Ugumu wa kuwakamata Matapeli wa mitandaoni na wale wa Kuuza Bata fake

Hawafanyi mambo kwa kukurupuka, huwa wanajipanga kwa muda wa siku kadhaa kabla ya kupiga tukio.
Na hio number hata u track vipi hutawakamata make, kwanza ni ya matukio pekee hawaitumii kwa normal communication
 
Mimi naona inawezekana kwa kutrace namba husika kujua mtumiaji anapatikana wapi.
 
Namba za matukio ni ngumu kuzitrak. Na hata ukimkamata mahakamani atachomoka kwa ukosefu wa ushahidi
 
"VIP hali yako Mimi mwenye nyumba wako tafadhali naomba tuwasiliane katika tigo hii 0716795102 sababu nashida na wewe "

Hiyo ni mojawapo ya mesej walionitumia juzi kati. Sema machale kundesa, nkashtuka maana mzee mwenye nyumba ananidai, faken nkaamua kupiga kimya. Baadae nkaangalia muandiko haufanani na biti zake. Kaeni chonjo
 
Namba za matukio ni ngumu kuzitrak. Na hata ukimkamata mahakamani atachomoka kwa ukosefu wa ushahidi
Unamaanisha nini unaposema kukosekana kwa ushahidi wakati Sms za money transactions zipo ?
 
Mwingine alipigia simu akasema yeye ni huduma kwa wateja nikarudi kuangalia namba naona za kawaida. Nikashtuka
 
Mimi naona inawezekana kwa kutrace namba husika kujua mtumiaji anapatikana wapi.
Inasoma mnara, sasa unless kila nyumba iwe na Mnara wake, hivi Mtaani kwenu Mnara mnao tumia unaweza track nyumba? Mnara unaweza kukuambia huyu jamaa yuko My be Mkata, lakini Je hio Mkata kuna mtu mmoja na nyumba moja?
 
Ulimwengu umebadilika yapo ma software yanayoweza kufanya iyo kazi vizuri tu.

Jaribu ku google utaona, nilishawahi kutumia software moja siikumbuki jina ilikuwa inalipiwa so nikatumia trial ya 24hrs ilikuwa na uwezo wa kuonesha kwenye map namba fulani iko wapi.

Kwa maendeleo makubwa ya technology yaliyopi Ulimwenguni kwa sasa tukiamua tunawapata mapema tu
 
Mbona kazi ndogo tu,ni kuripoti namba zote na kuzifunga
 
Hizi sio “Bata” za “Duck” hizi. Itakua huduma pendwa.
Liko moja nalilia timing linajiita husna limeshakula 2000 ya voucher ila nimestukia ni dume .iko siku yake nitalitatua marinda tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…