Naongea ukweli na huu ndio ukweli pekee
Vita ya kupambana na ushoga kwa karne hii ya teknolojia na utegemezi wa hali ya juu ni ngumu sana kwa sababu zifuatazo.
1. Mlengo wa serikali zetu-Serikali zetu nyingi zinaendeshwa kidemokrasia, moja ya haki za kidemokrasia ni usawa na haki za binadamu na uhuru wa faragha,hivyo by default ni kwamba tutake tusitake lazima tutafuata haki za binadamu ambazo ni haki ya faragha,ushoga na usagaji-wanaotukopesha wanataka hivyo.
2. Katiba na sheria zetu-katiba nyingi za nchi zetu,hazitambui au hazisemi moja kwa moja kwamba ushoga,umalaya na usagaji ni makosa kisheria hivyo hata mtu akikamatwa na polisi hakuna mashiko maana hakuna sheria ya kumhukumu mahakamani...ataachiwa huru.
3. Tunapigana kihisia zaidi kuliko uhalisia wa mambo.-Kihisia kwa maana kwamba mara nyingi sababu za kupigana na ushoga,umalaya na usagaji zimekua zile zilezile mfano kulinda maadili ya kiafrika_yapi? ,maadili ya kitanzania__yapi? ,kidini,dhambi, tumesahau kwamba uhalisia wa mambo yamebadilika sana,maadili ya watanzania na watu wote duniani yanabadilika kila siku,kuna watu ambao hawaamini dini,hivyo hawawezi kuacha ushoga na umalaya kwa kigezo kwamba ni dhambi.
Suluhisho.
1. Kupambana kidikteta-nchi au dunia nzima zikiendeshwa kidikteta,kwa maana kwamba kuachana kabisa na demokrasia jambo ambalo ni gumu kwa nchi za kiafrika maaana wafadhili watatukataa mfano, Magufuli,Ruto kwa sasa.
2. Katiba na sheria zionyeshe kabisa kwamba ushoga, usagaji na umalaya ni kosa kisheria___ni ngumu kwenye siasa za kimataifa
3. Kuachana na utegemezi wa kiuchumi,kisiasa,kijamii -mikopo, misaada,ufadhili,vigezo na masharti ni haki za binadamu ambazo ni _ushoga,usagaji,haki za kijinsia pamoja na mambo mengine.
Hii ni sababu kubwa maana hata viongozi wetu hawawezi kutoka hadharani kupinga au kubadilisha katiba maana tunategemea mikopo,ndio mana wamejikita zaidi kwenye sababu namba mbili maadili na dini ambayo kwa maisha ya sasa haiwezi kumaliza hili tatizo.
Karibuni sana kwa maoni na michango.
Hapo kwenye Demokrasia unakosea sana.
Pakiwa na Demokrasia nzuri na Katiba inayolinda maslahi ya wananchi ni rahisi sana kuwadhibiti Mapepo wachafu wanaowaingia na kuwashawishi watu kuwa mashoga na vitendo Vyote vichafu VYA Kizungu na uzungu wao.
Demokrasia itatufanya tuwapate viongozi wanaotikana na matakwa ya jamii.
Jamii yetu zaidi ya 95% wanapinga vitendo VYA kishoga.
Pakiwa na uchaguzi huru na Wa Haki tutapata viongozi Bora wanaolinda maslahi ya Umma na SIO wabinafsi na Mawakala Wa wazungu kama ilivyo Sasa.
Demokrasia itatufanya tuwakatae mashoga na wasagaji kuwa wabunge na Mawaziri. Sheria zitatungwa zenye maslahi ya Umma. Tutasimamia Rasilimali zetu Vizuri Kwa kuwachagua viongozi Bora . Tutawakataa wale wanafiki katika kupambana na Ushoga.
Leo anaweza akajiunga na CCM na kujitangaza wazi kuwa yeye ni shoga au msagaji na akapata mpaka uteuzi alimradi tu awe na uwezo Wa kuwachamba wapinzani na kuchoma bendera za Vyama vingine.
Kwa Sasa ndani ya vyama hakuna ushindani na kampeni ndani ya Vyama kutokana na udumavu Wa Demokrasia. Vyama vinaogopa mipasuko hivyo vinapitisha watu kimyakimya. Kwa huyo mkiwa na Mwenyekiti mnafiki basi atapitisha watu wake Hata kama wanachama hawamtaki na wengine WOTE wanaufyata. Matokeo yake ni kuwa na wagombea wasio na maadili Wala sifa .
Pakiwa na Demokrasia tutawapata viongozi wanye uchungu na kizazi cha mwafrika SIO Hawa wanaodanganywa na pesa za Wazungu kumaliza kizazi cha mwafrika ambao ni PAMOJA na watoto wao.
