Ugumu wa kuwakamata Matapeli wa mitandaoni na wale wa Kuuza Bata fake

Ugumu wa kuwakamata Matapeli wa mitandaoni na wale wa Kuuza Bata fake

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Wale Jamaaa wa tuma kwa number hii na pia wale wanao uza Bata Bukini fake kwenye Magroup ya Face book kuna ugumu sana wa kuwakamata.

Mwanzo sikujua kwa nini Police hawawakamati, na pia mbona wana watapeli hadi Wajeda na hao hao Police?

Nina Rafiki zangu Wajeda wamelizwa na pia Police wamelizwa sana na hawa wanao uza Bata.

Hawa matapeli hata ukisha watumia pesa hawawezi zima ile laini na ukipiga wanapokea kabisa simu ila ndo hivyo wanakuwa wameisha kuliza.

Juzi kati kuna askari rafiki yangu alilizwa na hawa wa Bata na hapo sasa ndo nikaja kujua kwamba kuna ugumu kuwakamata.

Ugumu uko wapi?

Hawa Jamaa wamesajili laini my be kwa majina fake, hili linawezekana make wasajili laini wenyewe ndo wale njaa nyingi sana.

Laini wanazo tumia kufanyia utapeli kamwe hawazitumiii kuwasiliana na iwe ndugu zao, Marafiki zao, au Jamaa wengine wa karibu.

Zile Laini za utapeli zina simu zao maalumu, na ile simu yaa maalumu hawawezi kamwe kuweka laini tofauti na ile fake laini.

Zile laini ni za Utapeli tu, na watu wote wanao wapigia simu ni either wametapeliwa tiyari au ndo wako kwenye process ya kutuma pesa wakijua wataletewa nzigo.

Sasa wakikutapeli, ukiwapigia simu wanapokea na wanaongea ila kamwe na Daima huwezi waambia njoo tuoanane waje, na pi wanajua fika zile number hakuna ndugu, wala jamaa wala nani wanao zijui so kamwe huwezi wadanganya kwamba njoo tuoanane waje na Ukitrack zile laini sana sana wanao wapigia ni walio tapeliwa au walitaka kutuma pesa na kadhalika.

Hili ndio lilifanya Police washindwe kuwakamata make, njia rahisi ni kutrack number zinazo wasiliana na number fake lakini kwa hili wanashindwa kwa sababu wote ni watapeliwa.

Pili ni kuangalia IMEI ya simu kama ilisha wekwa laini nyingine, sasa Jamaa simu yao kamwe hawaweki laini halisi yenye majina halisi.

Njia ya Minara ya simu pia haifanyia kazi make inaweza sema wako May be Mbezi sasa mbezi ni kubwa sana, na Minara haina uwezo sa kutrack location na distance kutoka kwenye minara kama ilivyo GPS
 
Juzi kati walimpigia kaka yangu simu kuwa mwanaye wa darasa la 5 amevunjika mkono shuleni yupo hospitali moja hivi, na wakamtajia jina la mtoto kabisa. kaka akawaambia ngoja niongee na mama yake wakamwambia tuma pesa, yaani wanachofanya hawakupi mda wa kufikiri.

nachojiuliza mpaka saivi ni kuwa walijuaje jina la mtoto?
 
Ramani huwa inatoka kwenye ma group ya wazazi wa wanafunzi wa shule husika
 
Tatizo liko apo kwenye utaratibu wakusajili lain

Uliletwa utartibu wakutumia fingerprint na kitambulisho cha taifa lakini bado lain zinasajiliwa kama njugu

Tunalegeza sana sheria kukimbia uhalisia (tunaishi sana kisiasa)
Mfano sasa ivi ukiwekwa utaratibu wakurasimisha namba 1 ambayo itakuwa yakutumika baada tuu yakusajiliwa kwa kitambulisho cha taifa

Mimi binafsi nitapoteza namba 3 maana ninazo nne licha mbili sinampango nazo tena

Watu nilio wasajilia sasa ndiyo kijiji siyo chini ya kumi

Hivyo likipigwa panga apa ni kelele
 
Sasa kinqchotokea ni wanao ajiriwa sio professional wa hio kada Sasa unapata namba ya simu unatafuta imei Sasa unashindwaje kutumia hio Imei kupata location halisi hii nakumbuka zile simu zilizumwaga tulizinunua kwa bei ya kawaha na kuzi repear hizo Imel na kuzitumia Tena
 
Mkuu ila kumbuka na mashinevya NIDA Arusha wanayo mtaani waliibada
 
Hizi sio “Bata” za “Duck” hizi. Itakua huduma pendwa.
 
Sasa kinqchotokea ni wanao ajiriwa sio professional wa hio kada Sasa unapata namba ya simu unatafuta imei Sasa unashindwaje kutumia hio Imei kupata location halisi hii nakumbuka zile simu zilizumwaga tulizinunua kwa bei ya kawaha na kuzi repear hizo Imel na kuzitumia Tena
Mkuu minara inasoma jina la mnara pekee, mfano Mnara wa Boko, ila huwezi jua ni Boko wapi hasa na huwa ina badilika kuna wakati inaweza soma mnara wa mtaa wa pili,
 
Bata ni nini? Zinauzwaje kwenye magroup?
Unaishi Nje ya Dunia? Kuna Matapeli hupost picha za hawa ndege wa mapamba hasa Bata bukini, hii ndo utapeli mkubwa umehamia ingawa kwa sasa watu walisha pigwa sana na wameshituka
 
Juzi kati walimpigia kaka yangu simu kuwa mwanaye wa darasa la 5 amevunjika mkono shuleni yupo hospitali moja hivi, na wakamtajia jina la mtoto kabisa. kaka akawaambia ngoja niongee na mama yake wakamwambia tuma pesa, yaani wanachofanya hawakupi mda wa kufikiri.

nachojiuliza mpaka saivi ni kuwa walijuaje jina la mtoto?
Hawafanyi mambo kwa kukurupuka, huwa wanajipanga kwa muda wa siku kadhaa kabla ya kupiga tukio.
 
Mnanunua Bata kwenye simu?
Kwani kule Instagram bidhaa wanauzaje mkuu? Facebook si kuna watu wanafanya Biashara online? Hapo ndo upigaji unapo anzia, Ni biashara za kwenye nitandao
 
Back
Top Bottom