Naongea ukweli na huu ndio ukweli pekee
Vita ya kupambana na ushoga kwa karne hii ya teknolojia ni ngumu sana kwa sababu zifuatazo.
1. Mlengo wa serikali zetu-Serikali zetu nyingi zinaendeshwa kidemokrasia, moja ya haki za kidemokrasia ni usawa na haki za binadamu,hivyo by default ni kwamba tutake tusitake lazima tutafuata haki za binadamu ambazo ni haki y faragha,ushoga na usagaji-wanaotukopesha wanataka hivyo.
2. Katiba zetu-katiba nyingi za nchi zetu,hazitambui kwamba ushoga,umayala na usagaji ni makosa kisheria hivyo hata mtu akikamatwa na polisi hakuna mashiko maaana hakuna sheria ya kumhukmu mahakamani...ataachiwa huru.
3. Tunapigana kihisia zaidi kuliko uhalisia wa mambo.-Kihisia kwa maaana kwamba mara nyingi sababu za kupigana na ushoga,umalaya na usagaji zimekua zile zilezile mfano kulinda maadili ya kiafrika_yapi? ,maadili ya kitanzania__yapi? ,kidini,dhambi, tumesahau kwamba uhalisia wa mambo yamebadilika sana,maadili ya watanzania na watu wote duniani yanabadilika kila siku,kuna watu ambao hawaamini dini,hivyo hawawezi kuacha ushoga na umalaya kwa kigezo kwamba ni dhambi.
Suluhisho.
1. Kupambana kidikteta-nchi au dunia nzima zikiendeshwa kidikteta,kwa maana kwamba kuachana kabisa na demokrasia jambo ambalo ni gumu kwa nchi za kiafrika maaana wafadhili watatukataa mfano, Magufuli,Ruto kwa sasa.
2. Katiba zionyeshe kabisa kwamba ushoga, usagaji na umalaya ni kosa kisheria.
3. Kuachana na utegemezi wa kiuchumi -mikopo, misaada,ufadhili,vigezo na masharti ni haki za binadamu ambazo ni _ushoga,usagaji,haki za kijinsia pamoja na mambo mengine.Hii ni sababu kubwa maana hata viongozi wetu hawawezi kutoka hadharani kupinga au kubadilisha katiba maana tunategemea mikopo,ndio mana wamejikita zaidi kwenye sababu namba mbili ambayo kwa maisha ya sasa haiwezi kumaliza tatizo.
Karibuni sana kwa maoni na michango.