Ugunduzi wa Erasto Mpemba, (Maji ya moto kuganda haraka kuliko ya baridi) 'The Mpemba Effect' kwanini hatukufundishwa mashuleni?

Ugunduzi wa Erasto Mpemba, (Maji ya moto kuganda haraka kuliko ya baridi) 'The Mpemba Effect' kwanini hatukufundishwa mashuleni?

Wajanja hupenda kukosolewa ili kuongeza elimu.Wasio hekima huchukia kukosolewa kwa sababu ya inflated ego.
 
kweli hata mimi sijawahi kumsikia na kibaya zaidi sijawahi kusoma hiyo theory popote pale ingawaje nimesoma physics.


The same to me, nimesoma physics/chemistry lakini hiyo effect sijawahi kuisikia ama enzi zetu ilikuwa haijatiwa kwen vitabu? hata huyo Mpemba ndo nimemsikia hapa...thanks to JF.....lakini yupo wapi wakati huu?
 
japo mimi sio mzuri sana wa kiingereza lkni hapo umekosea kidogo kwani mtu anayesoma fizikia kwa lugha ya kiingereza anitwa physicists na sio physician, nafikiri physician ni mganga, na hivyo ni vitu viwili TOFAUTI kabisa.....tumia lugha ya kwetu bro hautachemsha.....

Kijakazi,
Looks like you are correct! But why take more attention on the (typing of) the words or whatever, than the content of the message? You do not look like someone who deals with the "marginals" in her/his life, but apparently you must be!
 
Nashukru hii hoja imeibuka tena.Maana niliiweka hapa JF 06.11.07 Elimu na haikupata mchango.

Sasa naambiwa wapo wengine Kama;
1.Prof Shaba huyu ni Profesa wa medicine,Muhimbili ambae sasa kastaafu.Alikuwa mtu wa kwanza kueleza mabadiliko ya chembechembe kwenye ini linalosinyaa kutokana na madhala ya pombe(hepatocyte changes in Liver Cirhosis,1984)

2.Prof.Kaisi wa magonjwa ya akina mama Muhimbili,Mchango wake kwenye jedwari la kuratibu maendeleo ya mama mjazito wakati wa kujifungua 1974,baadae ikawa modified na daktari kutoka Zimbabwe

Nafikiri kuna haja ya kuwaenzi wataalam wetu bila kusubili utashi wa wanasiasa.Ni Rahisikusema Bibi titi street,kuliko kusema Mpemba road nk
 
mkama tatizo ni preferences zetu sisi na viongozi. The only place to make you remembered is politics.
Bado hatuna vipaumbele vya elimu
 
thread inasoma kuwa kwa nini wanasiasa wetu hawamuenzi.....?
umeshasema wanasiasa halafu dont complain maana there is no science in politics, there is lots of tricks and trips. Hivyo usiote hata ndoto kuwa kuna siku mpemba ataenziwa full stop.
Tanzania is a country which burries brights and creativeness.
I dare to talk openly kwamba tabia ya wanasiasa wetu haitobadilika mpaka watakapoacha kuiba kura
 
Nashukru hii hoja imeibuka tena.Maana niliiweka hapa JF 06.11.07 Elimu na haikupata mchango.

Sasa naambiwa wapo wengine Kama;
1.Prof Shaba huyu ni Profesa wa medicine,Muhimbili ambae sasa kastaafu.Alikuwa mtu wa kwanza kueleza mabadiliko ya chembechembe kwenye ini linalosinyaa kutokana na madhara ya pombe(hepatocyte changes in Liver Cirhosis,1984)..

.... Na sasa anaface wakati mgumu na uvumbuzi wake kwani ameamua kusinyaisha ini lake kwa kubugia vinywaji vikali mno. Tumuombee kwa mola aweze kubadilika mtu huyu adhimu.

Pia itabidi tumuenzi aliyevumbua yale mabomba ya maji ya mianzi.... au mnasemaje wanaforum?

leteni majina tuandandae kitabu cha mabingwa wa afrika/tanzania
 
Huyo mtu mnamsema mbona sioni alichokigundua,zaidi ya hadisi za wauza ice cream ambao nao wanalijua hilo,sababu gani imfanye awe katika kundi la wanasayansi hata aenziwe na Serikali au kama mlivyowakilisha wanasiasa.
Kama angeendelea na kutoa sababu ya msingi hapo angekubalika lakini kila nionapo zaidi amekuwa akihoji kwa nini jua halitoki magaribu na kuelekea mashariki.
 
Sidhani kama ni wajibu wa wanasiasa wetu kuwaenzi watu (mashuhuri). Huo ni wajibu wa jamii. Mimi na wewe tuna wajibu huo pia. Tukitegemea kila kitu kwa wanasiasa hatutafika popote.
 
