Samico Tanzania
JF-Expert Member
- Feb 6, 2022
- 486
- 1,237
Kiuhalisia kabisa hakuna kitu kinachothibitisha UGUMU WA MAISHA!
Hili ni jambo la kufikirika tu ambalo viumbe na wanadam waliamua kuyabatiza maisha!
Binadamu kaumbwa na akapewa mazingira ayatawale! Sasa unaposema MAISHA Ni MAGUMU mimi huwa simuelewi Magumu kwa kuyalinganisha na yepi?
Binadamu kapewa mazingira ili yampatie chakula, na chakula kipo aina nyingi tu!
Taarifa Alizonazo mtu kuhusu mazingira ndizo humfanya ashibe au aliye njaa!
Lakini kiuhalisia ugumu wa maisha hili jambo halipo!
Kuna watu mtakuja nakusema labda mimi ni mtoto wa kishua!
Story ya maisha yangu nilishwahi kuiweka humu!
Mimi nilipomaliza msingi wazee walilalamika ooh Maisha magumu sijui hawana Ada, Nikawaambia Mbona hatuna maisha magumu sisi!
Nikaondoka nikaenda Hanang'i kuchunga ng'ombe! Pamoja na kuchaguliwa kwenda shule maalum ya vipaji (moshi technical) lakini nilikubali kwenda kuchunga ng'ombe kwanza!
Nikiwa polini maisha yalikuwa matamu sana, nilikula matunda aina nyingi, nilichoma nyama nipendayo, nilicheza michezo ambayo binadamu ilinipa furaha, nilifunza dawa nyingi mno karibia 1200 za kutibu magonjwa mbalimbali!
Wakati wa likizo wala sikushangaa hao waliokwenda secondary waliporudi nakunikuta nachunga ng'ombe!
Hadi pale nilipotosheka nikapatiwa zawadi ya ng'ombe na kwenda kusomea ufundi umeme!
Baada ya kumaliza nilijiajili, nimefanya kazi za umeme ndani ya nchi na inje ya nchi, nimefanya kazi za umeme na wachina, wafrika, wafilipino, wajerumani, wajapan n.k!
Hadi sasa nafanya kazi zangu za umeme sijui kuhusu ugumu wa maisha!
Juzi wakati natokea Dodoma nilipita kwrnge gereza moja hapo morogoro kumsalimia moja ya tuliofaulu nao darasa la saba, wakasoma ngazi za master huko nilimkuta pale jamaa anatumikia kifungo baada ya taasisi aliyokuwa anaisimamia kupata hasara ya mabilioni ambayo inadaiwa kama waliyaiba!...Bado nilipomtembelea nilimwambia jamaa Hakuna ugumu wa maisha nikampatia na mifano hai nikamsihi avumilie kifungo kuna fursa mbele!
Mungu karuhusu tuje hapa duniani tukiwa kama sisi, na mazingira ya kuishi yashaandaliwa!
Tatizo kubwa la wanadamu wengi tunapenda sana kujilinganisha na wengine! Baada ya kujilinganisha ndiyo tunakuja na ubatizo wa MAISHA MAGUMU!
Kiuhalisia hakuna kitu kinachothibitisha maisha magumu! Mimi nafanya kazi za umeme, siku watu wasipojenga naanza kutibu watu ninajua dawa zaidi 1200.
Ukiachilia kujua dawa ninao uwezo wa kuangalia eneo mazingira na mimea ardhini nikagundua uwepo wa maji ukichimba au hakuna!
Nina uwezo wa kukaa msituni na wanyama wakali na wasinifanye chochte kwa kutumia mimea hiyo hiyo iliyopo porini!
Sasa hayo maisha magumu ni kitu gani, unayalinganisha na nini hadi uthibitishe maisha ni magumu?
Narudia tena kushindwa kutumia mazingira ndiko wengi kunawalaza njaa! Lakini hakuna kitu kinaitwa maisha magumu
Mazingira yanasifa kama silaha; Usipojua kuyatumia unaweza kujimaliza mwenyewe!