Ugumu wa kupata kibarua hapa Bwawa la Umeme la Nyerere

Ugumu wa kupata kibarua hapa Bwawa la Umeme la Nyerere

kasagamba

Member
Joined
May 27, 2020
Posts
46
Reaction score
51
Wakuu habari za wikend!

Wakuu baada ya Mh, Raisi Magufuli kuruhusu shughuli na miradi ziendelee , Nime Jaribu kutafuta riziki kwenye miradi ya ujenzi inayo endelea hapa Dar bila mafanikio, huku familia ikizidi kuumia njaa, Nikaona ni bora nijaribu kuja huku kwenye ujenzi wa bwawa la Umeme la Nyerere, Maarufu kama Stiegler's Gorge. Wakuu nimesha kabidhi Kwa Hr, CV na barua ya maombi ya kazi ya Fundi nondo (Steel fixer)

Kutokana na njaa ndani ya familia yangu Pia nimeomba kazi za kibarua( labour) kama nafasi ya kazi ya fani yangu ikichelewa kutoka. Kwa sasa barua zinazopewa kipaumbele ni za wazawa wa kijiji hiki na wale walio omba toka miezi ya nyuma. Wakuu Kwa utaratibu huu njaa itaiua familia yangu

Jamani wana JF wenzangu naombeni Kwa yeyote mwenye uwezo wa kunisaidia nikapata kazi hapa mapema anisaidie maana familia yangu itakufa njaa .Sina pakukimbilia zaidi ya kuja kwenu wana JF

Asanteni.

0765544791
 
Pole sana kiongozi ....mungu atakusaidia tu muda c mlefu...
 
Mkuu nashukuru sana Naamini Mungu ndio mtoa riziki atanifanyia njia
Pole. Maisha hayana huruma. Ni kujitahidi tu kwani kila mtu hupitia vipindi kama hivi. Ila... pamoja na kuwa una shida, kuweka namba yako ya simu hadharani namna hii ni risk kubwa. Kuna watu wakifanikiwa kujua namba ya simu ya mtu, basi ni windo zuri.

Na zaidi... wakijua namba ya simu na shida inayomkabili mtu na wasifu wake, hiyo ni zaidi ya ''windo nono'' la kukamata kwa ulaini. Najua unaweza kujiamini na kusema utakuwa makini, lakini usijiamini kwa 100%! Good luck!
 
Mkuu kuna dogo langu alisanda uko kwanza mbali afu afu hakuwa na connection yoyote...alirudi tu kijijini Ila ukpata kazi uko naskia mshahara wake mnono.
mkuu connection Ndilo tatizo Kwa hapa hasa kwetu wageni wa kijiji hiki.
 
..upo kisaki au kijiji gani mkuu? na umeomba kazi katika kampuni IPI tuanzie hapo.
 
Mkuu kuna dogo langu alisanda uko kwanza mbali afu afu hakuwa na connection yoyote...alirudi tu kijijini Ila ukpata kazi uko naskia mshahara wake mnono.

50% wako na 50% unauacha kwa ' aliyekuunganishia ' huo ' Mchongo ' huko. This is Tanzania!
 
mkuu njoo inbox tuyajenge,huenda ushauri wangu ukawa msaada kwako.
Mkuu samahani Nimechelewa kukujibu ila nikutokana na kemeo cha simu nilichonacho hakikai na charge.Mkuu mimi bado nipo hapa kijijini kisaki nasubiri ila matumaini Ni madogo tumejaribu hata kujitolea hapa kijijini kwenye mradi wa ujenzi was zahanati ya kijiji angalau tuonekane lakini wapi, Mkuu nimekupm tayari
 
Njoo inbox sijapokea meseji yako yoyote
 
Back
Top Bottom