Ugumu wa Maisha nchini Marekani upo kwenye nini hasa?

Ugumu wa Maisha nchini Marekani upo kwenye nini hasa?

TUKANA UONE

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
2,345
Reaction score
6,970
Ubaya Ubwela & Nyie Hamuogopi vimepita,tujikite kwenye mada kuntu!

Kuna mshikaji wangu mmoja tulimaliza wote Sekondari na bahati nzuri hata chuo tukasoma wote,Mimi na yeye tulitokea Kuwa marafiki sana na hata hapo nyuma Kuna Uzi niliuweka hapa unaohusu maisha ya Ughaibuni nilimzungumzia!

Baada ya sote kumaliza chuo hatukuwa vizuri kiuchumi,hivyo tukaunganisha nguvu Kwa pesa kidogo tulizokuwa nazo tukaona tufanye biashara ya nafaka,Biashara mwanzo ilikuwa na changamoto ila tukakomaa hatimaye tukajipata,nyumbani kwao ilikuwa kama kwetu na kwetu kama kwao!


Mama yake amezoea kuniita pacha wa Mwanaye kwasababu tulikuwa hatuachani!

Kumbe jamaa alikuwa anafanya mipango ambayo alijua yeye alifanyaje fanyaje ghafla anakuja kuniambia amepata Visa ya Kwenda Marekani,so nikamuuliza Marekani anakwenda Kusoma au?,Akaniambia amepata mchongo wa kazi!

Nikamuuliza mbona imekuwa ghafla sana na hakunishirikisha kama rafiki yake?,ok hilo nikaachana nalo maana ilikuwa ni pasheni yake siku nyingi kutimkia huko maana hata wakati tunafanya biashara ndoto zake ilikuwa kutimkia huko!

Ila baada ya yeye kufika huko akaniambia Kuna wabongo wengi wanatimkia huko kupitia Kongo na Burundi,sijui kama ni kweli au alinidanganya maana hata yeye anasema alipewa mchongo na wabongo hivyo akalipa Hela akaenda hadi Burundi ndiko alikoondokea,Sina hakika lakini sikujali sana!

Nakumbuka kabla ya kuondoka siku tukiwa pale kwao,mama yake wakati anamuaga jamaa alikuwa akilia Kwa Uchungu sana na kimhakikishia mama yake kwamba anaenda kupambana na atahakikisha kila Mwezi atakuwa anamtumia Hela ili wajenge nyumba za kiwango Cha Kimataifa!,Binafsi nilimtia moyo nikamwambia asije kuwasahau ndugu zake na mama yake kwasababu amebakiwa na dada 3 na mama yake na yeye ndiye kijana mkubwa na wapekee!

Kweli jamaa aliondoka na baada ya kufika huko tukawa tunawasiliana hadi Leo na bahati nzuri haikuzidi miezi 3 jamaa akaniambia amepata makaratasi (Documents)ambazo pia zimempa kibali Cha kufanya kazi,alipoanza kazi kiukweli alikuwa akimtumia mama yake kila mwezi Dolla 1000 na akaniaomba niwasaidie kuwatafutia kiwanja maeneo ya Tegeta,nilifanikiwa kupata eneo ambalo lilikuwa likiuzwa pesa chafu ambako nikajua fika kwasababu jamaa anajitafuta hawezi kulimudu,nikamshauri nimtafutie eneo mahali pengine ambako ni nje ya mji na bei ambayo ataimudu,baada ya kumwambia jamaa akagoma akasema yeye anataka Tegeta,hivyo nikamwambia Kuna eneo hilo la mara ya kwanza bei yake ni Tsh 150 milioni,nikaona jamaa hashituki,duuuuu nikapatwa maswali sana uenda jamaa kweli kapata kazi ya maana,kwasababu alikuwa akiniambia mahali anapofanya kazi analipwa $ 30 Kwa Siku na anafanya kazi saa 8,hivyo nikapiga hesabu zangu Kwa haraka haraka nikagundua jamaa Kwa mwezi anakunja si chini ya milioni 16 Kwa kipindi hicho!

Kweli nikaona jamaa ana kiburi kwasababu vumba lipo,Kile kiwanja hakukipenda tukatafuta kingine tukaambiwa ni Tsh 100 milioni,hivyo jamaa akamwambia mama yake pesa anayomtumia kila mwezi hiyo $ 1000 iwe Niya matumizi,kuhusu kiwanja atatuma Hela Kwa mkupuo!

