Uhaba wa chanjo kwa watoto wachanga

Uhaba wa chanjo kwa watoto wachanga

Planett

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
10,497
Reaction score
16,180
Ramadhan kareem kwa ndugu zangu waislamu,

Wakuu kuna hiki kitu nimekutana nacho huenda ni kawaida ila kwa miongo zaidi ya mitatu niliyopo hapa duniani ndio naona kwa mara ya kwanza.

Ni hivi, mke wangu kajifungua na ninavyojua (huenda nikawa sipo sahihi) kuna ile chanjo ya begani hua hua mtoto anachomwa pindi nanapozaliwa.

Sasa kwenye hiyo hospitali nimeambiwa chanjo hazipo tusubiri hadi tutakapotaarifiwa! Nikicheki naelekea wiki ya tatu sasa na hakuna taarifa yoyote juu ya uwepo wa chanjo hiyo na inasemekana hii ni kwa chanjo zote za watoto kwenye hiyo hospitali (hospitali ya wilaya) hazipo.

Sasa wasiwasi wangu ni Je! mtoto asipopata hizi chanjo KWA WAKATI au ASIPOPATA KABISA kunaweza kuwa na madhara gani?

cc Wizara ya Afya Tanzania
 
Mm mke wangu alipo jifungua zilipita wiki mbili ndo akachomwa hio ya begani saiz chanjo zimekua adimu watoto hawachomwi kwa wakati.mkoa wa njombe hili swala imenilazimu nimpeleke mwanangu mbeya ili akapate chanjo zote kwa wakat
 
Hospitali karibu zote nchini chanjo za watoto ziliadimika. Zimeanza kupatikana kwa uchache wiki iliyopita.

SABABU: mabeberu walikaza
 
Mke wangu mwanzoni mwa mwaka huu alienda kujifungua kwao Mafinga.
Mwezi march akafanikiwa kujifungua(Mungu ni mWema)
Hapo tulikosa chanjo ya kwanza ndani ya wiki mbili,mpka ya tatu tukawa tunapewa majibu hayohayo chanjo hakuna,ikabidi tutafute Njombe na Iringa nako huko hatukufanikiwa kupata.
Mpka akatimiza mwezi.
Week jana nimeenda kumchukua huko,ili apate chanjo huku kwetu mkoa wa Pwani.
Kukosekana kwa chanjo kumenigharimu sana kifedha.
Na kuvuruga ratiba na mipangilio zangu ambazo baada ya kujifungua nilitak kutekeleza,lkn ikawa ngumu kufanya maana mtoto hana kinga yeyote .

Hebu serkali kama inapepesa macho mpk huku itupe majibu.
Ni kwanini chanjo imeadimika haswa ktk mikoa inayotajwa,ni nini tatzo?
 
Hiyo chanjo ni muhimu sana kwa mtoto.
Inamkinga na magonjwa ya kuambukizwa.
Jitahidi upate kaka
 
Tunaendelea kununua ndege kwa sasa nyie wa chanjo subirini hamtakufa,on a serious note serikali haipeleki hela za kutosha wizara ya afya. Ndiyo maana kuna uhaba wa chanjo ,dawa, vitendea kazi pamoja na wahudumu wa afya huku ikiendelea kujinasibu kwa kuongeza budget ya afya kwenye makaratasi.
 
Ramadhan kareem kwa ndugu zangu waislamu,

Wakuu kuna hiki kitu nimekutana nacho huenda ni kawaida ila kwa miongo zaidi ya mitatu niliyopo hapa duniani ndio naona kwa mara ya kwanza.

Ni hivi, mke wangu kajifungua na ninavyojua (huenda nikawa sipo sahihi) kuna ile chanjo ya begani hua hua mtoto anachomwa pindi nanapozaliwa.

Sasa kwenye hiyo hospitali nimeambiwa chanjo hazipo tusubiri hadi tutakapotaarifiwa! Nikicheki naelekea wiki ya tatu sasa na hakuna taarifa yoyote juu ya uwepo wa chanjo hiyo na inasemekana hii ni kwa chanjo zote za watoto kwenye hiyo hospitali (hospitali ya wilaya) hazipo.

Sasa wasiwasi wangu ni Je! mtoto asipopata hizi chanjo KWA WAKATI au ASIPOPATA KABISA kunaweza kuwa na madhara gani?

cc Wizara ya Afya Tanzania
Kwani hizo chanjo hazitoki kwa mabeberu au tunazitengeneza sisi wenyewe.Tushambiwa vya mabeberu tuwaachie mabeberu wenyewe
 
Back
Top Bottom