Ugumu wa maisha; Mama anywesha wanae 5 sumu. Wawili wafariki dunia, watatu pamoja naye wanapatiwa matibabu

Ugumu wa maisha; Mama anywesha wanae 5 sumu. Wawili wafariki dunia, watatu pamoja naye wanapatiwa matibabu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.

Hata hivyo mama huyo amenusurika kifo licha ya kunywa sumu hiyo kwa madhumuni ya kujiua

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 2, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe inasema mama huyo mwenye watoto watano aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao kufariki.

Watoto hao wanumri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na miaka 12.

Watoto waliofariki dunia kutokana na sumu hiyo ni mwenye umri wa miaka 12 na miaka miwili.

“Watoto wengine wamelazwa Kituo cha Afya, Bwanga pamoja na mama yao akiwa chini ya ulinzi wa Polisi,”amesema Mwaibambe

Mwananchi
 
Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.

Hata hivyo mama huyo amenusurika kifo licha ya kunywa sumu hiyo kwa madhumuni ya kujiua

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe inasema mama huyo mwenye watoto watano aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao kufariki.

Watoto hao wanumri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na miaka 12.

Watoto waliofariki dunia kutokana na sumu hiyo ni mwenye umri wa miaka 12 na miaka miwili.

“Watoto wengine wamelazwa Kituo cha Afya, Bwanga pamoja na mama yao akiwa chini ya ulinzi wa Polisi,”amesema Mwaibambe

Mwananchi
 
Maisha ni kufundishana na kukumbushana
Kweli hata balozi wa nyumba 10 hana habari na watu wake

Ok labda sio majukumu yake vipi majirani yaani tumefikia ubaya huu hata hujui Jirani yako ana maisha yapi

Nashauri sio serikali tu hata waumini kwenye Nyumba za ibada wangekuwa wanatoa darasa la maisha kwa ujumla

Sio mara ya kwanza mambo haya yanatokea bali utakuta mtu anamuuwa mwenzie kwa deni la buku

Kama una shida bora kuisema tu
 
Kwa vile sehemu za Dini zimekuwa siyo kimbilio tena kwa watu walioshikwa na matatizo basi naomba serikali ianzishe kitengo cha kutatua shida zilizozidi kwa kuwapa mafunzo na mtaji na wawe wanajulikana ofisi zao pia wawe na vipindi kwenye TV kuonyesha Kila mwezi ni jamii ngapi zimesaidiwa kama anavyofanya frola wa Mwanza.
 
Inasikitisha. Taji liundi akisoma hii itamkumbusha ndugu zake walivyofariki dunia baada ya mama yao kuwapa sumu.
Yaani si angewapeleka hata wilayani ili serikali iwalee.
 
Ugumu wa maisha sio sababu ya mtu kujiua.

Ingekuwa ni hivyo basi Tanzania nzima Ingekuwa imejaa makaburi ya watu waliojiua kwa ugumu wa maisha.

Tujifunze kushukuru hata uhai tulionao.
Uhai na watoto wanakuangalia huna hata uji wa kuwapa unafikiri ni rahisi??
 
Inasikitisha. Taji liundi akisoma hii itamkumbusha ndugu zake walivyofariki dunia baada ya mama yao kuwapa sumu.
Yaani si angewapeleka hata wilayani ili serikali iwalee.

Serikali unayoilenga hapa imelea wangapi?
 
Back
Top Bottom