Wakati huo jamaa alikuwa ananimbia anaishi chumba kimoja tu chenye choo ndani na kabati la nguo na kisehemu Cha jiko analipa $ 2000 Kwa mwezi!

Siku za hivi karibuni mama yake amekuwa akilalamika jamaa hamtafuti na hata Hela ya kula tu inawapiga Chenga,hivyo anakuwa akiniambia ninapowasiliana naye nimkumbushe kuhusu hilo,lakini kila nikiongea na jamaa naye anakuwa mkali sana na kulalama kwamba hao ndugu zake wanadhani maisha ya huko ni mepesi kihivyo?,au wanadhani Hela anachota?

Kwa namna jamaa ambavyo huwa anaongea Kwa ukali,Mimi binafsi huwa naingia mfukoni mwangu nachukua pesa yangu nampelekea au namtumia mama yake na kumwambia imetoka Kwa jamaa lakini ukweli naujua Mimi namna jamaa anavyokuwaga mkali!

Kuna kipindi aliniambia Ile apartment aliyokuwa akikaa alihama na alihamia kijichumba kikubwa ambacho amekitenganisha kimekuwa chumba sebule ambacho analipa $ 4000 Kwa mwezi!,Nikamwambia kwanini asingeendelea tu kukaa pale pale kwenye Kodi ndogo Ili atimize malengo yake ila unajua unajua ndo zinakuwa nyingi!,nikamuuliza uenda kapata kazi mahali pengine palipo mlazimu yeye kuhama pale akasema kazi anafanya pale pale ila kaamua tu kubadiri makazi!

Kila nikimwambia ishu za maisha ya mama yake na ndugu zake jamaa anakuwa mkali kinoma na kuniambia ishu kibao ikiwemo Bills kitu ambacho kinafanya maisha kwake yasiwe rahisi na rafiki kuwatumia ndugu zake na mama yake pesa!

Swali ninalojiuliza,Je wakati amefika anaanza kazi na kila mwezi alipokuwa akimtumia mama yake pesa,Je hakuzijua hizo Bills?


Labda niwaulize swali ndugu zetu mnapokaa huko Marekani Kiranga na wengineo,Je ishu za Bills huko ni kubwa kiasi gani?

1.Je,ugumu wa bills upo kwenye Umeme?
2.Je ugumu wa Bills upo kwenye Maji?
3.Je Ugumu wa Bills upo kwenye Gesi?
4.Je Ugumu wa Bills upo kwenye Usafiri?
5.Je Ugumu wa bills upo kwenye Misosi?
6.Je Ugumu wa Bills upo kwenye Nyumba?
7.Je Ugumu wa Bills upo kwenye Internet?

Je,Bills ni kubwa sana kiasi kwamba msibaki na chochote kitu hata kusevu mnashindwa?,Kama ndivyo kwanini mnaendelea kuteseka huko?

Hebu nieleweaheni ndugu zangu Ugumu wa Maisha uko upo kwenye kitu gani?maana jamaa amekuwa akiwa mkali kama pilipili kila nikimgusia suala la kumtumia mama yake pesa,na kumbuka kila mwezi anapata zaidi ya $ 7000

Mmekuwa mkituambia kwamba huko kazi zipo za kutosha labda ushindwe wewe tu,Sasa kama kazi zipo za kutosha Ugumu wa Maisha unasababishwa na kitu gani?,Tumezoea kuona Watanzania wengi wanalia kuhusu Ugumu wa Maisha Kwasababu hakuna kazi zenye kipato kizuri,kama huko kazi zipo tena zenye kipato kizuri,Ugumu wa Maisha unasababishwa na kitu gani?
 
mimi niko dunia ya upili siyajui ya dunia ya kwanza. dogo kashakua limbukeni. lakini na home kwao walipaswa kutengeneza source of income na sio kukinga tu kila mwezi. dalari 1000 ni pesa mingi kila mwezi..wangejipanga leo wangeacha utegemezi
Mkuu mama yake ameshakuwa mtu mzima na anahitaji msaada wa kijana wake,pia kijana wake ndiye aliyemwambia pesa atakayokuwa anamtumia asifanyie chochote zaidi ya matumizi ya nyumbani,mipango ya maendeleo wamuachie yeye atamalizana nalo
 
