Ugumu wa kuwakamata Matapeli wa mitandaoni na wale wa Kuuza Bata fake

Ugumu wa kuwakamata Matapeli wa mitandaoni na wale wa Kuuza Bata fake

Hawafanyi mambo kwa kukurupuka, huwa wanajipanga kwa muda wa siku kadhaa kabla ya kupiga tukio.
Na hio number hata u track vipi hutawakamata make, kwanza ni ya matukio pekee hawaitumii kwa normal communication
 
Mimi naona inawezekana kwa kutrace namba husika kujua mtumiaji anapatikana wapi.
 
Namba za matukio ni ngumu kuzitrak. Na hata ukimkamata mahakamani atachomoka kwa ukosefu wa ushahidi
 
"VIP hali yako Mimi mwenye nyumba wako tafadhali naomba tuwasiliane katika tigo hii 0716795102 sababu nashida na wewe "

Hiyo ni mojawapo ya mesej walionitumia juzi kati. Sema machale kundesa, nkashtuka maana mzee mwenye nyumba ananidai, faken nkaamua kupiga kimya. Baadae nkaangalia muandiko haufanani na biti zake. Kaeni chonjo
 
Mwingine alipigia simu akasema yeye ni huduma kwa wateja nikarudi kuangalia namba naona za kawaida. Nikashtuka
 
Mimi naona inawezekana kwa kutrace namba husika kujua mtumiaji anapatikana wapi.
Inasoma mnara, sasa unless kila nyumba iwe na Mnara wake, hivi Mtaani kwenu Mnara mnao tumia unaweza track nyumba? Mnara unaweza kukuambia huyu jamaa yuko My be Mkata, lakini Je hio Mkata kuna mtu mmoja na nyumba moja?
 
Inasoma mnara, sasa unless kila nyumba iwe na Mnara wake, hivi Mtaani kwenu Mnara mnao tumia unaweza track nyumba? Mnara unaweza kukuambia huyu jamaa yuko My be Mkata, lakini Je hio Mkata kuna mtu mmoja na nyumba moja?
Ulimwengu umebadilika yapo ma software yanayoweza kufanya iyo kazi vizuri tu.

Jaribu ku google utaona, nilishawahi kutumia software moja siikumbuki jina ilikuwa inalipiwa so nikatumia trial ya 24hrs ilikuwa na uwezo wa kuonesha kwenye map namba fulani iko wapi.

Kwa maendeleo makubwa ya technology yaliyopi Ulimwenguni kwa sasa tukiamua tunawapata mapema tu
 
Wale Jamaaa wa tuma kwa number hii na pia wale wanao uza Bata Bukini fake kwenye Magroup ya Face book kuna ugumu sana wa kuwakamata.

Mwanzo sikujua kwa nini Police hawawakamati, na pia mbona wana watapeli hadi Wajeda na hao hao Police?

Nina Rafiki zangu Wajeda wamelizwa na pia Police wamelizwa sana na hawa wanao uza Bata.

Hawa matapeli hata ukisha watumia pesa hawawezi zima ile laini na ukipiga wanapokea kabisa simu ila ndo hivyo wanakuwa wameisha kuliza.

Juzi kati kuna askari rafiki yangu alilizwa na hawa wa Bata na hapo sasa ndo nikaja kujua kwamba kuna ugumu kuwakamata.

Ugumu uko wapi?

Hawa Jamaa wamesajili laini my be kwa majina fake, hili linawezekana make wasajili laini wenyewe ndo wale njaa nyingi sana.

Laini wanazo tumia kufanyia utapeli kamwe hawazitumiii kuwasiliana na iwe ndugu zao, Marafiki zao, au Jamaa wengine wa karibu.

Zile Laini za utapeli zina simu zao maalumu, na ile simu yaa maalumu hawawezi kamwe kuweka laini tofauti na ile fake laini.

Zile laini ni za Utapeli tu, na watu wote wanao wapigia simu ni either wametapeliwa tiyari au ndo wako kwenye process ya kutuma pesa wakijua wataletewa nzigo.

Sasa wakikutapeli, ukiwapigia simu wanapokea na wanaongea ila kamwe na Daima huwezi waambia njoo tuoanane waje, na pi wanajua fika zile number hakuna ndugu, wala jamaa wala nani wanao zijui so kamwe huwezi wadanganya kwamba njoo tuoanane waje na Ukitrack zile laini sana sana wanao wapigia ni walio tapeliwa au walitaka kutuma pesa na kadhalika.

Hili ndio lilifanya Police washindwe kuwakamata make, njia rahisi ni kutrack number zinazo wasiliana na number fake lakini kwa hili wanashindwa kwa sababu wote ni watapeliwa.

Pili ni kuangalia IMEI ya simu kama ilisha wekwa laini nyingine, sasa Jamaa simu yao kamwe hawaweki laini halisi yenye majina halisi.

Njia ya Minara ya simu pia haifanyia kazi make inaweza sema wako May be Mbezi sasa mbezi ni kubwa sana, na Minara haina uwezo sa kutrack location na distance kutoka kwenye minara kama ilivyo GPS
Mbona kazi ndogo tu,ni kuripoti namba zote na kuzifunga
 
Hizi sio “Bata” za “Duck” hizi. Itakua huduma pendwa.
Liko moja nalilia timing linajiita husna limeshakula 2000 ya voucher ila nimestukia ni dume .iko siku yake nitalitatua marinda tu
 
Back
Top Bottom