Andrew Tate
JF-Expert Member
- Jun 28, 2020
- 4,503
- 6,861
Una majibu simple sana.Ushajijibu mwenyewe kwamba maisha magumu hayana kipimo unataka nipruvu nini zaidi!
Jambo ambalo halina kipimo maana yake halipo!
Na lisipokuwepo maana yake ni la kufikirika! Halipo
Sija-jijibu mimi. Bali umejijibu mwenyewe. Unajichanganya na kujikanyaga. Kichwa cha habari kinasema
"
Ugumu wa maisha ni jambo la "kusadikika" halipo "kiuhalisia" na sijawahi kuliona na halitatokea
"Mada kuu hapa ni "uhalisia." "Maisha magumu." Simply ni subdivision. Je unaweza kupima "uhalisia" wa "muono" wako huo? Hapana, hauwezi. Je kunaondoa "uhalisia" wa huo "muono" wako kwako? Hapana vilevile, na ndio maana umeanzisha hii thread kwa kujiamini.
Kusema "jambo ambalo halina kipimo ni halipo." Sio fact. Bali ni muono na uhalisia wako wewe, proof ni wewe kuanzisha hii thread. Unakumbuka ulisema "simama mwenyewe"? Hicho ndicho ulichokifanya hapo. Na wengine wana haki ya "kusimama wenyewe" kama wewe.
Hapo itabidi tujue maana yako ya "uhalisia." Swali ambalo huwezi kulijibu na nina uhakika hulielewi. Lakini haijalishi. Sababu kwa kukusoma wewe, inaonekana bila kujua, unaamini "uhalisia ni kitu binafsi." Kitu ambacho ni sahihi.
Kwa maana hiyo, hata: kwa mujibu wa uhalisia wako, ambao ni "halisia za wengine ni za kufikirika." ni kitu kinachofanya uhalisia wako uwe ni kitu cha kufikirika vilevile. Maana yake "uhalisia" wako hauna maana yoyote kwa wengine. Sababu kila mtu ana wake.
Vinginevyo itabidi useme ni kitu gani kinachofanya "uhalisia" wako uwe halisi kwa wote na sio kwamba ni "fikra" zako tu.
Na utajuaje kama huo "uhalisia" wako ni halisi na sio wa kufikirika kwa asilimia 100%?
Kitu ambacho kamwe hautoweza kukifanya sababu the human consciousness has always been individualistic, never absolute, nor physically definable. Kitu kinachofanya "Uhalisia" always uwe kitu ambacho ni personally defined. Kama unavyofanya wewe hapa. Kitu ambacho hauko aware nacho.
Nimejaribu kuandika wazi kwa kiswahili chepesi na bado umeshindwa kuelewa ninachokiongelea wala unachokiongelea.
Kuna kitu wanaita Metacognition. Ni hali ya kufikiria, unachokifiria. Yaani uwezo wa kuona mawazo yako mwenyewe, na ya watu wengine, wanafikiria nini na kwanini. Metacognition ndio kitu ambacho bila shaka huna. Uwezo wako wa kufikiri bado ni mdogo sana, naive na personally limited. Hali inayofanya ushindwe kuelewa ninachokiongelea.
Mada ya "uhalisia" na nini ni "halisi" na nini sio "halisi" sio ya kitoto kiasi cha kuja na superficial pseudo-intellectual arguments, especially personally limited ones.
Kama umeshindwa kuelewa na kumake simple abstract reasoning. Then hauko kwenye nafasi ya kusema chochote juu ya kipi ni "uhalisia." Na kipi sio "uhalisia."
Sababu hata hivyo, siku zote huo utabaki kuwa "uhalisia" wako tu.