Huyo mtu mnamsema mbona sioni alichokigundua,zaidi ya hadisi za wauza ice cream ambao nao wanalijua hilo,sababu gani imfanye awe katika kundi la wanasayansi hata aenziwe na Serikali au kama mlivyowakilisha wanasiasa.
Kama angeendelea na kutoa sababu ya msingi hapo angekubalika lakini kila nionapo zaidi amekuwa akihoji kwa nini jua halitoki magaribu na kuelekea mashariki.

Mwiba,
Ni kweli kwamba hadithi hii wewe umelishikilia ya wauza ice cream lakini kumbuka hawa wenzetu weupe wamekuwa wakigundua vitu ambavyo sisi tumevikumbatia kwapani mwetu, mfano Lake Tanganyika David livingstone alivumbua Ziwa Tanganyika kitu ambacho si kweli bali naweza kusema alikuwa ni mzungu wa kwanza kuona Ziwa Tanganyika. Kwa hiyo hata kama kuna vitu tuko navyo kila siku mwenzetu mmoja anapogundua faida mbadala tumpe hongera zake tusisubiri hadi iwe ni mzungu.
 
Huyo mtu mnamsema mbona sioni alichokigundua,zaidi ya hadisi za wauza ice cream ambao nao wanalijua hilo,sababu gani imfanye awe katika kundi la wanasayansi hata aenziwe na Serikali au kama mlivyowakilisha wanasiasa.
Kama angeendelea na kutoa sababu ya msingi hapo angekubalika lakini kila nionapo zaidi amekuwa akihoji kwa nini jua halitoki magaribu na kuelekea mashariki.

Mwaiba,

Nafikiri wewe sio mwanasayansi, unafikiri wanaogundua vitu
wanaumba mtu kwa udongo? Uvumbuzi ni mambo haya haya madogo ambayo tunayo kila siku. Siku hizi kuna usemi kwamba haijalishi unajua nini bali umejua lini, mwenzetu aliona kile ambacho wengi walikuwa hawana uwezo wa kukiona.
 
Mwaiba,

Nafikiri wewe sio mwanasayansi, unafikiri wanaogundua vitu
wanaumba mtu kwa udongo? Uvumbuzi ni mambo haya haya madogo ambayo tunayo kila siku. Siku hizi kuna usemi kwamba haijalishi unajua nini bali umejua lini, mwenzetu aliona kile ambacho wengi walikuwa hawana uwezo wa kukiona.
Hii habari nimeisoma tokea mwanzo,huyo jamaa alipofika kwa wauza ice cream ,aliwakuta wanaijua hali hiyo zamani.
Ila alichofanya huyu ni kutaka kuwazidi nguvu kwa vile tu yeye amekwenda shule ,sababu iliyomfanya awazidi kete.Kama ulivyosema haijalishi unajua nini bali umejua lini kwa hivyo hii prosesi itakwenda hadi mmoja atapata facts na huyo ndie atakuwa mvumbuzi kama Livingstone ambae ndie alievumbua Ziwa Tanganyika alipokuwa akikatiza mwitu wenyeji hata walikuwa hawana habari ,wakiogopa kuliwa na simba sababu iliyowafanya wasiweze kucheza mbali au kwenda mbali.
 
Huyo mtu mnamsema mbona sioni alichokigundua,zaidi ya hadisi za wauza ice cream ambao nao wanalijua hilo,sababu gani imfanye awe katika kundi la wanasayansi hata aenziwe na Serikali au kama mlivyowakilisha wanasiasa.
Kama angeendelea na kutoa sababu ya msingi hapo angekubalika lakini kila nionapo zaidi amekuwa akihoji kwa nini jua halitoki magaribu na kuelekea mashariki.

Nina wasiwasi na uelewa wako wa mambo mengi!
Yaani vitabu vya rejea pamoja na maelezo yote ya Mpemba hapo juu bado tu hujaelewa jamaa kafanya nini mpaka sasa?
Kazi kweli kweli!
 
Jana katika mizunguko ya hapa mjini, nimekutana na mzee mmoja anaitwa Mpemba...ktk mazungumzo nilipomuambia nilisoma MKWAWA alistuka na kuniuliza kama nimewahi kusikia anything about MPEMBA EFFECT? Kilikuwa ni kitu kigeni sana kwangu.... Akaanza kunisimulia kuwa kuna siku akiwa O'level aligombana na rafiki yake baada ya kuchukua maji yaliyoganda kwenye freezer wakati alichelewa kuyaweka na aliweka yakiwa ya moto....

Aliyefanya pachimbike ni rafiki yake ambaye aliweka maji ya baridi kwenye freezer na kwa mapema zaidi...huyu bwana kila alipojitetea alionekana mzushi mpaka mwalimu wake FIZIKIA akamtandika kwa kudai hajui fizikia na ameiba maji ya mwenzake bila kuconsider facts kupoa kwa maji hayo.

Kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa maji aliyochukua ni ya kwake akaamua kufanya experiment peke yake na kugundua kuwa MAJI YA MOTO YANAGANDA HARAKA KULIKO YALE YALIYOPO ROOM TEMP. alipowaambia walimu wake na wanafunzi waliishia kumcheka bila kujaribu pia..

