Habari zenu wakuu,nina ndugu yangu amestaafu kwa hiyari tangu miaka minne iliyopita,Huyu ndugu yangu alipokuwa kazini alikopa kiasi fulani cha pesa toka TPB lakini huu mkopo alifanikiwa kuulipa wote kipindi yupo kazini,lakini tatizo likajitokeza kipindi mafao yalipotoka kwani kile kiasi cha pesa alichokopa kilikatwa tena,muhusika alijaribu kufuatilia lakini ikawa wanamzungusha tu mpaka leo hela haijarudi.
Cha kushangaza zaidi katika mshahara wake wa mwisho wa mwezi bado benki ya posta wanaendelea kumkata na hili muhusika alikuwa halijui mpaka PSSF walipomueleza kwamba Kiasi anachopokea siyo sahihi kwani kingine kinaenda TPB,Kumekuwa na ugumu wa kupata haki ya mstaafu toka benki hii ingawa PSSF walishawatumia barua kwamba anakatwa kimakosa
Naomba ushauri wenu katika hili maana mtu mmoja ameshalipishwa mara mbili na hii anayokatwa ni ya tatu.