Mkuu mama yake ameshakuwa mtu mzima na anahitaji msaada wa kijana wake,pia kijana wake ndiye aliyemwambia pesa atakayokuwa anamtumia asifanyie chochote zaidi ya matumizi ya nyumbani,mipango ya maendeleo wamuachie yeye atamalizana nalo
kumbeee..huyo dogo ana laana mamaye zake kashajaa kwenye mfumo wa ulimbukeni
 
duuuuu nikapatwa maswali sana uenda jamaa kweli kapata kazi ya maana,kwasababu alikuwa akiniambia mahali anapofanya kazi analipwa $ 30 Kwa Siku na anafanya kazi saa 8,hivyo nikapiga hesabu zangu Kwa haraka haraka nikagundua jamaa Kwa mwezi anakunja si chini ya milioni 16 Kwa kipindi hicho!
😝😝😝😝
 
Mkuu mama yake ameshakuwa mtu mzima na anahitaji msaada wa kijana wake,pia kijana wake ndiye aliyemwambia pesa atakayokuwa anamtumia asifanyie chochote zaidi ya matumizi ya nyumbani,mipango ya maendeleo wamuachie yeye atamalizana nalo
Sasa za kuambiwa si unachanganya na za kwako???
 
Waliowahi kufika huko majuu wanasema, ukiwa kitombise matokeo yake unakutana na kitu wenyewe wanaita child support...

Wanasema hiyo ni noma... ndio ilimkimbiza Le Mubebez akaja kufia huku kajambanani baada ya kuishi majuu kwa miaka 30!

Huyo jamaa'ako kashauingia huo mfumo.
 
Waliowahi kufika huko majuu wanasema, ukiwa kitombise matokeo yake unakutana na kitu wenyewe wanaita child support...

Wanasema hiyo ni noma... ndio ilimkimbiza Le Mubebez akaja kufia huku kajambanani!

Huyo jamaa'ako kashauingia huo mfumo.
ukiwa nje wazungu ni nje au kinga mfuko
 
Kuna kitu kwa kiingereza kinaitwa Revulsion : a sudden change of feeling especially from love to hate: nina mashaka huyo kijana kupatwa na hiyo hali kwa mama yake na nduguze sio bure, ila sasa cha kujiuliza ni kwamba hiyo hali imesababishwa na nini...!!!!??? Is nobody's guess.

Kwa sababu mbona mara ya kwanza alianza vizuri tu sasa nini kilicho mbadilisha ghafla..? Na hakuna uthibitisho kwamba baadaye amekuja kupata majukumu makubwa ya kumfanya abadili msimamo ghafla.
 
Kuna kitu kwa kiingereza kinaitwa Revulsion : a sudden change of feeling especially from love to hate: nina mashaka huyo kijana kupatwa na hiyo hali kwa mama yake na nduguze sio bure, ila sasa cha kujiuliza ni kwamba hiyo hali imesababishwa na nini...!!!!??? Is nobody's guess.

Kwa sababu mbona mara ya kwanza alianza vizuri tu sasa nini kilicho mbadilisha ghafla..? Na hakuna uthibitisho kwamba baadaye amekuja kupata majukumu makubwa ya kumfanya abadili msimamo ghafla.

Kapata akili kagundua hawezi kuwa everyone's savior. Ajenge maisha yake hao wengine wapambane na maisha yao. Utawalisha hadi lini?
 
mimi niko dunia ya upili siyajui ya dunia ya kwanza. dogo kashakua limbukeni. lakini na home kwao walipaswa kutengeneza source of income na sio kukinga tu kila mwezi. dalari 1000 ni pesa mingi kila mwezi..wangejipanga leo wangeacha utegemezi
Yes sahihi maana binaadamu huumwa au kufa 2.8m kila mwezi wangetafuta biashara
 
Alianzia na kuwazoesha vibaya katika maisha ya kibongo mshahara wa kwanza ndo unaweza kuugawa wote Kwa waliokupush ukafika hapo kama Asante na sio kulipa fadhila baada ya hapo tuma Hela Kwa ubahili sana na Kwa malengo usitoe ela constant itakughalimu siku ukibadili mfumo.

Ndo imemkuta jamaa baada ya kuwa huko amekutana au amefinguliwa macho michezo ya kutuma Hela nyumbani na kutumika ndivyo sivyo mfano watu ujifanya wanaugua mara Kwa mara , misiba, matatizo ya ukoo, uhaba wa chakula , yaani utaona shida za kila rangi adi upige salute ila ukiwapa masharti magumu ya kutoa pesa aisee yaani watakutafuta Kwa utaratibu mzuri sana .
Kuna jamaa yangu alifika mbele ana ata miezi sita ila dm yake inajaa maitaji ya million 5 Kwa mwezi wakati mtu ndo bado Yuko anajitafuta alisajili namba nyingine mpya haraka kupunguza mambo hayo
 
Back
Top Bottom