Alipofika A'level Mkwawa sec akaamua kufanya tena na kuandika paper na prof mmoja kutoka UD akamuona na alimshangaa sana na kuipublish paper hiyo.... Na mpaka leo ugunduzi huo unaitwa ''mpemba effect'' watu wengi wanashangaa na hawaamini lakini its real...

For more info google ''mpemba effect''
 
Du!
nai google sasa hivi hiyo mpemba effect!lakini nikitoka hapa break ya kwanza ku-prove mwenyewe kwenye kafreezer kangu ka mkoloni!!nitatoa ushuhuda wa niliyoyapata kesho!!
 
Ebwana eeh!! Hii ndo naipata leo wana JF, what happened to our education system? Yaani toka std one mpaka ngazi hii ya juu kabisa katika mfumo wa elimu duniani, sijawahi kusoma wala kusikia hii kitu!! Je hii ni kwa sababu shule zetu za voda fasta hazina well equiped libraries??? or waalimu tunaowaandaa kama chips za "american chips" kinondoni??

Anyway, wacha tujikite kwenye porojo za mafisadi, kugombea mafuta hewa na malumbano ya whether zanzibar ni nchi ama sio nchi, mambo ya msingi yametushinda wadanganyika!
 
Hii tulishawahi kuiongelea hapa, the ancients wa enzi za Ugiriki ya kale walilijua hili lakini sayansi ya leo ililipoteza, na Mtanzania akaja kulivumbua upya.

Ile library ya Alexandria inge survive tungekuwa mbali sana.

Ona

Mpemba effect - Wikipedia, the free encyclopedia

Mpemba Effect: Hot Water Freezes before Cold - Succeed in Physical Science: School for Champions

Bluray,

Hii kitu niliisikia nikiwa Arusha miaka ya 80 mwishoni kutoka kwa mwalimu wangu. Yeye aliniambia kuwa wanafunzi walikuwa wanagandisha maziwa na mmoja akichemsha kidogo na kuyaweka, yalikuwa yakiganda haraka kabla ya wenzake na apata ice cream mapema kabla ya wenzake. Alituambia kuwa jamaa aliipeleka hii kitu hadi UDSM na baadaye ikaenda hadi UK na kupotelea huko. Kumbe si kweli kuwa ilipotea ila ipo na imeandikwa. Nashukuru kwenye Wikipedia wameweka hadi jina la kijana.

Hata yule Mrumunia(Henri Coanda) na yeye alianza kama mchezo na leo hii ugunduzi wake unatumika sana kwenye AERODYNAMICS. Hapa chini naweka link ili kila mtu aijaribu hii COANDA effect ambayo unahitaji tape water na kijiko. Shika kwa juu na kisogeze kwenye maji yanapotiririka. Jaribu upande wa ndani kwanza na mwisho jaribu wa nje.... Mhhh, waweza tumia hata KUPULIZA UPEPO. Angalieni hii film...

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=AvLwqRCbGKY&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
Mhhh, check Mpemba Effect katika picha. Kumbe kuna watu hadi leo bado wanaifanyia utafiti. Inafurahisha jamaa anaposema "We've got Mpemba..."

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=lA1OHyzReuY&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
Jana katika mizunguko ya hapa mjini, nimekutana na mzee mmoja anaitwa Mpemba...ktk mazungumzo nilipomuambia nilisoma MKWAWA alistuka na kuniuliza kama nimewahi kusikia anything about MPEMBA EFFECT?kilikuwa ni kitu kigeni sana kwangu....akaanza kunisimulia kuwa kuna siku akiwa O'level aligombana na rafiki yake baada ya kuchukua maji yaliyoganda kwenye freezer wakati alichelewa kuyaweka na aliweka yakiwa ya moto....aliyefanya pachimbike ni rafiki yake ambaye aliweka maji ya baridi kwenye freezer na kwa mapema zaidi...huyu bwana kila alipojitetea alionekana mzushi mpaka mwalimu wake FIZIKIA akamtandika kwa kudai hajui fizikia na ameiba maji ya mwenzake bila kuconsider facts kupoa kwa maji hayo.
kwa kuwa alikuwa na uhakika kuwa maji aliyochukua ni ya kwake akaamua kufanya experiment peke yake na kugundua kuwa MAJI YA MOTO YANAGANDA HARAKA KULIKO YALE YALIYOPO ROOM TEMP. alipowaambia walimu wake na wanafunzi waliishia kumcheka bila kujaribu pia....
alipofika A'level Mkwawa sec akaamua kufanya tena na kuandika paper na prof mmoja kutoka UD akamuona na alimshangaa sana na kuipublish paper
hiyo....na mpaka leo ugunduzi huo unaitwa ''mpemba effect'' watu wengi wanashangaa na hawaamini lakini its real......
for more info google ''mpemba effect''

E bwana waweza kutusaidia jinsi ya kumpata huyu mzee 🙂
 
Back
Top Bottom