Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.
Hata hivyo mama huyo amenusurika kifo licha ya kunywa sumu hiyo kwa madhumuni ya kujiua
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Desemba 2, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe inasema mama huyo mwenye watoto watano aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao kufariki.
Watoto hao wanumri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na miaka 12.
Watoto waliofariki dunia kutokana na sumu hiyo ni mwenye umri wa miaka 12 na miaka miwili.
“Watoto wengine wamelazwa Kituo cha Afya, Bwanga pamoja na mama yao akiwa chini ya ulinzi wa Polisi,”amesema Mwaibambe
Watoto wawili wamefariki dunia baada ya mama yao mzazi, Veronica Gabriel (30), mkazi wa Kijiji cha Mwabagaru, Kata ya Buseresere, Wilaya ya Chato, mkoani Geita kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.
Hata hivyo mama huyo amenusurika kifo licha ya kunywa sumu hiyo kwa madhumuni ya kujiua
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe inasema mama huyo mwenye watoto watano aliwanywesha watoto wote sumu ya kuua wadudu kwenye nyanya na wawili kati yao kufariki.
Watoto hao wanumri kati ya mwaka mmoja na miezi tisa na miaka 12.
Watoto waliofariki dunia kutokana na sumu hiyo ni mwenye umri wa miaka 12 na miaka miwili.
“Watoto wengine wamelazwa Kituo cha Afya, Bwanga pamoja na mama yao akiwa chini ya ulinzi wa Polisi,”amesema Mwaibambe
Kwa vile sehemu za Dini zimekuwa siyo kimbilio tena kwa watu walioshikwa na matatizo basi naomba serikali ianzishe kitengo cha kutatua shida zilizozidi kwa kuwapa mafunzo na mtaji na wawe wanajulikana ofisi zao pia wawe na vipindi kwenye TV kuonyesha Kila mwezi ni jamii ngapi zimesaidiwa kama anavyofanya frola wa Mwanza.
Miaka 60 ya Uhuru!!!hali ya maisha ya mtanzania inasikitisha sana
Ajira ni tabu
Gharama za maisha hazifai
Watanzania wengi wamepoteza matumaini!!!
Wanasiasa ndio wanaotamba!?
Kweli ni huzuni Hili Taifa!
Inasikitisha. Taji liundi akisoma hii itamkumbusha ndugu zake walivyofariki dunia baada ya mama yao kuwapa sumu.
Yaani si angewapeleka hata wilayani ili serikali iwalee.