikiwa ..... Ni ngumu Sana , huko serikalini wakubwa pia wanahusika na haya mambo , ndo changamoto inakuwa ngumu zaid
 
Back
Top Bottom