Pakiwa na Demokrasia na Katiba nzuri Hata Vyama vya siasa haviwezi kuwa Mali ya MTU kama ilivyo Sasa. Watu wanaona kuwa Fulani akiondoka kwenye chama Fulani chama kitakufa.
Hakuna Haki ya Faragha ya kuoana wanaume Kwa wanaume hadharani au wanawake Kwa wanawake.
Hakuna Haki ya Faragha ya kuwarubuni watoto na kuwafundisha vitendo vya kishoga na kuhamasisha vitendo hivyo. Hakuna anayepata faida yoyote kulingana na matendo hayo machafu na yanayowaangamiza vijana Wa Kiafrika Kwa maradhi. Hata kiafya Bado hakuna uwezo Wa kuwasafisha mashoga Ili waishi Wakiwa na afya njema baada ya kufokolewa ?
Nani ananufaika na Ushoga Wa watu Wezi?
Je ,sisi tutapata faida au hasara Kwa kuweka Sheria Kali ya kuzuia watu wenye nia ovu ya kumaliza kizazi chetu ?Bila shaka tukikaa kimya waafrika tutapata hasara Kabwa sana mana Kwa wazungu Hali ya Ushoga imekuja Kwa Kasi baada ya maendeleo makubwa. Kwetu wanaeneza Ushoga kupitia umaskaini. Hivyo haiendani na Hiyari Bali ni ushawishi unaotokana na umaskini.
Uhalifu unaotokana umaskini ni hatari sana na mara nyingi unaletwa Kwa MALENGO mabaya .
Sasa hatuwezi kukaa kimya na kuwaangalia wazungu walete pesa zao kuhamasisha mambo ambayo kwao yametikana na maendeleo na Mila zao.
Kwa Nini tusiige maendeleo Yao tuige ujinga .
Hata Sasa pangekua na Demokrasia nzuri nadhani viongozi Wa Dini na wanasiasa wangejitokeza hadharani Kupinga Ushoga Kwa nguvu zote mana Hata Majeshi yetu hasa Jeshi la wananchi limekataa kuajiri mashoga waliopenyezwa na wapumbavu Kwa manufaa ya kudhoofisha Jeshi letu.
Sasa iweje Wanasiasa wawe waoga wakati Jeshi limekataa Ajira Kwa mashoga? Bila shaka ni woga unaotokana na Wizi wao . Wanaona pakiwa na Demokrasia ya kweli watakosa kura na watachaguliwa watu waadilifu na wao watakosa sapoti kutoka walikoficha Mali zao na walioungana nao kwenye mikataba Feki ya kuiibia nchi na Rasilimali zetu. Mikopo waliyokopa wakapeleka matumboni mwao wanaona shida kudaiwa Kwa kuwekewa vikwazo.
Kukosekana Kwa Demokrasia kunasababisha wakimbizi Wa kisiasa wanaofadhiliwa na Wazungu Hali inayopelekea kujifunza vitendo vya kishoga na Kuunga mkono Ushoga.
Na Kwa sababu ya Demokrasia changa wanashindwa kukataliwa Kwa wazi na wanachama wao Mana vyama navyo havina Demokrasia ya kweli.
Ukisema Udikteta ni Suluhu . Hii hapana.
Udikteta ungekua Suluhu basi Tanzania Visiwani wasingekua na vitendo hivyo mana ile ni nchi ya Kidikteta halisi na ni nchi iliyojengwa kwenye misingi ya Mapinduzi. Hiví udikteta ni kudhibiti wapinzani tu na SIO Wahalifu na Waovu . Kama udikteta Upo Kwa lengo la kudhibiti wapinzani tu basi Huo ni udikteta Wa kishetani na hauna faida yoyote.
Tofautisha udikteta na uzalendo. Kuna wakati dikteta mwenyewe anakua ni Basha au msagaji, sasa atadhibiti Vipi Ushoga ?
Tanzania ni Nchi ya Kidikteta kulingana na Katiba yetu mana MTU mmoja ndiye anayesoma dictation na wengine wanaandika anachosema .Ukiandika Tofauti unakua umekosea.
Sasa ni Vipi mengine yasemwe na MTU mmoja lakini Ushoga iwe suala la kidemokrasia.
Tuwaache wananchi wapate Katiba Bora na Demokrasia nzuri. Tuwaondoe Wakurugenzi wanaopitisha wabunge wasio na sifa Wala maadili. Vidada vimalaya vimejazana kwenye Vyama vya siasa Ili Hali waadilifu Wakiwa waoga Wa kushughulikiwa na wahuni wanaoteua na kuopitisha mahawara zao. Yote wanajua Sheria na Katiba mbovu zinawalinda .